TASABA SIMULIZI LA "NEVER SAY NEVER" SEHEMU YA NNE

SIMULIZI-NEVER SAY GOODBYE
MTUNZI-VICTOR DISMAS
SIMU(Watsaap)-0716616279
INSTAGRAM-VICTOR.DISMAS
FACEBOOK-Victor Dismas Van Manda
SEHEMU YA NNE
ILIPOISHIA
Dominic alikimbilia katika ule mgahawa ambao ulikuwa karibu yake kwa muda huo ili kusubiri mvua ikate.Mpaka anafika pale kwenye mgahawa alikuwa ameshalowa kidogo kitu kilichomfanya achukie sana na kulaani kwanini mvua imenyesha.Dominic wakati anajifutafuta alijikuta akishikwa bega na mikono milaini sana huku ikiambatana na sauti ya kike
“Hi”
“Hi”Dominic alihitika na kugeuza shingo yake
SONGA NYO
Macho ya Dominic yalikutana na msichana mrembo Doreen aliyekuwa amelowa kupita maelezo.Dominic alipigwa na bumbuwazi baada ya kumuona Doreen akionyesha tabasamu zuri na kufanya vishimo vijitokeze kwenye mashavu yake.Dominic aliendelea kumkodolea macho Doreen na kufanya Doreen aanze kuhisi aibu
“samahani kwa kukushika”Doreen alisema huku akitaka kuondoka
“usijali wala haujakosea”Dominic alisema huku akimshika mkono Doreen aliyekuwa anaondoka
Doreen aligeuka na kumuangalia Dominic aliyekuwa akitabasamu.Dominic nae alikuwa anamuangalia Doreen huku akisahau kumuachia mkono wake.Hakuna aliyediliki kuongea neno zaidi ya kutumbuliana macho na kuongea kwa kutumia macho
“naitwa Dominic”Dominic alifungua mdomo na kuongea
“naitwa……….”Doreen nae alianza kusema ila alikatishwa
“I know you(nakufahamu)”Dominic alisema
“how(kivipi)?”Doreen aliuliza
“nalifahamu jina lako”Dominic alisema huku akitabasamu
“okey,Can you be my friend(sawa ,unaweza kuwa rafiki yangu)?Doreen aliuliza
Dominic hakutegemea swali kama lile kutoka kwa Doreen,Msichana ambaye kila mwanaume alitamani kujenga urafiki nae.Dominic alijihisi kama yale maneno aliyokuwa anaambiwa ilikuwa ni ndoto tu ambayo muda siyo mrefu angeshtuka.Aligandisha macho yake na kuendelea kumuangalia Doreen aliyekuwa mbele yake
“Dominic”Doreen alihita kwa sauti nyororo
“naaam”Dominic alihitika huku akionekana kushtuka sana
“why don’t you answer my question(kwanini haujibu swali langu)?”Doreen alisema kwa upole
“yes,you can be my friend(ndiyo, unaweza kuwa rafiki yangu)”Dominic alisema bila hata ya yeye mwenyewe kudhani
“thanks Dominic,nice evining(asante Dominic,jioni njema)”Doreen alisema na kumpatia Dominic kikaratasi huku akianza kuondoka bila hata ya mvua kukata
“Goodbye Doreen(kwaheri Doreen)”Dominic alisema
“Dominic,never say goodbye because we will meet again(Dominic usiseme kwaheri sababu tutaonana tena)”Doreen alisema na kumfanya Dominic atabasamu
Doreen aliondoka huku akicheza kwenye mvua.Dominic alikuwa anamuangalia Doreen alivyokuwa anafanya kama mtoto mdogo.Moyo wa Dominic urifurahi kupita maelezo hasa baada ya kuongea na msichana mrembo ambaye kila mtu alikuwa anamtamani.Alikifungua kile kikaratasi na kukuta namba ya simu arafu kwa chini kulikuwa na maelezo yakiwa yameandikwa
“PLEASE CALL ME(tafadhari nipigie)”
“Nakupenda Doreen”Ilo ndiyo neno lililotoka katika kinywa cha Dominic huku akiendelea kumuangalia Doreen aliyekuwa anapotelea machoni mwake
Dominic alirudi chumbani kwao baada ya mvua kukatika.Kila mtu alimshangaa sana Dominic kwani alionekana akiwa na furaha sana kuliko siku nyingine.Mtu wa kwanza kumuhoji Dominic alikuwa ni Anthony
“vipi mbona leo una furaha sana?”Anthony aliuliza
“siwezi kuwaambia ila furaha yangu mtaiona siku moja”Dominic alisema
“yani unatubania kutuambia?”Edward aliuliza
“wala msijali siku ikifika nitawaambia”Dominic alisema dhuku akibadilisha nguo zake
Siku nazo ziliendelea kukatika bila ya Dominick kumtafuta Doreen,Dominick hakutaka kulifanya lile jambo kwa haraka sana sababu alijua madhara yake.
