
SIMULIZI-NEVER SAY GOODBYE
MTUNZI-VICTOR DISMAS
SEHEMU YA SABA
ILIPOISHIA
“okey nakuja”Yule mzee alisema na kusimama kuelekea upande wa ndani
Dominick alitumbua macho kumuona mzee akipandisha ngazi kuelekea ghorofa ya juu.Dominick aligeuza macho yake kwa Doreen aliyekuwa anatabasamu muda wote wakati yeye alikuwa anawaza ni jinsi gani ya kujiokoa kwani hali ilishaonekana kua mbaya
SONGA NAYO
Dominick hakujua afanye nini sababu Yule mzee aliondoka kwa kitisho huku akionyesha kwamba anaenda kuchukua kitu ndani.Baada ya akika kadhaa alishangaa kumuona Yule mzee akishuka kwenye ngazi huku mkononi akiwa ameshika kitu cheusi.Dominick hakujua ni kitu gani alichokishika Yule mzee sababu alikuwa amkibana kwa nyuma na kuonekana kidogo tu.
“eeh Mungu naomba uninusuru na ili balaa”Dominick alijisemea kimpoyomoyo huku akimuangalia Doeen aliyeonekana hana hata wasiwasi.
Kitendo cha Doreen kutokuonyesha wasiwasi kilizidi kumuogopesha Dominick na kuanza kuwaza kwamba Doreen ndiyo amemuuza kwa baba yake ali atolewe kafara.Akili ya Dominick ilimtuma kukimbia japo miguu yake ilikuwa inakataa kwani ilikuwa inatetemeka.Alichoamua ni kutulia ili kujua hatma yake ni nini sababu hata kama angekimbia asingeweza kutoka nje kutokana na ulinzi wa pale nje ulivyo, pia kulikuwa na ukuta mrefu uliozunguka nyumba nzima.
Wakati Dominick akiwaza hayo baba yake na Doreen alikuja na kukaa kwenye sofa huku akifungua kile kidude cheusi ambacho Dominick alijua ni bastora.Dominick alivutapumzi ndefu na kuiachia baada ya kuona baba yake na Doreen akitoa miwani kwenye kile kidude na kuivaa.Domiick aliamua kutabasamu kimoyomoyo japo jasho lilikuwa linamtoka kwa woga aliokuwa nao.
“ko ko ko Dominick kijana wangu”Yule mzee alikohoa na kumuhita Dominick
“naam”Dominick alihitika huku akijifuta jasho lililokuwa linamtoka
“kwanini unaogopa wakati Doreen alishaniambia kila kitu kuhusu wewe?Dominick,nampenda sana mwanangu Doreen,yeye ndiyo jicho langu kwa sasa,sitegemei kama utakuja kumuumiza au kumtesa.Doreen anakupenda sana kuliko unavyodhani.Mimi nimemruhusu kuwa na wewe bila kinyongo chochote sababu sipendi mwanangu akose furaha ambayo alikuwa anaikosa siku zote.Mimi ndiyo nilimuambia Doreen akuite siku ya leo ili nifanye mazungumzo na wewe na nikuulize swali langu moja tu,je upo tayari nikuulize?”Baba yake na Doreen aliongea kwa upole na kuuliza swali
“sawa mzee wangu unaweza kuniuliza”Dominick alisema
“je unampenda Doreen?”mzee aliuliza na kumfanya Dominick atabasamu huku akimuangalia Dominick aliyekuwa pembeni yake
“Nampenda sana Doreen baba”Dominick alisema kwa upole na kufanya Doreen machozi ya furaha yamdondoke
“naomba uilinde furaha ya mwanangu.Upendo uliopotea kati yangu na mama yake usije ukapotea kwako na kwake.Doreen mpende sana Dominick na mimi nawabariki kuanzia sasa”Mzee alisemana kufanya Dominick afurahi kupita maelezo kwani hakutegemea kama ataenda kukutana na kitu kama kile
Baada ya mazungumzo ya muda mrefu walikula na kunywa kwa pamoja huku kila mtu akionyesha furaha yake wazi wazi,Kwa kifupi kila mtu aliburudika siku ile.Dominick na Doreen walimuhaga mzee na kuondoka kurudi chuoni.
“Doreen leo nusu nusu nikimbie pale”Dominick alisema walipokuwa kwenye Tax kurudi chuoni
“kwanini?”Doreen aliuliza
“nilipoona mzee anashuka kwenye ngazi huku kashika kitu mkononi nilijua ni bastora kwahiyo nikajua kifo changu kipo miguuni mwangu kwahiyo nikataka kukimbia”Dominick alisema na kumuacha Doreen akicheka
“Dominick sikutaka tu kukuambia kwamba nilishaongea na baba kila kitu kuhusu wewe”Doreena alisema na kuegemea kwenye kifua cha Dominick
“una hatari wewe”Dominick alisema huku akitbasamu
Walipofika chuoni walihagana na kila mtu akaelekea kwenye chumba chake il kijandaa na mambo meninge ya chuoni.Dominick alipoingia chumbani kwake alkutana na rafiki zake wakiwa wanaongea.Alipoingia tu kila mtu alinyamaza kumuangalia yeye.Dominick aliingia huku akiwa anatabasamu na kufanya kila mtu awe anamshangaa pale chumbani
“mwanangu me nilijua hautorudi tena”Anthony alisema
“kwanini?”Dominick aliuliza
“niljua umeshapigwa risasi”Anthony alisema na kufanya Dominick atabasamu
“Anthony,sikutegemea kukutana na mzee mkamu kama baba yake na Doreen,japo mwanzani nilimuogopa lakini baadae nilikuja kumzoea na ugundua ni mtu mzuri sana kwangu
Dominick aliamua kuwaadithia kila kitu kilichotokea wakati yupo kwa kina Doreen,Story ile iliwavutia rafiki zake kwani waliona Dominick ni mwanaume mwenye bahati sana ,kwanza ya kupendwa na msichana mrembo Doreen pili kukubalika kirahisi nyumbani kwa kina Doreen
“kaka wewe ni mtu mwenye bahati sana,shukuru sana Mungu kwa kukupa bahati hiyo manake huyo Doreen watu walikuwa wanamshobokea lakini kwako amegoga mwamba kweli ndege mjanja ananasa kwenye tundu bovu”Rafael alisema
“hahahah kwahiyo mimi ni tundu bovu?”Dominick aliuliza
“hapana ila namaanisha kwamba,watu hawakutegemea kama Doreen anaweza akadata kwako”alisema Rafael na kufanya Dominick atikise kichwa
Siku zilisogea mpaka chuo kilipofungwa na kila mwanafunzi alirudi nyumbani kwao kwaajil ya likizo.Kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwa Dominick kuachana na Doreen kutokana na mazoea waliyowekeana kuonana kila siku.Likizo ilikuwa ni ya miezo mitatu kwahiyo ilikuwa inawatenganisha kwa Muda mrefu bila ya kuonana.
“Doreen mpenzi wangu acha tu nirudi nyumbani kwani hata mama yangu atakuwa amenikumbuka sana na hata mimi nimemkumbuka sana mama yangu,japo najua hii likizo itakuwa ndefu sana kwangu sababu nitakuwa mbali nawe ila nitajitahidi kuvumilia sana”Dominick alisema huku akimkumbatia Doreen huku akisubiri kupanda basi kuelekea kijijini kwao
“sawa Dominick hata mimi nitakukumbuka sana mpenzi wangu ila naomba uwe makini sana na usinisahau”Doreen alisema huku machozi yakimtoka
“miezi mitatu haiwezi kusababisha nikusahau mpenzi wangu na wala usiwe na wasi wasi tutakuwa tunawasiliana kila siku”.Dominick alisema kumtoa wasi wasi Doreen ambae alikuwa hataki kabisa Dominick aondoke
Baada ya kuzungumza sana Dominick alipanda kwenye basi huku akimuangalia Doreen aliyekuwa ananyoosha mkono kumuaga,Moyo wake ulimuuma sana kuachana na Doreen japo ilimbidi kufanya hivyo kwani ilikuwa ni lazima kwenda kuonana na mama yake.Taratibu gari lilianza kuondoka huku Dominick akichungulia dirishani na kumuona Doreen akiwa anamuangalia huku machozi yakimdondoka.Dominick hakuwa na lakusema zaid ya kumtupia busu la mbalimbali
“nenda salama mpenzi wangu”Doreen alisema kimoyo moyo kumuombea Dominick
“eehMungu naomba unifikishe salama na mpenzi wangu abaki salama”Dominick nae alisali kimoyomoyo kujiombea yeye na mpenzi wake
Taswira ya kuagana na Doreen ilijijenga kichwani na kukumbuka jinsi alivyokuwa anahagana na mama yake kipindi cha nyuma wakati anaenda chuo.Njia nzima Dominick alikuwa ametawaliwa na mawzo juu ya Doreen huku muda mwingine mawazo yake yakihamia kwa mama yake ambae alikuwa amemkumbuka sana kwa kipindi hicho.
“Doreen kwa heri,mama narudi mwanao”Dominick alisema na ghafla alishangaa kusikia mlio mkubwa chini ya gari alilopanda kuku gari likipepesuka na watu wakipiga kelele za kuomba msaada
“Mungu wangu tuokoe”Dominick alisema huku akiangalia watu waliokuwa wanapiga kelele
ITAENDELEA ………………..
Je ni nini kitatokea hapo?
Usikose sehemu inayofuata kujua ni kitu gani kilitokea hapo
LIKE,COMMENT NA SHARE
0 comments :
Post a Comment