SIMULIZI YA "NEVER SAY GOODBYE SEHEMU YA SITA",

SIMULIZI-NEVER SAY GOODBYE
MTUNZI-VICTOR DISMAS
SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA
“KIJANA NAONA UNAINGILIA ANGA ZA WAKUBWA ,SASA TUONE KAMA UTAMALIZA CHUO”ujumbe ulisomeka hivyo na mtumaji hakuandika jina lake
SONGA NAYO
Dominick aliurudia kuusoma ule ujumbe kila mara ili kuhakikisha yale maneno yaliyoandikwa mule.Hakujua ni mtu gani aliyeandika ule ujumbe na kumtumia sababu ile namba ilikuwa ni ngeni machoni mwake.Kingine kilichokuwa kinamuumiza kichwa ni anga gani anazowaingilia watu wakubwa na kwanini asimalize chuo?.Dominick alikosa raha kabisa ndani ya muda mfupi toka ule ujumbe utumwe.
“Dominick”Anthony alihita
“yap”Dominick alihitika na kumuangalia Anthony aliyekuwa na macho ya udadisi
“mbona umekuwa kimya ghafla?nini kimetokea?”Anthony aliuliza
“kuna mtu amenitumia ujumbe ambao umenitatiza na sijui ni nani”alisema Dominick huku akimkabidhi Anthony simu yake
Anthony alipokea ile simu na kuanza kusoma ule ujumbe kwa makini huku sura yake ikionekana kujenga makunyanzi.Alirudia kusoma mara tatu na kugeuza macho yake kwa Dominick aliyekuwa ameinama chini akitafakarii.
“ina maana huyu aliyetuma huu ujumbe haumjui?”aliuliza Anthony
“mimi simjui”Dominick alisema
“sasa atakuwa ni nani anayefanya hivi? Na kwanini usimalize chuo?”Anthony aliuliza
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..
Proffesor James Donald James alikuwa ni Proffesor kijana kabisa katika chuo kikuu cha Dares salaam.Proffesor aliyekuwa na taaluma ya siasa,Proffesor aliyekuwa na majivuno kila alipokuwa anatembea.Hiyo ilitokana na umri wake kuwa mdogo lakini alikuwa na elimu kubwa.Umri wa Proffesor huyo ulikuwa hauzidi miaka arobaini kwahiyo ulimfanya aonekane mtanashati machoni mwa watu.
Proffesor James alikuwa ni miongoni mwa watu waliotumia nguvu nyingi sana katika kumpata Doreen lakini aliambulia patupu.Alitumia kila mbinu ili ampate Doreen lakini bado alikutana na kizingiti kikubwa sana kutoka kwa msichana huyo mrembo.Proffesor James aliamua kutafuta mwanafunzi mmoja ambae alikuwa anasoma na Doreen kwaajili ya kumsaidia katika mipango yake ya kumpata Doreen alyeonekana kuwa na msimamo.
Yule mwanafunzi pamoja na Proffesor James walitumia kila haina ya mbinu kwaajiliya kumpata Doreen lakini ilishindikana kutokana na Doreen kutokuwa na mapenzi na huyo Proffesor.Kitendo cha kumkosa Doreen kilimuuma sana James huku akiapia lazima amkomeshe kwani ilikuwa ni fedhea sana kumkosa mwanafunzi kimapenzi.
“Doreen atanijua mimi ni nani”alisema Proffesor James alipokuwa na Yule kijana wake
“unataka kumfanya nini?”aliuliza Yule kijana
“nitahakikisha atafeli tu mitihani yake sababu mimi nafahamiana na walimu wake wote kwahiyo lazima nitamfanyia mchezo”alisema James huku akionekana kuwa na hasira za wazi wazi
“mkuu hapo utakuwa umekosea,kama kumpata utampata tu Doreen wewe endelea kuwa na subira tena ikiwezekana wewe ndyo uwashawishi walimu wake wamuongezee marks iliajue uwepo wako”alisema Yule kijana na kumfanya James atikise kichwa kukubali
“hapo umeongea jambo la msingi sana,ila huyu motto ni msumbufu sana”alisema James huku akitabasamu
James alifanya kila jambo lakini bado jibu alilokuwa analipata ni “hapana” kutoka kwa Doreen.Mwaka wa kwanza ukaisha na Doreen akaingia mwaka wa pili lakini mambo yalikuwa ni yale yale,hakukuwa na dalili yoyote ya kumpata Doreen.Tetesi za Doreen kuwa na mwanaume hapo chuoni ndizo zilimfumbua macho Proffesor James na kuona kwamba hatoweza kumpata Doreen tena
“hivi ni kweli Doreen ana mwanaume hapa chuoni?”alimuuliza kijana wake
“hizo ni taarifa za kweli”alisema Yule kijana huku akimuangalia Proffesor alivyokunja sura yake kwa hasira
“naomba unitafutie jina la huyo kijana,kitivo anachosoma pamoja na namba yake ya simu”alisema Proffesor James na kuagana na Yule kijana
Haikuwa kazi ngumu kupata taarifa za Dominick kwani alishatengeneza umaharufu pale chuoni baada ya kuanza mahusiano na Dominick.Yule kijana alifanya kama Proffesor alivyoagiza na kumpelekea taarifa zote.
“okey nitamkomesha huyu kijana hawezi kuingia anga za wakubwa”alisema Proffesor huku akiandika ujumbe kwenye simu yake kasha akautuma
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
Kichwa kilimuuma sana Dominick huku asijue ni kitu gani cha kufanya kwani alikuwa hajui ni anga gani amewaingilia watu.Anthony alibaki akimuangalia Dominick huku akimuonea huruma kwani hata yeye alikuwa bado anawazua ni anga gani alizoingia Dominick.Anthony alichukua tena simu ya Dominick na kuanza kuusoma tena ule ujumbe kasha akang’ata meno yake na kuanza kumtikisa Dominick.
“unasemaje Anthony”Dominick aliuliza kwa taratibu
“naweza nikawa nimepata mwanga wa hii message uliyotumiwa”alisema Anthony na kumfanya Dominick akae vizuri
“niambie ni mwanga gani ulioupata”alisema Dominick kwa shahuku
“Dominick rafiki yangu,Doreen ni msichana mzuri sana ambae kila mtu anatamani kuwanae,siyo wanafunzi tu wanaotamani kuwa na Doreen hata maproffesor nao wanafukuzia sana kwa Doreen.Inavyosemekana mahusiano yako na Doreen yamewafikia watu wengi sana katika chuo hiki,na siyo wote wanaopenda wewe uwe na Doreen.Mimi nahisi kuna Proffesor ndiyo atakuwa ameandika ujumbe huo japo sina uhakika”Anthony alisema kwa kirefu na kumuacha Dominick kjasho kikimtoka.
“sasa kama ni hivyo,e unanishauri niachane na Doreen?”Dominick aliuliza kinyonge
“je unampenda Doreen?”Anthony aliuliza
“Nampenda sana Doreen”Dominick alijibu kwa kifupi
“sasa utawezaje kumuacha mtu ambae unampenda?,usijaribu kufanya hivyo wewe endelea kuwa na Doreen”Anthony alisema na kumuacha Dominick akiwa kimya
Wakati wanaendelea kuongea simu ya Dominick ilianza kuhita na mpigaji alikuwa ni Doreen,Dominick alisogea pembeni ili kusikiliza ni kitu gani Doreen anachotaka kumuambia
“hellow ma love”Dominick alisema baada ya kupokea simu
“Dominick nimekupigia ili nikutakie usiku mwema,arafu kesho nataka unisindikize nyumbuni kwetu”Doreen aliema na kufanya Dominick ashtuke
“nyumbani kwenu!!!?”Dominick aliuliza kwa mshangao
“ndio nyumbani kwetu na wala usiwe na wasiwasi mpenzi wangu”Doreen alisema
“sawa nitakusindikiza”Dominick alisema kasha wakaagana na kukata simu
Dominick alikuwa mnyonge sababu hakujua ni kwanini Doreen anataka kumpeleka nyumbani kwao.Wasiwasi aliokuwa nao Dominick ulimmfanya Anthony awe na shahuku la kutaka kujua ni kitu gani alichokuwa anazungumza na Doreen
“mbona unatetemeka?”Anthony aliuliza
“Doreen anataka nimpeleke nyumbani kwao kesho”Dominick alisema
“kuwa makini rafki yangu si unajua watoto wa kishua wazazi wao walivyo”Anthony alisema na kutoka nje
Usiku mzima Dominick aliutumia kuwaza kwani haujua hatma yake na Doreen kutokana na vitisho vya ule ujumbe wa simu aliotumiwa.Baada ya kuwaza sana hatimae usingizi ulimpitia na kulala.Asubuhii alichelewa sana kuamka na kujikuta akiamshwa kwa kutikiswa na mtu.Taratibu alifumbua macho yake na kukutana na sura nzuri ya mrembo Doreen ikiwa imeachia tabasamu zuri
“Dominick unalala mpaka sasa hivi?”Doreen aliuliza
“kwani sasa hivi saa ngapi?”Dominick aliliza
“saa nne na nusu”Doreen alijibu
“ila jana nilichelewa sana kulala ndiyo maana nimechelewa kuamka”Dominick alisema
“basi amka ujiandae unisindikize ile safari niliyokuambia jana”Doreen alisema
“sawa ngoja nijiandae japo jana sikujua kama tutaondoka muda huu”Dominick alisema na kwenda bafuni kujiandaa
Baada ya dakika kadhaa walianza safari ya kuelekea nyumbani kwa kina Doreen kwa kutumia Tax.Moyoni Dominick alikuwa amebeba maswali mengi sana kwani hakujua anaenda kufanya nini huko kwa kina Doreen.Aliogopa sana wazee wenye pesa kwasababu ni watumizi wazuri sana wa bastora hasa unapocheza na watoto wao.
“Doreen kwani kwenu tunaenda kufanya nini?”Dominick aliuliza
“kuna kitu naenda kuchukua arafu tutarudi chuoni”Doren alisema huku akitabasamu
“baba yako hayupo nyumbani?”Dominick aliuliza tena
“baba hayupo nyumbani leo na hata kama akiwepo sidhani kama kuna ubaya wowote”Doreen alisema
“Doreen unataka kunifanya mbuzi wa kafara leo?”Dominick aliuliza
“kwanini unasema hivyo?”
“wazee wenye pesa uwa wana mkono mwepesi sana wa kutumia bunduki”Dominick alisema na kumfanya Doreen acheke
Wakati wanaendelea na maongezi gari lilikuwa limeshafika kwenye jumba kubwa na la kifahari maeneo ya mbezi beach.Geti lilifunguliwa na mlinzi aliyekuwa amevalia sare huku mkononi mwake akiwa ameshika bunduki.yule mlinzi alisalimiana na Doreen kisha gari likaingia ndani na Doreen ndiyo alikuwa wa kwanza kushuka.
“Karibu nyumbani kwetu Dominick”Doreen alisema
“asante sana”Dominick alisema huku akkodoa macho kuangalia jumba kubwa lililokuwa mbele yake
Taratibu walianza kuelekea ndani huku Dominick akiendelea kuangalia madhari nzuri ya ile nyumba.Katika maisha yake yote hakuwahi kuingia kwenye jumba kubwa kama lile.Moyoni bado alikuwa na wasiwasi kama likitokea tatizo humo ndani wapi angekiimbilia kwasababu ukuta wa ile nyumba ulikuwa mrefu kwahiyo ilikuwa ni vigumu sana kwa mtu kuruka.
“eeh Mungu nisaidie”Dominick alijisemea kimoyo moyo
Baada ya kuingia ndani alikaribishwa kwenye sofa na kukaa.Doreen alienda kwenye Jokofu kwaajili ya kumchukulia juisi.Wakati Dominick akiwa amekaa kwa wasiwasi pale kwenye sofa alisikia mlango wa kutokea nje ukifunguliwa.Macho ya Dominick yaliutana na macho ya kipande cha mtu kikiingia pale sebuleni huku akiwa ameshika gazeti kubwa mkononi.
“shikamoo Dady”ilikuwa ni sauti ya Doreen ndiyo iliyomzibua masikio Dominick na kujiona yupo nusu nusu,nusu mtu nusu mfu
“Mungu wangu nakufa leo”Dominick alijisemea kimoyo moyo
Dominick alimsalimia Yule mzee japo kwa uoga sana.Baba yake na Doreen alihitikia ile salamu ya Dominick na kukaa kwenye sofa la pembeni huku macho yake yakiwa yanamuangalia Dominick.Dominick alijitahidi sana kujikaza lakini jasho lilikuwa linatoka japokuwa kulikuwa na Ac.
“Dady huyu ni rafiki yangu anaitwa Dominick”Doreen alisema kumtambulisha Dominick
“ni rafiki yako?”Yule mzee aliuliza
“ndiyo Dady”Doreen alisema
“okey nakuja”Yule mzee alisema na kusimama kuelekea upande wa ndani
Dominick alitumbua macho kumuona mzee akipandisha ngazi kuelekea ghorofa ya juu.Dominick aligeuza macho yake kwa Doreen aliyekuwa anatabasamu muda wote wakati yeye alikuwa anawaza ni jinsi gani ya kujiokoa kwani hali ilishaonekana kua mbaya
ITAENDELEA…………………………………………
Je unahisi baba yake na Doreen amefuata nini Ndani?
Usikose sehemu inayofuata ili kujua nini kiliendelea

Share on Google Plus

About Unknown

TEAM TASABA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment