TASABA HABARI ZA MICHEZO LEO

Sababu iliyofanya Wayne Rooney kuchezea Everton August 2 hii hapa

_84630948_roo-2
Mshambuliaji na nahodha wa Manchester United Wayne Rooney amewahi kuchezea klabu ya Everton ya Uingereza kabla ya mwaka 2004 kuhamia katika klabu ya Manchester United kwa ada ya uhamisho ya pound milioni 25, akiwa na Everton Rooney aliichezea mechi 77.
r1
Rooney amerejea tena August 2 katika jezi ya Everton na mtu aliyemsababisha avae jezi hiyo ni Duncan Ferguson ambae ni mchezaji wa zamani wa Everton aliyewahi kuchezea klabu hiyo mwaka 2000-2006. Duncan ni miongoni mwa wakongwe waliocheza na Rooney katika klabu hiyo na uliandaliwa mchezo wa heshima kwa ajili yake licha ya kuwa alistaafu toka mwaka 2006.
Duncan-Fergusons-Testimonial
Mbele ya mashabiki 34,718 ambao walitoa heshima kwa Rooney kwa kusimama wakati anaingia uwanjani dakika 15 za mwisho katika mchezo wa Everton wa kirafiki dhidi ya klabu ya Villarreal ambao waliibuka na ushindi wa goli 2-1, kitu ambacho huwa ni ishara ya kuheshimika sana kama Uwanja mzima umesimama kwa ajili ya kumpa heshima Rooney ya kurejea tena Goodson Park baada ya miaka 11.
2015-08-03_spo_11649336_I1
Duncan ambae ndiye mlengwa wa mchezo huo aliingia uwanjani dakika 7 za mwisho.
Hapo chini nimekusogezea picha Wayne Rooney na Duncan Ferguson walipokuwa wanacheza pamoja zaidi ya miaka 1o iliyopita 
2AB3551E00000578-0-image-m-4_1437408254974
2AB354F200000578-0-image-a-1_1437408233567

Hii ni good news kwa mashabiki wa kike wa Manchester United (Pichaz)

446407-e9b0defc-395f-11e5-b9fd-ad0b337aa4fa
Siku kadhaa zimepita toka klabu ya Manchester United ya Uingereza itangaze jezi zake mpya na kampuni itakayokuwa inatengeneza jezi hizo, August 3 nimekutana na story nyingine tena kwa ajili ya mashabiki wa kike wanaoipenda Mancheater United… Zamani tulizoea kuona mashabiki wa kike wa Manchester United Tanzania na hata Uingereza wakivaa jezi za kiume wanapoenda uwanjani na sehemu zingine za kutazamia mechi kwa njia ya TV.
shirt-comp
Manchester United hawakuishia tu kutengeneza jezi za kiume zitakazotumiwa na wachezaji na mashabiki wa kiume, kampuni ya ADIDAS ambayo ndio yenye mkataba na Man United katika kipindi cha miaka 13 ijayo, imetoa jezi kwa ajili ya mashabiki wa kike.
f17786fa-2ebf-4764-ad56-105a96d9775c_16x9_600x338
Kushoto ni jezi ya Kike na upande wa kulia ni jezi ya kiume
Man United wameingia mkataba wa miaka 13 wenye thamani ya pound milioni 750 na kampuni ya vifaa vya michezo ya Kijerumani ADIDAS baada ya mkataba wa miaka 10 na kampuni ya Nike kumalizika.
446407-e9b0defc-395f-11e5-b9fd-ad0b337aa4fa

Ni kweli baba mzazi alimzuia Msuva kusaini Yanga kisa ni shabiki wa Simba?

Mwanzoni mwa mwezi July kulikuwa na habari mbalimbali zilizoweka headlines katika mitandao ya kijamii kuhusu mchezaji wa Yanga Simon Msuva na baba yake Mzee Msuva, kila mtu alikuwa anazungumza kuhusiana na Simon Msuva.

August 3 Simon Msuva aliongea na millardayo.com na kuweka wazi kuhusiana na taarifa za yeye kupuuza ushauri wa baba yake, awali kulikuwa na uvumi kuwa baba yake Simon Msuva alimshauri aondoke Yanga na kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine hususani klabu ya Simba ambayo baba yake ndio klabu anayoipenda.
msuvaMsuva amezungumzia hizo taarifa za baba yake kutaka aondoke Yanga >>> “kiukweli Mzee anamapungufu yake siwezi kumuongelea sana sababu yeye sio mtu anayeniongelea mimi, mtu anayeniongelea mimi ni Management yangu ambayo inaweza ikaongea kila kitu kuhusu mimi”

“kwa hiyo mzee anaweza ongea chochote kama mzazi, mzee kama mzee anaweza akawa kaongea ila watu wakamuelewa vingine. Mzee hawezi kuongea sitaki mwanangu acheze Yanga  aende nje au acheze Simba hicho kitu nakataa inawezekana waandishi labda wakawa wamemuuliza hivyo inategemea si unajua waandishi wanavyouliza ” >>> Simon Msuva
IMGS6569

Picha: Hivi ndivyo ilivyokuwa ndoa ya wakala wa Ronaldo, mastaa waliohudhuria.

Hatimaye wakala namba moja wa wanasoka bora ulimwenguni, Jorge Mendes jana alifunga ndoa na mchumba wake wa siku, Sandra Barbosa.
 
Sherehe ya ndoa ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali wa soka ulimwenguni, huku Cristiano Ronaldo, mteja mkuu wa Mendes akiwa ‘mpambe rasmi’ wa bwana harusi.

Cristiano Ronaldo akiingia kanisani

Wageni waalikwa wengine walikuwa ni kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson, Raisi wa Real Madrid, Florentino Perez, James Rodriguez, Jose Bosingwa na Deco De Souza pamoja na Pepe.
Mwanasoka Pepe wa Real Madrid nae alikuwepo
 
Mchezaji wa zamani wa Chelsea na Barcelona Deco De Souza
  
James Rodriguez wa Real Madrid nae alihudhuria
 
Bwana Harusi Jorge Mendes
  
Jose Bosingwa – mchezaji wa zamani wa Chelsea
 
Rais wa Real Madrid Florentino Perez
   LEO

Alichokisema Arsene Wenger kuhusu Karim Benzema nimekuwekea hapa

article-2681864-1F6B640000000578-973_634x639
Wiki kadhaa sasa zimepita toka uvumi kuhusiana na mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa anaeichezea klabu ya Real Madrid ya Hispania Karim Benzema kuuhusishwa kujiunga na Arsenal. Wengi wanaamini Benzema atahamia Arsenal kutokana na Wenger kuwa na utamaduni wa kupenda wachezaji kutokea Ufaransa.
Karim+Benzema+Marcelo+Real+Madrid+v+Malaga+hhDRUO1Wc-fl
Mwezi uliopita mkurugenzi wa Arsenal Lord Harris alisema Wenger tayari ana jina la mshambuliaji wa kati anayetaka kumleta Emirates msimu huu ambapo watu walihisi atakuwa Karim Benzema. Sasa habari zilizotoka August 3 kutoka kwa Wenger anashangazwa na taarifa hizo zinatoka wapi.
Benzema-BugattiMAIN
“Hakuna kinachotokea, kiukweli hakuna, sijui nani anaibua hizi taarifa, ni vyombo vya habari vya Hispania au Uingereza? Sijui”>>>Wenger

Baada ya kuwasajili Mesut Ozil na Alexis Sanchez misimu miwili iliyopita kwa dau ambalo sio kawaida kwa Wenger kununua mchezaji kwa kiasi hicho cha fedha, wengi walijua huenda atamsajili Benzema kutokana na mkurugenzi wa Arsenal Lord Harris kuthibitisha kuwa na kiasi cha fedha cha kutosha kumsajili mchezaji yoyote.

Hata hivyo kauli ya Wenger pekee haitoshi kwa vyombo vya habari kuamini kama kweli hana mpango na Karim Benzema kwani chochote kinaweza tokea.

Headlines zimeanza kupambwa, mpaka mwisho wa wiki huyu kipa atakua kasaini Madrid?

balon-oro-real-madrid
Moja kati ya Story ambazo zimeteka hisia za mashabiki wengi wa soka bila kusahau vyombo vya habari za michezo bila shaka ni story ya usajili wa kipa Mhispania David De Gea ambaye ulimwengu mzima unafahamu kinachoendelea kati yake na klabu mbili za Real Madrid na Manchester United.

Jarida moja la kila siku Hispania limeripoti kuwa kipa huyu atakuwa mchezaji wa Real Madrid mpaka ifikapo jumamosi ya wiki hii wakati ambapo Ligi Kuu ya England itakapokuwa ikianza rasmi msimu wake wa 2015/2016.

Taarifa hii inazidi kupata nguvu kutokana na tetesi ambazo zilizuka hapo jana ambapo kocha wa United, Louis Van Gaal aliripotiwa kusema kuwa angependa kuona De Gea akiuzwa kutokana na hali inayoendelea kuleta sintofahamu ndani ya timu.
Madrid watamsajili De Gea mpaka kufikia jumamosi ya wiki hii .
Madrid watamsajili De Gea mpaka kufikia jumamosi ya wiki hii.
Real Madrid imepanga kumfanya De Gea kuwa kipa wake namba moja baada ya kuondoka kwa Iker Casillas ambaye ameitumikia Madrid kwa muda wa miaka 25 karibu miaka 18 kati ya hiyo akiwa kipa namba moja.

Endapo United itakubali kumuuza De Gea katika wakati huu huenda wakajikuta kwenye wakati mgumu kutokana na kutokuwa na mtu ambaye timu hii imemuandaa kuwa mrithi wa De Gea huku wakiwa hawajaanza mazungumzo na kipa yoyote yule.

Kulikuwa na stori kwamba United imekuwa ikiigomea Madrid kuhusu De Gea huku wakisema wanahitaji kulipwa pound milioni 40 kwa ajili ya kipa huyo na Madrid wakiwa tayari kulipa pound milioni 25 pekee.

Beki wa Manchester United asajiliwa Ufaransa.

Football - Manchester United v Arsenal FA Cup Quarter Final - Old Trafford - 12/3/11 Fabio da Silva (R) celebrates with Rafael da Silva after scoring the first goal for Manchester United Mandatory Credit: Action Images / Carl Recine Livepic
Football – Manchester United v Arsenal FA Cup Quarter Final – Old Trafford – 12/3/11
Fabio da Silva (R) celebrates with Rafael da Silva after scoring the first goal for Manchester United
Mandatory Credit: Action Images / Carl Recine
Livepic

Beki wa kulia wa Manchester United Rafael Da Silva yuko mbioni kuihama klabu hii akiwa karibu kabisa na uhamisho kuelekea klabu ya Olympique Marseile ya nchini Ufaransa ambayo amekuwa akifanya nayo mazungumzo kwa muda wa siku kadhaa .

Da Silva anaihama klabu hii takribani miaka miwili baada ya pacha wake Fabio Da Silva naye kuhama akijiunga na timu Cardiff City ya huko Wales inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini England .

Kuondoka kwa Rafael kumekuwa kwenye mpango kwa muda sasa tangu ilipofahamika wazi kuwa Mbrazil huyo hatakuwa kwenye mipango ya muda mrefu ya kocha Louis Van Gaal .
Pacha wa Rafael,Fabio Da Silva aliondoka United misimu miwili iliyopita.
Pacha wa Rafael,Fabio Da Silva aliondoka United misimu miwili iliyopita.

Kocha huyo kwa muda amekuwa akimtumia Antonio Valencia ambaye kwa asili ni winga katika nafasi ya beki wa kulia hata pale ambapo Rafael amekuwa hasumbuliwi na matatizo ya majeraha na kwa msimu huu tayari United imemsajili beki Mtaliano Matteo Darmian jambo linalofanya nafasi ya Rafael kuwa finyu .

Rafael Da Silva amekuwa na United kwa kipindi cha muda wa miaka saba tangu mwaka 2008 alipojiunga rasmi na timu hiyo ambayo ilimsajili yeye na pacha wake tangu wakiwa na miaka 15 na walilazimika kungoja mpaka walipotimiza miaka 18 ili kuingia rasmi mkataba na klabu hiyo .

Hii ndio aina ya gari ambayo mastaa wengi zaidi wa soka wanatumia, Mtanzania mmoja nae yumo… (Pichaz)

Mchezo wa mpira wa miguu ni miongoni mwa kazi zenye mishahara mikubwa sana, kama ambavyo mtu kipato chake kinavyoongezeka ndivyo anavyotamani kumiliki kitu kizuri zaidi… Mastaa wa soka ni watu ambao wamekuwa na utamaduni wa kumiliki magari mengi na ya gharama ila kila mtu anapenda gari kulingana na hitaji lake au mapenzi yake
August 3 nakusogezea gari ambalo linamilikiwa na mastaa wengi zaidi wa soka.
Range_Rover_Sport_SDV6_SE_(Facelift)_–_Heckansicht,_5._September_2012,_Wuppertal
Mastaa wenye urefu kama Peter Crouch hupenda kutembelea Range Rover kwani magari ya chini huwa sio rafiki na maumbo yao. Range Rover ni gari ambalo lina thamani ya zaidi ya dola 60,000/= ambazo ni zaidi ya Tsh 120,000,000/=.
1. Peter Crouch ni staa ambae amewahi kuichezea timu ya Liverpool na sasa yupo katika klabu ya Stoke City.
article-2218994-158BF30B000005DC-348_634x730
Crouch akiingia kwenye mchuma wake wa nguvu !!
2. Robin van Persie wengi tulianza kumjua kupitia vilabu vya Arsenal, Manchester United ila kwa sasa yupo katika klabu ya Fenerbahce ya Uturuki.. Jamaa nae ana huu mchuma pia aisee !!
PAY-Van-Persie-pulled-over-by-Police
Robin Van Persie anaenda kuingia kwenye Range yake.. Hii picha ilinaswa ni kama jamaa aliingia kwenye utata na Police hivi..
3. Dareen Bent huyu ni mkali mwingine ambae amewahi kutamba katika vilabu vya Aston Villa, Tottenham Hotspur sasa yupo katika klabu ya Derby County.
Darren-Bent-pictured-in-2011-beside-the-luxury-Range-Rover-stolen-from-his-home-at-the-weekend
Dareen Bent nae ana hii Range Rover Sport yake kali kabisa.
4. Ryan Giggs ni mkali ambae ana heshima kubwa Manchester United kabla na hata baada ya kustaafu soka, mcheki anavyoisukuma sasa Range Rover yake mtaani… taratiibu namna hii.
article-2438591-1865BD5500000578-380_634x430
5. John Terry ni nahodha wa klabu ya Chelsea lakini pia anaichezea timu ya taifa ya Uingereza.
article-2438591-1865BC8F00000578-263_634x393
John Terry yuko zake mtaani anakula stori na watu wake.
6. Wayne Rooney nahodha wa Manchester United nae yumo katika orodha ya mastaa wanaomiliki Range Rover
1365503034
7. Michael Essien mkali wa soka kutokea Ghana ameingia pia katika hii orodha
Michael Essien Foundation new

maxresdefault
8. David Beckham hadi anastaafu soka alikuwa anatajwa kuwa mwanasoka tajiri Duniani, akaona sio mbaya na yeye kumiliki Range Rover yake kali kabisa!!
tyres-for-footballers-David-Beckhams-Range-Rover
Beckham na watoto wake.
9. Javier Hernandez Chicharito ni mkali wa mipira ya kuvizia jina lake lilikuwa kubwa zaidi baada ya kujiunga na Manchester United mwaka 2010.
range-rover-sport
10. Mbwana Ally Samatta huyu ni mchezaji pekee wa Kitanzania ambae ameingia katika hii orodha, amewahi kutamba na klabu ya Simba kabla ya kutimkia TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mbwana Samatta
Mbwana Samatta mbele ya gari yake

Tazama hapa picha za utoto za Cristiano Ronaldo

Cristiano Ronaldo ni mchezaji nyota wa kimataifa wa Ureno ambae wengi tumemfahamu kupitia vilabu vya Manchester United na Real Madrid ya Hispania, Ronaldo ni mtoto wa nne katika familia ya  Maria Dolores dos Santos na Jose Dinis Aveiro.
Cristiano-Ronaldo-Childhood-pic1
Hadi sasa moja kati ya vitu vinavyomuumiza Cristiano Ronaldo ni kifo cha baba yake mzazi marehemu Jose Dinis Aveiro ambapo huwa anatamani angekuwa hai hadi leo hafaidi mafanikio yake aliyoyapa katika soka. Jose Dinis Aveiro alifariki mwaka 2005 kutokana na ulevi wa pombe kupindukia ambao ulisababisha kupata tatizo la Ini.
Cristiano-Ronaldo-Childhood-pic2
Nimekusogezea picha za utoto za Cristiano Ronaldo akiwa na wazazi wake na ndugu zake wengine.
Cristiano-Ronaldo-Childhood-pic6
Cristiano Ronaldo akiwa na baba na mama yake
Cristiano-Ronaldo-Childhood-pic5
Cristiano-Ronaldo-Childhood-pic4
Cristiano-Ronaldo-Childhood-pic03
De-vader-van-Cristiano-Ronaldo
cristiano_ronaldo_roots_003
Kaburi la baba yake Ronaldo na mama yake kulia

Simba yaendeleza usajili kimya kimya kwa kumsajili mshambuliaji huyu kutoka Kongo

Tukiwa tunaelekea kuanza kwa Ligi Kuu soka Tanzania bara vilabu kadhaa vimezidi kujizatiti kwa kusajili wachezaji wenye viwango vya juu. Klabu ya soka ya Simba ambayo bado ipo katika hali ya sintofahamu juu ya mshambuliaji Laudit Mavugo raia wa Burundi lini atatua Dar Es Salaam, Simba imetangaza kumsajili mshambuliaji mwingine.
IMG-20150625-WA0062
Simba imemsajili mshambuliaji Danny Lyanga kutoka katika klabu ya DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Lyanga amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Simba na atasafiri August 2 kuelekea visiwani Zanzibar kuungana na wachezaji wenzake walioweka kambi visiwani humo.

Zikiwa zimebaki siku nne kufungwa kwa dirisha la usajili, klabu ya Simba ndani ya siku tatu imesajili wachezaji watatu ambao ni kiungo kutoka Zimbabwe Justice Majabv na beki kutoka Burundi Emery Nimubona.
IMG_1903

 


 

 


 


 


 

 

 

 

00746F2C00000258-0-image-a-6_1437407822849

 

Share on Google Plus

About Unknown

TEAM TASABA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment