LIKE NIONE WANGAPI MTAISOMA SIMULIZI HII
SIMULIZI-NEVER SAY GOODBYE
MTUNZI-VICTOR DISMAS
SIMU(Watsaap)-0716616279
INSTAGRAM-VICTOR.DISMAS
FACEBOOK-Victor Dismas Van Manda
SEEMU YA PILI
Ndani ya Gari Dominick alikuwa anawaza ni jinsi gani atakavyo yaanza maisha mapy katika jiji la Dar es salaam ambapo alikuwa hajawai kufika hapo kabla.Mawazo yalikuwa mengi lakini yalimezwa na usingizi mzito.Safari ilichukua masaa takribani matatu na nusu mpaka kufika katika jiji la Dar es salaam.Abiria wote walishuka na kuanza kuelekea majumbani kwao kwa kuchukua usafiri tofauti tofauti
Dominic alibaki akishangaa shangaa sababu alikuwa hajui wapi pa kuanzia.Taratibu aliazna kufuata mahali zilipopaki tax kwaajili ya kuchukua moja ili impeleke chuoni.
“Samahani naomba unipeleke chuo”alisema Dominic baada ya kumfikia dereva wa tax
“chuo kipi manake vyuo vipo vyingi hapa?”Dereva wa tax aliuliza
“chuo kikuu cha Dar es salaam”Dominic alisema
“bei si unaijua?Dereva aliuliza huku akipepesa macho kumuangalia Dominic
“sh ngap?”Dominic aliuliza
“elfu kumi”dereva alijibu bila wasiwasi baada ya kumuona Dominic ni wakuja
“me nina elfu tano”Dominic alisema
“hapana ongeza tatu iwe nane”Dereva alesema
“sawa twende”Dominic alisema huku akipanda kwenye tax
Safari haikuwa ndefu sana kwani hapakuwa na umbali kutokea ubungo mpaka chuoni.Dominic alifurahi sana kuyaona mazingira ya chuo.Kila mtu alionekana akiwa kwenye mishe mishe zake za mchana.Moja kwa moja Dominic alielekea kwenye jengo la utawala ambapo usajili ndipo ulikuwa unafanyika.Alikuta baadhi ya wanafunzi wachache wakisubiri kusajiliwa
Dominic alifanikiwa kumaliza usajili siku hiyo hiyo na kufanikiwa kupata hostel ndani ya chuo.Kupata hostekl ndani ya chuo lilikuwa ni jambo gumu sana hasa kwa wanafunz wanaotokea katika mkoa wa Dar es salaam.Wanafunzi wengi waliokuwa wanapata hostel ndani ya chuo ni wale waliokuwa wanatokea mikoani .
Baada ya kukamilisha kila kitu Dominic alianza rasmi masomo yake katika chuo hicho.Dominic alikuwa ni mwanafunzi mkimya katika Kitivo chao cha Uchumi (Barchelor of arts in Economic).Dominic alikuwa hajazoeana na mtu yoyote zaidi ya salamu na wale watu waliokuwa wanakaa wote katika chumba chao.Muda wa vipindi unapokwisha Dominic uwa anarudi katika chumbani na kufanya mambo yake mengine.
Chumba alichokuwa anakaa kulikuwa na wenzake watatu ambao nao walionekana kutoka katika mikoa mbalimbali.Moja kati ya watu hao watatu alikuwa na tabia aliyokuwa nayo Dominic kwani nae alikuwa mpole kuliko wale wengine wawili.Huyu aliitwa Raphael,Raphael alikuwa mkimya kama alivyokuwa Dominic kiasi kwamba Dominic akaona Yule ndiyo mtu ambae anaweza kujenga urafiki nae wa karibu katika masomo na mambo mengine ya kimaisha
Wale wenzao wawili ambao ni Anthony na Edward walikuwa ni watu wa club na sehemu nyingine za starehe hiyo ilitokana wao kuwa mwaka wa pili kwahiyo walishazoea mazingira katika Jiji la Dar es salaam.Hawakuwa na urafiki mkubwa sana zaidi ya kusalimiana na kila mtu kuendelea na mambo yake mengine
“Natamani sana nilizunguke jiji hili ili nione watu wanavyosemaga”Dominic alisema siku moja akiwa na Raphael wakiongea
“hili jiji ni kubwa sana hata mimi natamani sana nilizunguke sababu nimechoka kukaa hapa chuoni”alisema Raphael kumuunga mkono
“tutafute siku moja kwaajili ya kutembea”alisema Dominic akionyesha wazi kuchoshwa na upweke wa kukaa sehemu moja
“Ninyi wajinga kweli mnawaza kutembea wakati mimi kichwa changu kinawaza ni jinsi gani naweza nikampata Doreen”alisema Athony na kumfanya Edward acheke
“Doreen ndiyo nani?”Dominic aliuliza
“ndiyo Malkia wa chuo hiki”alisema Anthony na kumfanya Dominic apatwe na bumbuwazi baada ya kusikia pale chuoni kuna malkia
“kwanini mnamuhita malkia?”Dominic aliuliza
“kwasababu ndiyo msichana mrembo kuliko wote katika chuo hiki,na kila sehemu utakaposikia wanazungumza warembowa chuo basi lazima jina la Doreen liwepo”alisifia Anthony
“ipo siku nitamuona huyo malkia wa chuo hiki”Dominic alisema na kufanya kila mtu acheke
“hahahahaha wewe umetumwa na kijiji chenu uje kusoma na siyo kutafuta wanawake,na hata kama itatokea siku ukamuona huyo Doreen sidhani kama utaweza hata kunyanyua mdomo wako na kumuongeresha neno lolote hata kama ni salamu”alisema Anthony kwa kukejeri
“sijaja kutafuta mwanamke ila napenda tu nimuone sababu hizo sifa zake nahisi kama mnampamba sana”Dominic alisema
Story zilikomea hapo kwani kila mtu alikuwa na mambo yake mengine.Dominic alijilaza kitandani kwaajili ya kupumzika kidogo ili baadae afanye mambo yake mengine.Usingizi nao ulimchukua mpaka alipokuja kushtuka ni usiku sana
Siku zilikatika pale chuoni huku Dominic akiwa bado hajapata bahati ya kukutana na Doreen,Dominic alijitahidi kutengeneza picha ya Doreen kichwani kwake kwa kutumia zile sifa alizopewa na wenzake.Dominic alidiriki kufumba mpaka macho bila kujua yupo sehemu gani,yote hiyo ilikuwa ni kutengeneza urembo wa mwanamke aliyekuwa anazungumziwa.
“ina maana huyo msichana ni mzuri sana?,Tuseme ana sura nzuri ya kuvutia?,ana umbo lililojijenga vilivyo na kuweka muonekano mzuri kwenye macho ya watu?,Huyo msichana ana kila kitu cha kuitwa malkia wa chuo?”Dominic alikuwa anajiuliza maswali huku akimtengeneza msichana mzuri kichwani mwake ambae anaweza akafanana na huyo msichana anayezungumziwa
“kwanini najitesa wakati nilishasema sihitaji msichana,kweli mimi sina akili”Dominic alijisemea kimoyoni huku akifumbua macho yake
Moyo ulimlipuka baada ya kuona kitu ambacho hakukitarajia kukiona kwa muda huo.Alikuwa ni msichana mzuri aliyekuwa anakatiza mbele yake huku akiwa ameongozana na mwenzake.Dominic alifikicha macho ili kuhakiki kile alichokuwa anakiona mbele yake
“ina maana huyu ndiyo Doreen?”Dominic alijikuta akijiuliza kwa sauti
“huyo ndiyo Doreen malkia wa chuo niliyekuwa nakuambia sifa zake,na hapa nilikuwa namfuatilia yeye”Dominic alisikia sauti ikimuongeresha huku akishikwa begani
Alipogeuka alikuwa ni Athony ambae wanakaa wote chumba kimoja.Dominic alitabasamu kisha akarudisha macho yake kwa Yule mrembo aliyekuwa bado anatembea kwa madaha.Macho yake yaliishia kumuona Doreen akiingia kwenye Restaurant ambayo ipo hapo chuoni
“kwanini mlimpunja sifa zake?”Dominic alimuuliza Anthony
“kivipi?”Anthony nae aliuliza
“hakika huyu msichana ni mzuri sana na zile sifa mlizokuwa mnazitaja hakuzimaiza zote”Dominic alisema huku akigeuza macho yake kuangalia pale alipokaa Doreen
Hapakuwa mbali sana na pale alipokuwa yeye kwahiyo alipata fursa ya kumuona vizuri Doreen,aliweza kuuona vizuri uzuri wa msichana huyo.Hakika Doreen alionekana ni mzuri sana kwenye macho ya Dominic kuliko kwenye macho ya mtu mwingine yoyote.Moyo wa Dominick ulisuuzika viivyo na kujikuta yupo sehemu ya mbali sana
“Dominic naomba unisindikize”Anthony alisema huku akimshika mkono Dominic na kumvuta
Waliongozana mpaka pale kwenye restaurant ambapo Doreen alikuwa amekaa na mwenzake wanakula chakula.Anhtony hakuwa na aibu yoyote sababu alishajiona kwamba yeye ndiyo anastahili kuwa na msichana Yule mrembo.Waliongozana mpaka kwenye ile meza aliyokaa Doreen na rafiki yake.Dominic alionyesha hali ya wasiwasi sababu lile jambo lilikuwa ni geni sana kwake.
“za saa hizi warembo”Anhtony alisalimia
“salama”waliitika wote kwa pamoja
“tunaweza kujiunga nanyi?”Anthony aliuliza huku akionyesha sura ya tabasamu
“why not?”alijibu Doreen akimaanisha kwamba wanaweza kujiunga
Anthony na Dominic walikaa pale kwenye viti huku Dominic akionekana kama bumbuwazi kutokana na kutoongea neno lolote lile,Anthony alinekana kuwa mchangamfu kuliko Dominic ambae alionekana kuwa kimya muda wote akimuangalia Doreen kwa macho ya kuibia
“Doreen mimi naitwa Anthony”Anthony alijipendekeza kwa kutaja jina lake
“nani aliyekutajia jina langu?”Doreen aliuliza
“sidhani kama kuna mtu ambae anasoma katika chuo hiki hakujui wewe au kukusikia hata jina lako”alisema Anthony
“kwanini?”aliuliza Doreen
“Doreen sifa yako ya uzuri ndiyo inamfanya kila mtu atake kukufahamu,Wewe ni mzuri”alisema Anthony na kumfanya Dominic aangalie chini kwa aibu
“Asante sana”Doreen alijibu
Ile sifa ya kuambiwa kwamba yeye ni mzuri alishaisikia kwa watu wengi kwahiyo hakuona neno jipya.Neno lile ndiyo lilikuwa neno la kwanza kwa wanaume wakware kulitamka ili kummaliza mwanamke kisha wanatuma nduano zao,Doreen alipoona hali ile inataka kutokea alitabasamu kisha akaanza kukusanya vitu vyake kwaajili ya kuondoka.
“Goodbye(kwaherini)”Doreen alisema kuwaaga huku akivuta hatua
“sorry Doreen(samahani Doreen)”silisikika sauti nyingine ngeni katika masikio ya Doreen ikimuomba radhi,Si mwingine bali alikuwa ni Dominic aliyetamka neno lile na kumfnya mpaka Anthony amuangalie sababu hakujua ni kitu gani anachotaka kuzungumza wakakti muda wote alikuwa kimya
ITAENDELEA……………………………..
We unadhani Dominick anataka kumuambia nini Doreen

0 comments :
Post a Comment