TASABA SIMULIZI SEHEMU YA PILI

SIMULIZI; YAATIMA
MTUNZI; Pascal Pahali
Email;pascalpahali@rocketmail.com
Contact;+255655-123 103
WhatsApp;+255655-123 103
Instagram; santiano del pahali
LIKE ILINIPOST SEHEMU INAYOFUATA
SEHEMU YA II
ILIPOISHIA
Ukiwa bado…………………………………..............................
ENDELEA
Hujaja katika dunia hii iliyojaa kila aina ya mateso na masumbufu.Mimi mama yako nilikuwa nikihangaika kutafuta riziki kwa ajili ya familia yetu.Katika kuzunguka kwangu huku na huko nilibahatika kufanya kazi katika kampuni moja ya wachina huko jijini Dar es salaam.Nikiwa kama kibarua katika kampuni hiyo na kipindi hicho nilikuwa bado msichana na mzuri sana.Nilikutana na mtanzania mwenzangu ambae ndiye aliyekuwa mtafsiri wa lugha kati ya wafanyakazi wa pale na wachina hao.Kwakuwa mtanzania huyo alikuwa ameishi na wachina kwa kipindi kirefu alikuwa ameshajua lugha ya wachina hao, kwahiyo aliweza kututafsiria lugha hiyo kwa wafanyakazi wengine.Siku moja nikiwa naingia geti la pale kazini mtanzania yule aliniita wakiwa na mchina ambapo waliongea kwa ishara na baadae kuniita.Niliitikia wito wao na kwenda kuwasikiliza.Baada ya kufika eneo lile yule mtafsiri au mkaliman aliniambia baadae kabla ya kuondoka nimtafute nami nilikubali na kisha kwenda eneo langu la kazi.
Baada ya muda wa kazi kuisha nilimtafuta mkaliman kama ambavyo tulikuwa tumekubaliana na ndipo aliniomba tukakae ofisini kwake kwa mazungumzo mafupi.Nilikubaliana nae maana mpaka muda ule sikujua alikuwa akinitafutia kitu gani.Nilipoingia mule ofisini kwa mkaliman mara mkaliman alishika simu yake na kuongea na mtu kisha kukata simu yake.Baada ya kukata simu yake aliniuliza jina langu nami nikamtajia.Baada ya muda kama dk 10 mchina mmoja aliingia mule ofisini kwa mkaliman.Nilipomtizama mchina yule kumbukumbu ilinijia ni yule mchina niliyewakuta na mkaliman wakati naingia getini.Mchina yule alikaa kitako na ndipo mkaliman kuniambia kuwa mchina yule aliomba kuwa mpenzi wangu.Nilishituka sana na kuogopa maneno yale ya mkaliman.Sikuogopa kama kwamba maneno yale yalikuwa mageni kwangu lakini nilichoogopa ni kwamba iweje mchina atembee na mimi? Baada ya maneno hayo ya mkaliman niliruhusiwa kwenda nyumabni na kujifikiria juu ya suala hilo na kisha siku iliyofuata wangenifuata kwa jibu.Niliwaaga na kuondoka kwa unyonge sana mule ofisini kwa mkaliman.Nilirudi nyumbani na njia nzima niliwaza juu ya suala hilo.
Masaa hayakawii siku iliyofuata nilijiandaa na kwenda kazini kama ilivyokuwa kawaida yangu.Pamoja na kuwa usiku uliyotoka niliwaza sana juu ya suala hilo lakini njiani pia mawazo yalinijia na kujisemea endapo nitamkatalia mchina yule basi kwa asilimia kubwa nisingekuwa na kazi tena mahali pale.Lakini potelea mbali endapo watanifuata nitajua nini cha kuwajibu na kama wasipokuja basi ingekuwa ni afadhari kwangu maana usumbufu ungepungua.Nilifika kazini na kuandaa mazingira ya pale ofisini kwangu na kisha kuanza kuendelea na shughuli zangu za kila siku.Nilifanya shughuli zangu kama masaa 3 mbele niliamua kutoka na kuelekea kupata kifungua kinywa moja ya kefteria za pale kazini.Nilipomaliza kufungua kinywa nilienda kaunta kwa ajili ya malipo lakini nilipotoa hella kwa ajili ya malipo mhudumu wa pale kaunta aliniambia nilishalipiwa na nilipouliza ni nani aliyefanya hivyo mara mhudumu yule alinyoosha mkono wake na kunionyesha sehemu ambapo nilipotazama nilimuona yule mkaliman amekaa na kisha kutabasamu.Nilinyanyua miguu yangu taratiibu…………….................................................................
Itaendelea>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Je mama yake Yaatima mara baada ya kumuona mkaliman yule na kuambiwa alikuwa tayari ameshalipiwa alinyanyua miguu yake na kufanya nini? Soma sehemu inayofuata ya simulizi hii
Share on Google Plus

About Unknown

TEAM TASABA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment