INTERNATIONAL NEWS TODAY

Maneno mengine ya T B Joshua mwaka mmoja baada ya Jengo la Kanisa lake kuanguka..

Umepita mwaka mmoja sasahivi toka litokee tukio la kuanguka kwa Jengo la Kanisa la Synagogue Church of All Nations Nigeria ambalo linaongozwa na Mchungaji T B Joshua… kuna watu wengi walifariki katika tukio hilo na ilikuwa stori ambayo iligusa watu wengi kwa sababu ya umaarufu wa Mchungaji huyo nje ya mipaka ya Nigeria.
T B Joshua ameandika ujumbe unaogusa kumbukumbu ya tukio hilo, kwenye alichokisema kuna haya maneno pia >>> ‘Ni muhimu kukumbuka kwamba sisi ni Familia ya MUNGU, wakati mwingine kwenye mazingira kama haya tunatakiwa kumuachia MUNGU… Tunatakiwa kuamini kwamba vifo vya ndugu zetu ilikuwa ni mapenzi ya MUNGU, na haikuwezekana kupingana nao‘- T B Joshua.
3
Ajali ya kuanguka kwa Jengo la Kanisa hilo ilitokea September 12 2014, ambapo watu 115 walifariki na 84 kati yao walikuwa Raia wa South Africa.

Watu na Rekodi zao… Huyu kavuta Ndege kwa kutumia masikio yake tu !! 

Johnny Strange kutoka Uingereza, umri wake ni miaka 26, jina lake linaandikwa kwa wino mzito kwenye Kitabu cha Kumbukumbu kubwa Duniani, Guinness World Records baada ya kuandika Rekodi ambayo watu wengi wamebaki vinywa wazi wakimshangaa.
Strange kayafanya maajabu yake na Dunia itamkumbuka kwa rekodi nyingi alizowahi kuziandika ikiwemo hii mpya ya kuvuta ndege kwa kutumia masikio yake !!… YES, haikuwa kazi rahisi kwake lakini tayari ameikamilisha na Rekodi yake imeingizwa kwenye Kitabu cha Kumbukumbu za Guinness cha mwaka 2016.
Haikuwa kazi rahisi kufanikiwa kuandika Rekodi hii… Ninafurahia sana kuandika Rekodi mpya kila wakati na jina langu kuandikwa kwenye Kitabu cha Guinness, yani mpaka nakosa sehemu ya kutundika vyeti vyangu sasahivi‘– Johnny Strange.
STRANGE2
Johnny Strange na Cheti chake mkononi baada ya kuingia kwenye Kumbukumbu za Guinness mwaka 2016.
Ndege ambayo jamaa kaivuta ina uzito wa Kilo 670, na amefanikiwa kuivuta Ndege hiyo kwa umbali wa kama Mita 20 hivi… hii inakuwa ni mara ya nane kwake kuvunja rekodi na jina lake kuingia kwenye Kumbukumbu za Kitabu cha Guinness, rekodi ya kwanza aliivunja akiwa na umri wa miaka 10 tu.

 


 

Share on Google Plus

About Unknown

TEAM TASABA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment