SIMULIZI; YAATIMA
MTUNZI; Pascal Pahali
Email;pascalpahali@rocketmail.com
Contact;+255655-123 103
WhatsApp;+255655-123 103
Instagram; santiano del pahali
LIKE ILINIPOST SEHEMU INAYOFUATA
SEHEMU YA I
UTANGULIZI
YAATIMA huyu ni msichana mwenye asili ya kitanzania mchanganyiko na kichina.Msichana huyu tangu utoto wake amekulia mikononi mwa mama yake kipenzi Salome.Msichana huyu hakubahatika kukutana na malezi ya baba yake tokea utoto wake mpaka sasa kakuwa na kuwa mtu mzima
ANZA NAYO
Katika kijiji cha Lugoba mkoani Pwani alitokea mama mmoja aliyefahamika kwa jina la Salome.Salome aliishi na mama yake kijijini hapo kwa muda wote wa maisha yake.Familia ya kina Salome ilikuwa na maisha duni sana ambapo hata kupata chakula chao ilikuwa ni tatizo.Mama huyu alibahatika kupata mtoto mmoja wa kike ambaye alimuita jina la Yaatima.Yaatima aliishi na mama yake na bibi yake kijijini hapo.Maisha ya msichana Yaatima yalikumbwa na misukosuko ya kila aina ambapo msichana huyu alipofikisha umri wa kwenda shule alishindwa kabisa.Mama yake Yaatima alikuwa akijihangaisha huku na huko walau kutafuta riziki katika familia ile ambayo ilikuwa na wakazi watatu tu yaani Yaatima, mama yake na bibi yake.Kwakuwa umri wa bibi yake Yaatima ulikuwa umeenda sana bibi huyo alishindwa kujishughulisha na shughuli yoyote ambayo ingewasaidia kupata riziki na kwakuwa umri wa Yaatima kuwa mdogo hakuweza kutafuta riziki pia.Kwahiyo basi mama yake Yaatima ambaye alikuwa bado ana nguvu alijihangaisha kutafuta riziki na kushindwa kumsimamia mwanae Yaatima kuhudhuria shule.Mama yake Yaatima kwa bahati mbaya naye hakubahatika kupata elimu huko nyuma kwahiyo naye pia hakutambua umuhimu wowote wa elimu.
Mama yake Yaatima alipata riziki yake kwa shida sana.Siku moja moja alikuwa akienda soko la mahindi na kuokota mahindi yaliyokuwa yamedondoka chini na kuwapa wenye mahindi na kisha wao kumpa mahindi kidogo tu na kiasi kidogo cha fedha.Mama yake Yaatima alichukua mahindi hayo na kuyapeleka mashineni ambapo yalibanguliwa na kuwa unga ambao ndiyo ulikuwa ukitumiwa pale nyumbani kwao.Na kiasi kile cha pesa alichokuwa akipewa alitumia kwa mahitaji mbalimbali kama kununua maji, sabuni, na mahitaji madogo madogo yaliyokuwa yakihatajika ndani ya nyumba.Familia hii iliishi kwa dhiki sana hata ilipokuwa ikifika mtu mmoja wao kuugua mule ndani familia hii ilishindwa kumpeleka mgonjwa hospital au kununua dawa.Kipindi kigumu kwa familia hii ni pale msimu wa mahindi sokoni ulipokuwa ukiisha familia hii ilitia sana huruma.Kipindi hicho mama Yaatima alilazimika kuamka asubuhi sana na kuzunguka kwa baadhi ya watu pale kijijini ambao walikuwa wanauafadhari kimaisha na kuomba nguo zao na kuwafulia.Kule alipokuwa akienda kufua alikuwa akiomba vyakula vilivyokuwa vimebakia na kuvikusanya kwenye mifuko ya rambo na kuvileta nyumbani na kisha kuvipasha na kuwapa mama yake na mwanaye kipenzi Yaatima.Familia hii iliendelea kuishi maisha hayo na kutokuwa kabisa na tumaini la baadaye kwani hakukuwa na mtu hata mmoja aliyejaribu kuwasaidia na pia katika familia yao hakukuwa na mtu aliyeenda shule ambaye ndiyo ingekuwa tumaini la familia yao ya baadaye.
Yaatima aliendelea kukua japo kwa misukosuko na shida nyingi lakini Mungu mkubwa siku zilisogea na umri kwa Yaatima ulisogea.Katika kucheza kwake Yaatima alisikia marafiki zake pale mtaani wakiliita jina la baba.Yaatima alishangaa maana tangu utoto wake pale nyumbani kwao hakuwahi kusikia jina hilo zaidi ya jina la mama na bibi tu.Kitu hiki kilimuumiza sana Yaatima.Yaatima alijiongelea moyoni ipo siku kitu hiki nitakuja nimuulize mama yangu na kama mama hatotaka kuniambia basi nitamuuliza bibi yangu maana bibi yangu ananipenda sana.Siku moja asubuhi Yaatima kama alipatwa na kitu fulani maana alivyoamka tu alianza kuita baba.Mama yake Yaatima siku hiyo alichelewa kwenda kazini kwahiyo Yaatima alitumia fursa hiyo kumuuliza mama yake habari za baba yake.Lakini kila alipojaribu kumuuliza mama yake alipuuzia na kufanya kutokulisikia swali la binti yake Yaatima.Binti yule alianza kulia sana na kujua hiyo ndiyo njia sahihi ya mama yake kumsikiliza.Yaatima alifaulu mtego huo na ndipo mama yake kusimamisha shughuli aliyokuwa akiifanya na kuanza kumsikiliza mwanaye Yaatima.Nini tatizo mama yangu kipenzi Yaatima? Mama aliuliza.Naomba uniambie baba yangu yupo wapi? Yaatima mwanangu naomba unyamaze na habari za baba yako nitakwambia ukishakuwa mkubwa sawa? Yaatima alikataa katu katu na kudai anaomba aambiwe muda ule.Mama yake Yaatima alikaa kitako na kumwambia Yaatima mwanangu naomba unisikilize kwa makini sana.Ukiwa bado………………..
Itaendelea>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Yaatima mwanangu naomba habari hizi nikusimulie siku ukiwa mkubwa.Yaatima alikataa katu katu na kuomba mama yake amsimulie siku ile.Kujua kilichotokea baada ya mama yake Yaatima kukaa kitako endelea kufuatilia simulizi hii

0 comments :
Post a Comment