Freeman Mbowe kuhusu Dk. Slaa… Mrithi wa Jimbo la Lowassa? Waliogoma kusaini matokeo? Udiwani wa Manji na Said Fella..
MWANANCHI
Binti wa Waziri mkuu wa zamani, Edward Sokoine ambaye anaitwa Namelock Sokoine ameshinda kura za maoni kugombea ubunge Jimbo la Monduli kupitia CCM huku mkwe wa Lowassa, Siyoi Sumari akishindwa Jimbo la Arumeru Mashariki.
Namelock ambaye ni mbunge wa Viti Maalumu CCM alipata kura 29,582 akifuatiliwa na Loota Sanare aliyepata kura 8,809 na nafasi ya tatu, ilichukuliwa na Lolinyu Mkoosu aliyepata kura 235 na Payani Leyani akipata kura 226.
MWANANCHI
Wadau wawili wa michezo na burudani Tanzania Yusuf Manji na Said Fella wameibuka kidedea katika kinyang’anyiro cha udiwani katika jimbo jipya la Mbagala jijini hapa.
Manji ambaye ni
Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Quality Group,
alishinda katika Udiwani katika Kata ya Mbagala Kuu wakati Fella ambaye ni msimamizi wa kazi za wasanii na muasisi wa Kundi la Mkubwa na Wanawe, akishinda katika Kata ya Kilungure.
Fella ni Meneja wa mwanamuziki maarufu nchini, Diamond Platnumz, TMK Family na Yamoto Band.
Kaimu Katibu CCM Wilaya ya Temeke, Rutami Masunu
alisema uchaguzi huo ulikwenda vizuri katika maeneo mengi isipokuwa
kulitokea changamoto kidogo katika kata moja ambayo itafanya uchaguzi
leo.
MWANANCHI
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amezungumzia kukosekana kwa Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Willibrod Slaa
katika vikao vya chama hicho vinavyoendelea, >>>
“Nitazungumzia suala hilo muda muafaka ukifika… Siwezi kusema zaidi ya
hapo”- hilo ndio jibu lake alipoulizwa.
Kauli hiyo ya Mbowe haikuondoa wingu
zito lililotanda CHADEMA baada ya kutoonekana hadharani kwa kiongozi
huyo katika matukio manne muhimu ya chama hicho kikuu cha upinzani,
tangu Waziri Mkuu Wa Zamani, Edward Lowassa ajiunge nacho.
Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Mnyika
alionekana jana kwa mara ya kwanza katika kikao hicho na kufuta uvumi
uliokuwa umesambaa kuwa alikuwa na mpango wa kuachana na CHADEMA kama
inavyodaiwa kwa Dk Slaa.
Viongozi hao walianza kutoonekana katika
shughuli za chama tangu Lowassa alipojiunga na Chadema Julai 28 na
kukabidhiwa fomu ya kugombea Urais Julai.
“Suala
la kutokuwapo Dk Slaa ni kitu cha kawaida, anafanya kazi nyingine huko,
lakini pia kuna wasaidizi wake hapa ambao ni sisi manaibu. Mlikuwa
mnazungumzia Mnyika naye haonekani, si huyo. Hatuwezi kuendelea kujibu
‘rumors’ (uzushi) wa kwenye mitandao… nyie subirini si tupo mtaona kama
yupo au la”– Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu.
Mbunge Mnyika alionekana katika viwanja vya hoteli hiyo lakini alikataa kuongelea chochote >>>“Siwezi kuzungumza chochote”—Mnyika.
NIPASHE
Wagombea wawili wa kiti cha Ubunge
katika Jimbo la Moshi Mjini kwa tiketi ya CCM, ‘wamegoma’ kusaini
matokeo ya kura za maoni yaliyompa ushindi mfanyabiashara maarufu wa Dar
es Salaam, Davis Mosha.
Waliogoma kusaini matokeo hayo ni Buni Ramole na Patrick Boisafi, ambao walikuwa washindani wakuu wa Mosha kati ya wagombea 12 waliojitokeza kuomba kuteuliwa na CCM kugombea Ubunge Jimbo la Moshi Mjini.
Katibu wa CCM Moshi Mjini, Loth Ole Nessele
amesema Buni alikataa kusaini matokeo hayo akidai amepata `presha’
kutokana na mchakato huo wakati Boisafi alimweleza kwamba hawezi kusaini
kwa sababu yupo nyumbani peke yake na amechoka kutokana na mchakato
huo.
“Ni
kweli nimekataa kusaini matokeo na tayari nimewaandikia na kuwakabidhi
CCM barua nikiwaeleza kuhusu uamuzi wangu. Rushwa za wazi wazi na
upendeleo kwa mgombea mmoja ni hatari na wala CCM isifikiri kwa mwendo
huu italikomboa Jimbo la Moshi Mjini”– Buni Ramole.
NIPASHE
Baadhi ya Vigogo wakiwamo Mawaziri, Wabunge wameangushwa katika Kura za Maoni za kutafuta wagombea Ubunge kupitia CCM.
Miongoni mwa waliangushwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.
Wamo pia Manaibu Mawaziri wa Mambo Ya
Ndani ya Nchi Na Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, mawaziri wa
zamani, Mkuu wa Mkoa na wabunge.
Kwa upande wa Zanzibar, Wabunge na wawakilishi wa CCM wanaotetea tena nafasi hizo wengi wamejikuta wakianguka.
Wabunge na wawakilishi hao waliotupwa katika kura hizo yumo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, aliekuwa akigombea Ubunge jimbo la Paje wilaya ya Kusini Unguja.
Huyu ndio msichana ambae anasoma PhD India na umri wake ni miaka 15 tu…!!
Kwa hesabu ya kawaida tu, mtoto anaanza
Shule ya akiwa na miaka sita, au saba hivi… alafu mpaka kumaliza anakuwa
na kama miaka 14, sasa kuna mtu kwenye umri huo alikuwa kamaliza high
school na alikuwa Chuo tayari anamaliza zake degree!!
Anaitwa Sushma Verma ni msichana ambaye umri wake ni miaka 15, aligraduate Degree ya Microbiology Chuo cha Lucknow kilichopo India na kajiunga Babasaheb Bhimrao Ambedkar University (BBAU) kwa ajili ya kusomea Masters, kamaliza mwezi June 2015 na anaendelea kujipanga ili kuendelea na masomo ya PhD.
Hii
ilikuwa wakati Sushma Verma anasoma Masters, alikuwa na miaka 13 tu..
kuna wakati baba yake ilibidi atumie baiskeli kumsindikiza mwanae shule.
Sushma
amewashangaza wengi lakini ndio hivyo, ana uwezo mkubwa sana darasani
kitu ambacho Mkuu wa Chuo hicho amemuahidi kumpa ofa ya kulipiwa ada
pamoja na Hostel bure akianza PhD ya environmental microbiology
>>> “Lazima tumpe moyo kwa kipaji chake, tutamsajili na kumpatia Hostel na scholarship pia” >>> Prof. R C Sobti, Makamu Mkuu wa Chuo Babasaheb Bhimrao Ambedkar University.
Maneno ya Steve Nyerere baada ya kushindwa kwenye kura za maoni
Stori ninayokusogezea ni hii kutoka kwa
msanii wa filamu Tanzania, Steve Nyerere ambaye wiki iliyopita
hakufanikiwa kuwania ubunge wa jimbo la Kinondoni kutokana na kura zake
kuwa chache.
Sasa leo msanii huyo amefunguka baada ya kukutana na ripota wa millardayo.com & AYO TV na kusema ‘Kwanza
namshukuru Mwenyezi Mungu lakini niwashukuru Wananchi wa wiliaya ya
Kinondoni wamenionesha upendo ambao sikutarajia kwao, la pili
sikubahatika kulishika gurumo hili la kuwa kiongozi na sitaweza kukata
tamaa kwasababu hivi vitu vinahitajika uvumilivu kidogo, siasa
inahitaji kuwa mvumilivu na kila kitu kinachofanywa kama mwanadamu
kinachotaka kupigiwa kura au kutafuta maisha ni uvumilivu unaohitajika
kusonga mbele’ – Steve Nyerere
‘Kwasasa nipo kidogo mapumziko
nikitafakari kuna yale niliyoyafanya na changamoto nilizozipata katika
uchanguzi huo nimejifunza mambo mengi mengi ambayo kwangu yanatija kwa
hiiyo kwangu ni changamoto kubwa sana’ – Steve Nyerere
RipotaTZA:Kuna taarifa tumezisikia kuwa kuna baadhi ya wasanii wameama kutoka chama cha mapinduzi na kwenda Chadema hizi taarifa zikoje?
Steve Nyerere...’Kwanza
wao sio wavumilivu pili wamezaliwa na kukikuta chama cha Mapinduzi
vile vile kama wasanii hapa tulipofika ni msaada mkubwa sana wa mh.Rais
Jakaya Mrisho Kikwete kutuonesha thamani yake kubwa kwetu ameweza
kutukanwa kwaajili yetu na ameweza kututhamini, sasa leo na mimi nasikia
kuwa kuna watu 15 wakiwemo wasanii wa bongo movie na wasanii wa Bongo
Fleva 3 wamekiama chama cha CCM na kuhamia CHADEMA’
‘Mimi nasema milango iko wazi
watajichuja watabaki sahihi ambao ni sisi, na mtu kama mimi sina mawazo
kwasababu nimeshindwa kura za maoni niseme kwamba nihamie chama Fulani
sina mawazo hayo na sitarajii kuhama mimi nimezaliwa ndani ya chama cha
Mapinduzi na nitakufa ndani ya chama cha Mapinduzi na ni chama changu
nakipenda kwa dhati na pia nawambia wenzangu wakishindwa huko watarudi
tu kwenye chama hiki cha Mapinduzi’ -Steve Nyerere
0 comments :
Post a Comment