LIKE NIKUTUMIE INBOX
SIMULIZI-NEVER SAY GOODBYE
MTUNZI-VICTOR DISMAS
SIMU(Watsaap)-0716616279
INSTAGRAM-VICTOR.DISMAS
FACEBOOK-Victor Dismas Van Manda
SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA
“Goodbye(kwaherini)”Doreen alisema kuwaaga huku akivuta hatua
“sorry Doreen(samahani Doreen)”silisikika sauti nyingine ngeni katika masikio ya Doreen ikimuomba radhi,Si mwingine bali alikuwa ni Dominic aliyetamka neno lile na kumfnya mpaka Anthony amuangalie sababu hakujua ni kitu gani anachotaka kuzungumza wakakti muda wote alikuwa kimya
SONGA NAYO
“What?”Doreen aliuliza huku akiacha kutembea,wakati huo Dominic nae alikuwa amesimama
“Never say Goodbye(usiseme kwaheri)”Dominic alisema na kumfanya kila mtu apatwe na mshangao
“why(kwanini)?”aliuliza Doreen
“word Goodbye means that we won’t meet again(neno kwaheri linamaanisha kwamba hatutoonana tena)”Dominic alisema na kumpa mkono Doreen
Doreen alinyoosha mkono wake bila hata ya kutarajia na kumpa Dominic,Doreen alitoa tabasamu huku Dominic akilijibu lile tabasamu kwa tabasamu mara dufu.Walishikana mikono kwa sekunde kadhaa bila hata ya kuachiana kitu kilichomfanya Anthony ashikwe na bumbuwazi sababu lile suala lilikuwa geni kwa msichana mrembo kama Doreen kushikana muda wote mkono na Dominic au na mvulana mwingine
“okey nimekuelewa,kwahiyo nisemeje?”Doreen aliuliza huku akiweka nywele zake vizuri
Uzuri wa Doreen ulimchanganya sana Dominic na kujikuta akishindwa kuongea neno lingine zaidi ya kumkodolea macho Doreen.Doreen alitabasamu kisha akamshika mwenzake na kuondoka.Hule muondoko wa Doreen ulizidi kumchanganya Dominic na kujikuta macho yake yakiganda bila hata ya kupepeseka,Doreen nae alionekana akigeuka nyuma kumuangalia Dominic huku akitikisa kichwa
“baba vipi mbona hivyo?”Dominic alishtuliwa na sauti ya Anthony
“hakuna kitu”Dominic alisema na kubeba begi lake
Waliongozana na Anthony mpaka chumbani kwao na kila mtu alijitupa kitandani kwake,Dominic alionekana ni mwingi kwenye mawazo tangu alipomuona Doreen kwa siku hiyo.Uzur wa msichana huyo ulionekana kumchanganya sana Dominic na kujikuta taratibu akianza kuvutiwa na mrembo huyo.Msichana ambae kila mwanaume alikuwa na hamu ya kuwa nae hata kwa siku mbili tu ili apate sifa kati ya watu waliyommiliki Doreen
“Hivi huyu Doreen ni mtu au jinni?”Dominic alijiuliza
********************************************************************************************************************
Doreen siyo jinni bali ni mtoto aliyezaliwa kwenye familia ya kitajiri.Mama yake na Doreen alikuwa ni Balozi wa Tanzania Nchini Canada,Baba yake na Doreen alikuwa mfanya biashara mkubwa nchini Tanzania.Biashara zake zilimuwezesha kumuingizia hela nyingi na kufanya kuwa kati ya watu matajiri katika nchi ya Tanzania.Familia yao ilikuwa na kila sifa ya kuitwa familia bora.
Katika familia hiyo kulikuwa na Watoto wawili tu ambao ni Doreen na kaka yake wa kiume aliyejulikana na kwa jila la David.Familia yao ilikuwa na furaha na kufanya watoto wao wawe katika maisha bora huku afya zao zikionekana kuwa njema.Maisha ya furaha yalitawala katika nyumba yao na kusababisha utajiri uweze kuongezeka katika nyumba yao japo kulikuwa na ubaguzi kidogo katika malezi ya watoto.
Kitu kilichoshangaza wengi ni Doreen kumpenda sana baba yake kuliko mama yake.Hiyo ilitokana na mama yake kumpa kipaumbele sana David kuliko yeye.Mama yake na Doreen alimpenda sana David kuliko hata Doreen kitu kilichosababisha mapenzi katika familia hiyo yaanze kupungua
“mke wangu kwanini unaonyesha wazi kumchukia mtoto?”mumewe alimuuliza siku moja wakiwa chumbani kwao
“hapana mimi simchukii mwanangu ila kusema ukweli nampenda sana David kutokana nimemzaa kwa tabu sana na nadhani unalijua ilo”alisema mkewe
“hata kama ni hivyo basi usionyeshe utofauti mpaka mtoto ajue”Baba yake Doreen alimuambia mkewe
“sawa mume wangu”mkewe aliitika
Japo Doreen alionekana mzuri kupita maelezo lakini moyoni mwake alitawaliwa na chuki kali sana kwa mama yake,Chuki iliyokuwa inamfanya akatae kabisa kumuona mama yake.Japo baba yake alijitahidi kurudisha mahusiano mazuri lakini alishindwa.
Mgogoro uliokuwepo kati ya Doreen na mama yake ulisababisha mzee Danford ashindwe kuvumilia.Mzee Danford aliamua kutengana na mke wake ili kupunguza migogoro ambayo ilikuwa haiishi kila walipokuwa wanazungumzia suala la Doreen.Mzee Danford aliamua kuishi nchini Tanzania na Doreen huku mkewe akiishi nchini Canada na mtoto wake wa kiume.
Mzee Danford alitumia kila aina ya mbinu kumfanya Doreen ajisikie na amani sababu hakutaka mtoto wake ajisikie vibaya wakati yeye yupo.Alimpatia kila kitu alichookuwa anakitaka ili Doreen alidhike.Doreen nae alizidisha mapenzi kwa baba yake na kujikuta akiwa na amani kuliko alivyokuwa na mama yake
Uzuri aliokuwa nao Doreen uliwachanganya wavulana wengi hasa wale aliokuwa anasoma nao shule ya secondary.Doreen alikuwa ni msichana mzuri sana kuanzia juu mpaka chini.Alikuwa na sura nzuri iliyopambwa na macho ya wastani ambayo hayakuwa madogo wala makubwa,Doreen alipewa mdomo wenye lips nzuri kitu kilichofanya awe anavutia kila alipokuwa akitabasamu.Katikati ya mdomo na macho kulikuwa na pua nzuri iliyonogesha urembo wake
Doreen alikuwa na shingo ndefu kidogo iliyokuwa inaongeza maringo kila alipokuwa anatembea.Kifuani alikuwa na muonekano mzuri hiyo kutokana kubeba chuchu za wastani ambazo zilikuwa zimetengeneza uwiano mzuri na umbo lake.Doreen alikuwa na umbo namba nane kitu kilichofanya wanaume wengi wakware wampigie misele huku wakiambulia patupu.
“Doreen nakupenda sana na nitafurahi sana kama ukinipa nafasi katika moyo wako”hizo zilikuwa kauli za wanaume waliovutiwa na Doreen
Doreen hakuwa na jibu lingine kwa mwanaume wa namna hiyo zaidi ya jibu la “Hapana”,Japo kuwa alikuwa anapata tabu sana kutoka kwa wanaume lakini Doreen alijitahidi kuwakwepa mpaka alipofanikiwa kumaliza elimu yake ya secondary na kujiunga na chuo kikuu cha Da es salaam.
Doreen alipojiunga na chuo kikuu alisababisha mtafaruku mkubwa sana kwa wanaume ambao walionekana kuchanganyikiwa kila walipokuwa wanamuona.Doreen aliamua kukaa hostel ndani ya chuo kutokana na kuwa mpweke akiwa nyumbani kwao.Wanaume wengi walijitahidi sana kurusha nduano zao ili kumnasa Doreen lakini waliambulia patupu,Doreen alisimamamia msimamo wake wa kutokuwa na mwanaume ili asije akaipoteza heshima yake ambayo alitaka kuja kumpatia mume wake wa ndoa.
“Doreen kiukweli mimi nakupenda kutoka moyoni na ukikubali nitakupa kitu chochote unachokitaka”kijana mmoja aliyesemekana ni mtoto wa tajiri alisikika akimuambia Doreen
“hapana John mimi sipo tayari kuwa na mwanaume kwa sasa na kama ukiendelea kuniambia maneno hayo,sidhani kama nitakuwa nakusalimia tena”Doreen alisema bila hata ya kupepesa macho
Wanaume wengi walianza kumchukia Doreen kwa msimamo wake huo.Doreen hakuogopa wanaume waliokuwa wanamchukia bali aliwaona kama wapumbavu.Mwaka wa kwanza ulikatika na kuwa kati ya wanafunzi waliobahatika kuingia mwaka wapili.
Doreen haikuwahi kutokea hata siku moja akajenga urafiki na mwanaume katika chuo hicho.Lakin siku moja Doreen aliongea maneno ambayo yalimuacha hoi rafiki yake na kumfanya aanze kumshangaa.Maneno hayo aliyaongea siku chache baada ya kukutana na Dominic katika mgahawa wa chuo
“Jack Yule kaka tuliyekaa nae pale kwenye mgahawa natamani sana awe rafiki yangu”Doreen alimuambia rafiki yake
“Yule kaka aliyekuwa anaongea sana?”Jackline aliuliza
“hapana Yule mwenzake aliyekuwa kimya mda wote”Doreen alisema akimaanisha Dominic
“si Yule aliyesema Never say goodbye(kamwe usiseme kwaheri)?”aliuliza Jackline
“ndiyo huyo”Doreen alisema
“kwanini umetaka awe rafiki yako?”aliuliza Jackline
“me nimependa tu na sijui kwanini”alisema Doreen na kumfanya Jkline amshangae
“sasa utampataje na mwanaume mwenyewe ni mgeni pale chuoni na watu wengi hawamjui?”aliuliza Jackline
“Nahisi tutakutana”Doreen alisema na kujifunika shuka lake kulala huku akitabasamu
**********************************************************************************************************************
Dominic alionekana kuchanganyikiwa tangu siku aliyomuona Doreen.Dominic alitamani sana kumuona Doreen kwa mara nyingine ili roho yake ilidhike hata kama atapata muda wa kuongea nae.Zilikuwa haziwezi kupita dakika kumi bila ya Dominic kumuwaza Doreen,msichana aliyetokea kuiteka nafsi yake tangu alipomuona,msichana aliyetaka kubadilisha msimamo wake wa kutokuwa na msichana pale chuoni.
“Anthony uliyokuwa unasema ni ya ukweli”Dominic alimuambia Anthony
“kuhusu nini?”Anthony aliuliza
“Doreen ni msichna mzuri sana”Dominic alisema na kusababisha Anthony acheke sana mpaka machozi yakawa yanamtoka
“unacheka nini sasa?”Dominic aliuliza huku akikunja uso
“wewe ulidhani nilivyokuambia kwamba Doreen ni malkia wa chuo nilikuwa nadanganya?”Anthony aliuliza huku akijifuta machozi kwa kitambaa
“nilijua ni wa kawaida tu ila tangu nimemuona nimejikuta moyo wangu ukiingiwa na kitu”Dominic alisema kwa hisia
“unamaanisha umempenda ?”Anthony aliuliza
“ndiyo nimempenda sana”Dominic alisema na kumuangalia Anthony aliyeonekana kuwa makini sana kumsikiliza Dominic
“Dominic wala usijisumbue kumfuatilia Doreen,Sidhani kama utaweza kumpata.Doreen ni msichana wa matawi ya juu sana na watu wengi wenye fedha zao wamemfuata lakini wameambulia patupu.Vilevile Doreen hawezi kuwa na mwanaume wa mwaka wa kwanza ,Sisi wenyewe wajanja wa mji tunaambulia patupu sembuse wewe”Anthony alisema kwa kirefu na kumfanya Dominic akate tamaa
“hapo Anthony umesema ukweli,acha tu niendelee na masomo yangu”Dominic alisema kwa kukata tama
Siku nazo zilikuwa zinakimbia huku Dominic akiendelea na masomo yake kama kawaida.Dominic alifuta mawazo juu ya Doreen na kukazania masomo yake.Tangu walipoonana siku ile ya kwanza Dominic hakupata bahati ya kumuona Doreen kwa mara ya pili.Dominic alifuta kabisa mawazo juu ya Doreen kutokana na maneno aliyoambiwa na Anthony
Kuna siku wingu lilitanda sana angani na kuonyesha dalili ya mvua kunyesha muda mchache unaofuata.Baada ya dakika kadhaa mvua kubwa ilianza kunyesha na kila mwanafunzi alianza kutafuta sehemu ambayo anaweza kujikinga na mvua.Dominic alikuwa ni miongoni mwa watu hao waliokuwa wanakimbia kujikinga na mvua
Dominic alikimbilia katika ule mgahawa ambao ulikuwa karibu yake kwa muda huo ili kusubiri mvua ikate.Mpaka anafika pale kwenye mgahawa alikuwa ameshalowa kidogo kitu kilichomfanya achukie sana na kulaani kwanini mvua imenyesha.Dominic wakati anajifutafuta alijikuta akishikwa bega na mikono milaini sana huku ikiambatana na sauti ya kike
“Hi”
“Hi”Dominic alihitika na kugeuza shingo yake
ITAENDELEA………………………….
Je ni nani aliyemshika bega Dominick?
Usikose kusoma simulizi hii ya kusisimua kwani utajifunza mengi sana
LIKE ,COMMENT NA SHARE II TUSONGE

0 comments :
Post a Comment