Siku moja Dominick alikuwa anaumwa marralia kwahiyo hakuweza kwenda darasani wala kutoka nje.Maralia ilimshika kisawa sawa na kumfanya akae kitandani kuugulia.Dominic aliamua kuchukua kile kikaratasi alichopewa na Doreen siku kadhaa zilizopita na kuanza kuzibonyeza zile namba kisha akaweka sikioni
“hallo”Sauti ya upande wa pili ilisema
“hallo Do……….”Dominic alikatisha kutaja jina kwani hakutaka watu wajue mtu anayeongea nae
“hey nani?”sauti ya upande wa pili iliuliza
“Dominic naongea”Dominic alijitambulisha
“wooow!!!!nafurahi sana Dominick kwa kunitafuta,kwanini ulikaa kimya siku zote hizo?”ilisikika sauti ya upande wa pili
“Sorry siwezi kuongea sana naumwa”Dominick alisema
“unaumwa?”sauti ya upande wapili iliuliza
“ndiyo naumwa
“please nielekeze ulipo nakuja kukuona”sauti ya upande wa pili ilisema
Dominic alielekeza chumba anachokaa kisha akakata simu.Wenzake walikuwa wanamuangalia sababu walikuwa hawajui anaongea na nani.Dominic alishajua wenzake wanafikiria nini kutokana na ukimya wake
“kaka ulikuwa unaongea na nani?”Anthony aliuliza
“usijali utamuona”ilo ndiyo lilikuwa jibu kutoka kwa Dominic
Kila mtu alikuwa na hamu sana ya kumuona ni mtu gani aliyekuwa anaongea na Dominick.Kila mtu alikuwa anahisi ni msichana ndiyo aliyekuwa anaongea na.Saa nazo zilikatika bila ya mtu yoyote kuingia pale chumbani
“kaka mbona huyo mtu mwenyewe hafiki?”Anthony aliuliza
Mara ulisikika mlango wa chumba chao ukigogwa taratibu.Aliyeenda kufungua mlango alikuwa ni Anthony ambae nusu azimie baada ya kumuona mtu ambae alikuwa hamtalajii kuja pale.Macho ya Anthony yalikuwa yameganda yakimuangalia Doreen akiwa ameshika mfuko mweusi huku akitabasamu
“samahani naweza kuingia ndani?”Doreen aliuliza
“humu?”Anthony nae aliuliza
“Ndiyo nimekuja kumuona Dominick”Doreen alisema na kumfanya Anthony ashikwe na bumbuwazi
Anthony alimpisha Doreen aingie ndani,Doreen aliingia na moja kwa moja alienda kukaa kwenye kitanda alicholala Dominick.
“pole Dominick”Doreen alisema huku akimbusu Dominick kwenye shavu na kufanya kila mtu asiamini tukio lile
“asante Doreen”Dominic alisema
Tangu Doreen alipoingia pale chumbani alisababisha wanaume wengi wawe wanainga pale chumbani kwaajili ya kumpa pole Dominick.Robo tatu ya watu waliokuwa wanaenda kumpa pole Dominick ilikuwa ni kwaajili ya kumuona Doreen ambae habari zilienea kwamba yupo pale hostel.Watu hawakuamini kama Dominick ana urafiki wa karibu na Doreen
“jamani hawa watu wametengeneza vipi urafiki?”jamaa mmoja aliuliza wenzake
“me mwenyewe nashangaa sana,Yule mwanamke ni mgumu sana”alisema mwingine
“ebu tuone mwisho wake”alisema Yule wa kwanza
Gumzo lilizidi kutapakaa baada ya Doreen kumlisha Dominick chakula.Hakuna aliyekuwa anaamini kama kijana huyo kutokea katika kijiji cha mgeta angeweza kujenga ukaribu wa haraka na msichana aliyeaminika kwamba ndiyo mrembo kuliko wasichana wote pale chuoni.Doreen alipamaliza kumlisha Dominick chakula alimpatia na ule mfuko ambao kulikuwa na matunda pamoja na juice
“Dominick nitakuja kukuona kesho”Doreen alisema
“asante Doreen,usiku mwema”Dominicka alisema
Hapo ndipo ukaribu kati ya Dominick na Doreen ulipoanza kukomaa.Doreen alimuhudumia Dominick mpaka alipopona kabisa.Kila mtu ndani ya chuo alianza kumuona Dominick kama mchawi baada ya kujenga ukaribu na Doreen.Anthony alikosa maneno ya kumuambia Dominick zaidi ya kumuangalia kwa macho ya wivu.
“Hivi Dominick umewezaje kumpata Doreen?”siku moja Anthony aliamua kuvunja ukimya na kumuuliza Dominick swali ilo
“Mimi sijampata Doreen na wala siyo mpenzi wangu ila ni urafiki tu wa kawaida”Dominick alisema huku akimuangalia Anthony kwa macho ya udadisi
“mh ni wanaume wengi sana walitamani kuwa na Doreen japo kwa urafiki wa kawaida lakini wameshindwa,mimi nahisi wewe utakuwa umetumia dawa”Anthony alisema huku akitoka nje
“kama fikra zako ndo zinakutumahivyo sawa ila ukweli naujua mimi”Dominick alisema na kujitupa itandani
Ukaribu wa Doreen na Dominick ulipamba moto huku kila mmoja akiwa na kitu kikubwa moyoni mwake ambacho alishindwa kumueleza mwenzake,Japo mwanaue ndiyo anatakiwa kuwa jasiri katika kumueleza mwanamke hisia zake lakini kwa Dominick haikuwa hivyo kwani bado alikuwa na zile aibu za kijijini.
Dominick”Doreen alihita siku moja walipokuwa wanapata chakula
“naam”Dominick alihitika
“nikikupa nafasi ya kuniambia neno lolote,utaniambia neno gani?”Doreen aliuliza
Ulikuwa mtihani mkubwa sana kwa Dominick kwani hakujua Doreen anamaanisha nini,Dominick alimkazia macho Doreen aliyekuwa mbele yake huku akionekana kama anakitu anataka kusema lakini alikuwa anashindwa.Doreen aliliona ilo kwa Dominick na kuamua kuvunja ukimya kwani Dominick alikuwa haongei kitu chochote
“Ongea Dominick”Doreen alisema kwa upole na kufanya mwii wa Dominic usisimke
“yapo mengi sana Doreen”Dominick alisema huku akimuangalia Doreen
“niambie neno moja tu ambalo litanifanya nijisikie vizuri maisha yangu yote”Doreen alisema huku akimkazia macho Dominick
“Nakupenda Doreen”Dominck alisema huku kijasho kikimtoka
ITAENDELEA………………………..
Je unataka kujua jibu alilolitoa Doreen?
Usikose sehemu inayofuata ili kujua nini kiliendelea hapo
Share on Google Plus

About Unknown

TEAM TASABA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment