Kama unajenga ofisi na pesa inaruhusu… tazama hizi picha labda utapata idea!
Ukiangalia wenzetu wamekua na uwezo wa kutengeneza vitu vizuri ambavyo hata wakati mwingine sio vya gharama kubwa lakini vina muonekano mzuri utaomvutia hata mgeni au mteja.
Hii
inawafaa wale wanaojenga mall ndogondogo au wenye maduka ndani ya
majengo au sehemu zenye usalama.. kuna uwezekano vibanda kama hivi
vikajengwa kwa kutumia mbao na vioo na ukapata mvuto kama huu na wa
kisasa na hata gharama isiwe kubwa sana na kikaweza kuhamishika au kuwa
chepesi unapotaka kufanya mabadiliko ya muonekano.
Hii
inafaa kwa wale watu wangu wenye ufinyu wa nafasi kwenye ofisi zao,
kwenye mistari miwili ya upande wa kulia unaweza kupanga team na upande
wa kushoto ukamaliza na wakuu wa Idara, nimeikubali sana kwenye upande
pia wa Taa, na meza za mbao.
Reception
inaweza kuwa simple lakini yenye ubunifu mkubwa sana, tazama kuanzia
meza ilivyo na rangi moja, ukuta wa mbao, taa zake juu na sakafu…. nzuri
sana
0 comments :
Post a Comment