Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Old Trafford umemalizika kwa Mashetani wekundu kuendeleza ubabe dhidi ya Liverpool kwa mara ya tatu mfululizo.
Daley Blind alianza kuifungia United goli la kwanza muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza, kabla ya Ander Herrera kufunga la pili kupitia mkwaju wa penati.
Christian Benteke aliifungia Liverpool goli la kufutia machozi kwa mtindo wa ‘tik tak’ mwishoni mwa kipindi cha pili kabla ya mshambuliaji mpya wa Man United – Anthony Martial kufunga goli la 3 kwa United.
Hiki ndicho kilichowakuta Espanyol walipocheza na Real Madrid leo
Mchezo uliopigwa katika dimba la Cornella El Plat umeshuhudia mwanasoka anayeshikilia taji la uchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo akifunga magoli 5 katika mchezo uliomalizika kwa Real Madrid kushinda 6-0.
Ilimchukua Cristiano Ronaldo dakika 20 tu kufunga hat trick katika dakika ya 7, 17 na 20, kabla ya Karim Benzema hajafinga goli la 4 katika dakika ya 28 na hivyo kupelekea Madrid kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa 4-0.
Kipindi cha Ronaldo akaongeza magoli mawili katika dakika ya 60 na 80 ya mchezo huo na hivyo kukamilisha ushindi wa 6-0
Timu zilipangwa hivi
Espanyol: Lopez, Arbilla, Alvaro, Ciani (Paco Montanes 46), Duarte, Victor (Joan Jordan 64), Javi Lopez (Canas 46), Alvarez, Salva, Gerard, Caicedo
Substitutes not used: Bardi, Juan Fuentes, Raillo, Sylla
Booked: Alvaro, Canas
Real Madrid: Navas, Carvajal, Pepe, Ramos (Varane 74), Marcelo, Casemiro, Modric (Kovacic 55), Isco, Bale, Ronaldo, Benzema (Vazquez 62)
Substitutes not used: Casilla, Kroos, Arbeloa, Jese
Scorers: Ronaldo 7, 17 pen, 20, 61, 80; Benzema 28
Nimekusogezea matokeo ya Arsenal vs Stoke na Man City vs Crystal Palace
Arsenal wakiwa nyumbani waliikaribisha timu ngumu ya Stoke City- mechi ambayo imemalizika kwa vijana wa Arsene Wenger kupata ushindi wa 2-0.
Magoli ya Arsenal yalifungwa na Theo Walcott na Oliver Giroud.
Manchester City wakicheza ugenini leo wamefanikiwa kuendeleza rekodi yao ya kushinda mechi zao zote za EPL kwa goli 1-0 dhidi ya Crystal Palace.
Tayari ninayo matokeo ya mechi ya African Sports Vs Simba (+Pichaz)
September 12 ndio siku ambayo pazia la Ligi Kuu Tanzania
bara limefunguliwa kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti
tofauti, mchezo uliyokuwa umeteka hisia za watu wengi ni mechi kati ya African Sports dhidi ya Simba mechi iliyochezwa katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Mvuto wa hii mechi unatokana na rekodi ya klabu ya Simba kwa hivi karibuni kutofanya vizuri katika mechi zake za Ligi Kuu alizocheza Tanga katika uwanja wa Mkwakwani. Huku kwa upande wa African Sports
ndio wamerudi Ligi Kuu baada ya kushuka miaka kadhaa nyuma hivyo
hawakuwa tayari kupoteza mechi yake ya kwanza ya msimu, tena katika
uwanja wake wa nyumbani.
Mechi imemalizika kwa klabu ya Simba kuondoka na ushindi wa goli 1-0 goli pekee lilifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda aliyewahi kuichezea Yanga Hamisi Kiiza, kipindi cha pili. Licha ya kukosa nafasi kadhaa Simba ilifanikiwa kutumia nafasi moja kutoka kwa nahodha wao Musa Mgosi na Kiiza kutia nyavu kwa kichwa.
Golikipa wa African Sports Yusuph Yusuph akiokoa goli
Matokeo ya Chelsea vs Everton nimekuwekea hapa
Mchezo huo uliopigwa katika jiji la Liverpool ndani ya uwanja Goodison Park umemalizika kwa Chelsea kuambulia kipigo kingine kwa kufungwa 3-1.
Magoli matatu ya mshambuliaji Naismith yametosha kuipa Everton ushindi mzito dhidi ya vijana wa Jose Mourinho.
Naismith alianza kufunga katika dakika ya 17, dakika 5 baadae akaongeza la pili kabla ya Matic hajaifungia Chelsea goli la kufutia machozi.
Dakika 8 kabla ya mchezo kumalizika Naismith akashindilia msumari wa mwisho na kuipa ushindi wa 3-1 Everton.
First Eleven ya African Sports Vs Simba (+Pichaz)
African Sports mwenyeji wa mchezo huu
- Yusuph Yusuph 30
- Ayoub Masoud 2
- Mwaita Gereza 21
- Juma Shemvuni 24
- Rahm Abdalah 26
- Novat Lufungo 22
- James Mendi 5
- Hussein Amir 4
- Hassan Matemema 10
- Omary Issa 16
- Pera Mavuo 7
- Zacharia Mwaluko 1
- Alfani Twenye 23
- Ally Ramadhani 13
- Mussa Chambe 6
- Bakari Masoud 20
- Victor Hangaya 23
- Nzara Ndaro 19
- Peter Manyika
- Mohamed Hussen
- Hassan Kessy
- Juuko Murishid
- Justice Majbavi
- Awadh Juma
- Said Ndemla
- Mwinyi Kazimoto
- Mussa Mgosi
- Hamisi Kiiza
- Peter Mwalyanzi
1. Angban Vicent
2. Said Issa
3. Simon Serenkuma
4. Emery Nimubona
5. Boniface Maganga
6. Pape Ndaw
7. Issa Ngoah
Pichaz za mwanzo kutoka uwanja wa Mkwakwani Tanga African Sports Vs Simba
September 12 ni siku ambayo Ligi Kuu Tanzania bara itazinduliwa rasmi kwa michezo kadhaa kupigwa, lakini millardayo.com inakuweka karibu na moja kati ya michezo ya Ligi Kuu. African Sports ya Tanga inaikaribisha Simba Sports Club ya Dar Es Salaam hii ndio habari ya mjini kwa hapa Tanga.
Nakusogezea pichaz 22 za mwanzo kutoka Uwanja wa CCM Mkwakwani
0 comments :
Post a Comment