TASABA TOP STORY TODAY

Huyu ndiye mbadala wa Kpah Sherman Yanga

Vilabu mbalimbali vinavyoshiriki Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu huu vinazidi kujiimarisha kwa kufanya usajili wa mwisho kabla ya dirisha la usajili halijafungwa August 6, klabu ya Dar Es Salaam Young African imemleta kiungo wa FC Platnum ya Zimbabwe Thabani Kamusoko.
Thabani-Kamusoko
Yanga imefanikiwa kumleta Kamusoko ambae amewasili jioni ya August 5 akitokea Zimbabwe na amepokelewa na meneja wa Yanga Hafidh Saleh katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere(JNIA) na kupelekwa moja kwa moja katika kikao na viongozi kinachotajwa kuwa atasaini mkataba wa miaka 2.
ngodzo-kamusoko550
Kamusoko anawasili Dar Es Salaam ikiwa ni siku kadhaa zimepita toka mshambuliaji wa kimataifa kutokea Liberia Kpah Sherman aondoke na kwenda kujiunga na Mpumalanga Black Aces ya Afrika ya kusini. Dirisha la Usajili litafungwa August 6 na kutakuwa na muda wa wiki moja kwa ajilii ya kuwasajili wachezaji walio huru.

Furaha ya mjukuu ikakamilika baada ya kuona bibi kasimamia harusi yake …

maids
Tumezoea kuona harusi nyingi  wasichana ambao hufahamika zaidi kama wapambe au ‘Maids’  ndio hupewa jukumu la kusimama mbele na maharusi kw alengo la kunogesha sherehe.

maids3
Christine na mume wake wakiwa na wapambe wao akiwemo bibi yake Nana Beth
Lakini hii inaweza kuwa Stori kwako mtu wangu baada ya bibi harusi Christine kumchagua bibi yake Nana Beth mwenye miaka 89 kumsimamia kwenye harusi yake sambamba na wasichana wengine.

Si ndugu zake tu walioshangazwa na uamuzi huo kwani hata muhusika mwenye alishangaa kuona mjukuu wake akimpa jukumu hilo huku akimuuliza zaidi ya mara 10 kama ana uhakika na anachokisema, lakini uamuzi wake ulibaki pale pale.
maids4
Christine akiwa na bibi yake Nana Beth
Ushiriki wa bibi huyo ulivuta hisia za wageni wengi katika sherehe hiyo huku mwenyewe akimudu vyema katika shughuli ya mjukuu wake huyo pamoja kucheza kuanzia mwanzo hadi mwisho wa sherehe.
maids5

Mascherano ala shavu Barca.

barca
Kiungo raia wa Argentina Javier Mascherano ameteuliwa kuwa nahodha wa nne kwenye klabu ya Barcelona akiongeza idadi ya manahodha ambayo ilikuwa imebakia manahodha watatu baada ya kuondoka kwa Xavi Hernandez.

Kuondoka kwa Xavi Hernandez kumefungua nafasi moja ya unahodha baada ya kupandishwa kwa Andres Iniesta ambaye amekuwa nahodha wa kikosi cha kwanza huku Lionel Messi akiwa nahodha wa pili na Sergio Busquets akiwa nahodha wa tatu.

Kocha wa Barcelona Luis Enrique amemzungumzia Mascherano kama mchezaji ambaye ana sifa ya uongozi hata kama sio nahodha rasmi kwenye timu na kwa sababu hii ana kila sifa ya kuwemo kwenye orodha ya manahodha wa klabu.

Enrique ameongeza kuwa Mascherano ni mchezaji ambaye timu nzima inamheshimu na hivyo ni uchaguzi ambao haukuwa na pingamizi toka kwa wachezaji wengine.

Aliambiwa hatokuja kupata mtoto, miaka 60 baadae stori ni hiki kilichokutwa tumboni !!

ANCIANA DE 92 AÑOS PORTA FETO MOMIFICADO EN SU VIENTRELA BOCA 19 DE JUNIO 2015FOTOGRAFÍAS CHRISTIAN PAVEZ CISTERNA
Estela Melendez 91
Nimekutana na stori moja kutoka mji mdogo wa La Boca ulioko Chile ambako mwanamke wa miaka 91 amekutwa na mtoto tumboni ambapo mtoto ujauzito huo kaubeba kwa zaidi miaka 60.

Estela Melendez mwenye umri wa miaka 91 amekua akilalamika kwa zaidi ya miaka ishirini kwa kuwa na uvimbe mgumu tumboni mwake na hakuwahi kuhisi ana ujauzito na wala hakuwa na dalili zozote za kuwa na ujauzito.
ES2
Estela Melendez akiwa na baadhi ya ndugu zake
Baada ya madaktari kumfanyia vipimo na uchunguzi wa kutosha wamegundua ya kuwa mwanamke huyo alishika ujauzito akiwa na umri wa miaka 30 hivi, kitu ambacho kimewashangaza ndugu zake wengi ni kwamba yeye na mume wake waliambiwa hawawezi kupata watotoalafu leo zimekuja stori nyingine.

Estela Melendez amesema hakuwahi kuhisi dalili zozote kwa kipindi chote ila alijihisi uvimbe mdogo ukimuuma na kuacha kwa nyakati tofauti…alikuwa akipata maumivu mara mojamoja lakini zaidi ya hapo uvimbe huo umemkosesha raha kwa miaka mingi.
ES4
Hiki ndio kilichokutwa tumboni mwa Estela Melendez
Madaktari wamesema uvimbe huo hauna madhara yoyote kwa mwanamke huyo ila wanajianda kumfanyia upasuaji kuutoa uvimbe huo, kwa sasa Estela Melendez amelazwa hospitalini akisubiri kufanyiwa operation hiyo.

Mastaa wa soka na vioja vyao Uwanjani>>Balotelli, David Luiz na Ibrahimovic na wamo…

Wachezaji mpira ni miongoni mwa watu maarufu sana kutokana na kazi yao kupendwa au kuwa na mashabiki wengi kutoka sehemu mbalimbali, miongoni mwa vitu ambavyo huwezi kuvidhania kama unaweza kuviona kwa mastaa wako wa soka ambao umezoea kuwaona wakiwa katika muonekano uliozoeleka kuonekana labda wakiwa katika mechi au matukio ya kawaida.

Katika pitapita zangu mtandaoni nimekutana na hii list ya mastaa wa soka waivyoamua kujiachia kwa vioja kabisa.
Dani Alves
download (1)
Dani Alves aliwahi kuvaa wigi wakati akisherehekea ushindi wa Timu yake ya Taifa
Andrey Arshavin
download (2)
Ni mchezaji wa zamani wa Arsenal anatajwa kuwa sio miongoni mwa watu wanaouchukulia mchezo wa mpira wa miguu serious.. Ndani ya Uwanja akaona afanye kioja kupindisha uso wake.
Mario Balotelli
download (3)
Chochote anachokifanya Balotelli huwa hakiko mbali na headlines za Waandishi wa Habari.
Antonio Cassano
download (4)
Antonio Cassano akishangilia ushindi wa goli 2-0 Italy ilivyoifunga Ufaransa katika michuano ya Euro 2008.
Zlatan Ibrahimovic
download (6)
Zlatan Ibrahimovic wakati alipovua nguo Uwanjani bila hofu kabisa.
Stephen Ireland
download (7)
Kiungo wa zamani wa klabu ya Manchester City Stephen akishangilia goli kwa staili ya kuvua bukta
David Luiz
download (8)
David Luiz beki ghali wa klabu ya PSG ya Ufaransa akishangilia goli

 

Ripoti kutoka Makao makuu ya CUF Dar es Salaam… (Pichaz)

Screen Shot 2015-08-05 at 2.56.23 PM
Ripota wa millardayo.com amefika Ofisi za Chama cha CUF Buguruni Dar es Salaam ambapo Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba alipanga kuongea na Waandishi wa Habari August 05 2015.

Kikao hicho kimeahirishwa ambapo Mwenyekiti huyo amesema ameitwa ili akaongee na wazee wa Chama hicho alafu ndio aje kuongea na Waandishi wa Habari.
Hizi ni pichaz nje na ndani kulivyokuwa.
Screen Shot 2015-08-05 at 2.56.30 PM
Screen Shot 2015-08-05 at 2.56.40 PM
Screen Shot 2015-08-05 at 2.56.49 PM
Screen Shot 2015-08-05 at 2.56.59 PM
Screen Shot 2015-08-05 at 2.57.10 PM
Screen Shot 2015-08-05 at 2.57.21 PM
Screen Shot 2015-08-05 at 2.57.33 PM

 


 


 

 


 

Share on Google Plus

About Unknown

TEAM TASABA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment