SIMULIZI ZA HADITHI

LIKE NIONE WANGAPI MTAISOMA SIMULIZI HII
SIMULIZI-NEVER SAY GOODBYE
MTUNZI-VICTOR DISMAS
SIMU(Watsaap)-0716616279
INSTAGRAM-VICTOR.DISMAS
FACEBOOK-Victor Dismas Van Manda
SEHEMU YA KWANZA
Ilikuwa ndani ya chuo kikuu cha Dar es salaam ambapo kulikuwa na kundi la wanafunzi wengi katika jengo la utawala.Kundi ilo la watu lilikuwa ni wanafunzi wapya ambao walikuja kufanya usajili katika chuo hicho kujiunga na masomo ya shahada ya kwanza.Baada ya taasisi ya elimu ya juu nchini Tanzania kutangaza majina ya wanafunzi ambao walitakiwa kujiunga na elimu ya chuo kikuu katika vyuo mbalimbali,Zoezi la kuwasajili lilianza rasmi katika kila chuo husika alichochaguliwa mwanafunzi.
Katika chuo kikuu cha Dar es salaam kulikuwa na msongamano wa wanafunzi wengi sana ambao walionekana kuchoka hasa baada ya zoezi kwenda taratibu.Kitendo kile kiliwakera wanafunzi wengi sana na wengi wao kuanza kuondoka huku wakipanga kuja siku nyingine sababu lile zoezi ndiyo kwanza lilikuwa limeanza na bado siku zilikuwa nyingi za kufanya usajili.
“Yani tangu asubuhi mpaka sasa hivi hata robo ya wanafunzi haijaisha kufanya usajili!!!”aliongea kwa kuhamaki mwanafunzi mmoja aliyeonekana kuchoshwa.
“me hapa nilipo nimechoka sana na nahitaji kuondoka”alisema mwanafunzi mwingine.
Katika tukio la kushangaza ni pale alipoonekana msichana mrembo akikatiza maeneo yale na kufanya kila mtu ageuze shingo yake kumuangalia.Hakuna mwanaume aliyethubutu kumuangalia Yule mwanamke bila kutikisa kichwa chake na kugandisha macho yake kwa Yule binti mrembo.Siyo wanaume peke yao kwani hata wanawake nao walivutiwa na kuendelea kumuangalia msichana Yule mrembo aliyekuwa anakatiza maeneo yale kwa madaha huku akichezesha nywele zake ndefu zilizoongeza urembo wake.
“msichana huyu ni nani?mbona ni mzuri sana!!”alisikika mvulana mmoja akiwauliza wenzake.
“hakika huyu ni malkia”alisikika mvulana mwingine akiongea.
“kaka zangu hapo mna haki ya kupagawa,huyu binti ni mzuri sana”alisikika msichana mmoja akiwajibu wale wakaka aliokuwa wanaongea wao kwa wao.
Tangu kupita kwa Yule msichana kulijenga taswira mpya kwa wanafunzi waliokuwa nje ya jengo lile,Kila mtu alikuwa anazungumzia uzuri wa Yule msichana .Kila mtu hakutaka kushindwa katika kuuelezea uzuri wa Yule msichana,Huku wengine wakionyesha wazi kumtamani Yule mwanamke kutokana na uzuri wake.Baadhi ya wavulana walianza kumuumba kwa maneno huku wakionyeshana jinsi alivyo
“Dah hivi Yule mtoto anakasoro gani kwenye mwili wake?”aliuliza mvulana mmoja.
“sidhani sababu amekamilika kila hidara,na kiukweli nimetokea kumpenda ghafla”alisema mwingine na kusababisha watu wote watoe kicheko.
“kaka Yule binti hautoweza kumpata hata uwe na dawa gani,Yule binti ni mali ya maprofessor ndiyo watakuwa wanajilia,wewe mwenzangu na mimi utampataje wakati hata hauna pesa wala elimu”alisema mvulana mwingine na kusababisha watu waendelee kucheka.
Wakati story zinaendelea kupamba moto muda nao ulikuwa unakimbia na kufanya watu waanze kurudi majumbani kwao huku kila mtu akihaidi aje tena pale chuoni kwaajili ya kufanya usajili huku akitaka kumuona Yule binti.Wale waliotoka mikoani walirudi sehemu zao walizofikia ili kesho yake warudi chuo kwaajili ya kuendelea na zoezi la usajili.
Katika kijiji cha mgeta mkoani Morogoro kulikuwa na kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Dominic,Dominic alikuwa ni kijana wa kwanza katika kijiji chao kupata nafasi ya kujiunga na chuo kikuu cha Dar es salaam.Hakukuwa na kijana mwingine yoyote katika kijiji chao aliyepata nafasi hiyo hasa baada ya vijana wengi wa kijiji hicho kutokupenda elimu.
Furaha aliyokuwa nayo Dominic baada ya kuchaguliwa kujiunga na chuo kikuu ndiyo furaha aliyokuwa nayo mama yake kipenzi.Mama yake na Dominic alifurahi kupita maelezo hasa baada ya mwanae kuchaguliwa chuo kikuu sababu alishaona njia ya kupata msaada kutoka kwa mwanae imekaribia.
Katika familia yao kulikuwa na watu wawili tu ambao ni Dominic na mama yake,baba yake na Dominic alifariki miaka mingi iliyopita wakati huo Dominic akiwa na umri wa mwaka mmoja.Dominic na mama yake waliishi katika kijiji hicho huku wakitegemea kilimo kama ndiyo nguzo katika maisha yao.Mama yake na Dominic alikuwa ni mkulima mzuri sana katika kijiji hicho,alijitahidi kujituma katika kilimo ili kufanya maisha yao yaende bila kuyumba yumba.
Malengo makubwa aliyokuwa nayo mama yake na Dominic ilikuwa ni kumsomesha Dominic ili afanikiwwe kupitia elimu.Mama yake na Dominic alitaka mwanae asome mpaka awe mtu mashuhuri katika nchi ya Tanzaniakwani alishachoshwa na maisha ya umasikini.Baadhi ya mazao aliyokuwa ayavuana alikuwa anauza huku mengine akitumia kama chakula pale nyumbani kwao.
“mwanangu nitapambana kufa na kupona mpaka upate elimu ya kutosha”alisema mama yake na Dominic.
“sawa mama nami nitasoma kwa bidii ili tufanikiwe katika maisha”Dominic alisema na kufanya mama yake atabasamu.
Dominic alijitahidi sana kutimiza ahadi yake ya kusoma kwa bidii kwani alionyesha uwezo mkubwa sana darasani na kusababisha kila mtu pale kijijini pamoja na shuleni wawe wanamshangaa.Sala pamoja na juhudi ya kusoma zilimsaidia kujiunga na kidato cha kwanza baada ya kufahulu vizuri masomo yake ya msingi kitu kilichomfanya mama yake afurahi.
Kaika shule ya secondary alijitahidi na kufanikiwa kufahulu kwa daraja la pili katika matokeo ya kidato cha nne,Dominic alijiunga na kidato cha tano kwa mchepuo wa HGE kwani alipenda sana aje kuwa mchumi siku za usoni.Miaka nayo ilisogea kwani Dominic alihitimu kidato cha sita na kufahulu kwa daraja la kwanza.Furaha iliongezeka katika familia yao kwani milango ya kuingia chuo kikuu ilikuwa imeshafunguka.
Dominic alifanya maombi ya kujiunga na chuo kikuu pamoja na maombi ya mkopo kama ilivyo utaratibu wa elimu ya juu.Dominic alifanikiwa kupata mkopo wa asilimia themanini huku asilimia ishirini zilizobaki alitakiwa kuzimalizia mwenyewe .Haikuwa hela kubwa sana kwani mama yake alishapanga kufa na kupona mwanae lazima asome.
“mama nahitajika kuondoka sababu zimebaki siku chache usajili ufungwe”Dominick alimuambia mama yake siku moja wakiwa wanakula chakula cha usiku
“sawa mwanangu jiandae kesho kutwa utaondoka”mama yake alisema
“sawa mama ila nitakukumbuka sana”Dominic alisem huku akimuangalia mama yake usoni.
“hata mimi mwanangu ila naomba ukazingatie kitu kinachokupeleka huko”mama yake alisema.
“mama nafahamu ni kitu gani kinachonipeleka huko na sitokuangusha”Dominic alisema.
“mwanangu mjini kuna kila aina ya starehe,mjini kuna wanawake wazuri sana ambao wanaweza kuiteka akili yako na kusababisha upoteze muelekeo wako wa kimaisha,cha msingi mwanangu ni kuwa makini na hao wanawake”mama yake alisema
“mama suala la wanawake liweke kando,mimi sitokuwa na msichana mpaka nitakapomaliza masomo yangu”.Dominic alisema kwa kujiamini na kufanya mama yake acheke sana
“mama kwanini unacheka ?”Dominic aliliza
“Mwanangu,Mapenzi na kifo vinakuja bila kukaribishwa,unaweza ukampenda mtu bila hata ya kutegemea sababu mapenzi yanakuja Ghafla na hauwezi kuyazuia.Kikubwa unachotakiwa kufanya ni kuangalia unayempenda kama nay eye anakupenda,hapo mnaweka kutengeneza mahusiano ambayo yatakuwa hayayumbishwi ,Dominic wewe si mtoto tena ila ni mtu mzima akili kichwani mwako”mama ake aliongea kwa kirefu
Dominic hakuwa na neno lingine la kuongea zaidi ya kukaa kimya huku akifikiria ni jinsi gani anaweza kuzikabiri changamoto atakazokutana nazo chuoni,Hukicheki chuo hicho kipo katika jiji lenye starehe nyingi,jiji lenye kila aina ya vishawishi.
Siku iliyofuata Dominic alifanya maandalizi ya safari na kesho yake waliongozana na mama yake mpaka Morogoro mjini kwaajili ya kupanda basi la kuelekea Dar es salaam
“mwanangu nilitaka kusahau jambo muhimu sana”mama yake alisema huku akifungua mkoba wake
“jambo gani mama?”Dominic aliuliza
“hili hapa”mama yake alisema huku akimkabidhi kitabu
“Biblia!!”Dominic alishangaa
“ndyo mwanangu kila siku jitahidi kusoma maandiko hata kama ni mstari mmoja”mama yake alisema na kumkabidhi
“asante mama “Dominic alisema
Gari lilipiga honi kuashiria kwamba linataka kuondoka.Dominic aliagana na mama yake kwa kukumbatiana kisha akapanda kwenye gari huku akimuacha mama yake machozi yakiwa yanamtoka,walipungiana mikono kwa ishara ya kuagana kisha gari likaanza kuondoka na kumuacha mama yake akilisindikiza kwa macho mpaka lilipopotea machoni mwake.
ITAENDELEA…………………………….
Huu ni mwanzo wa simulizi yetu ya Never Say Goodbye,ushirikiano wenu ndio utanifanya niwe naituma kila simu
Mungu atuongoze tuimalize salama
Share on Google Plus

About Unknown

TEAM TASABA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment