GOSSIP OF THE DAY WITH TASABA

Nuru The Light karudi na video yake mpyampya, inaitwa ‘L’… ni kazi ya Director Adam Juma…

Nuru The Light ni moja ya mastaa ambao wana nafasi zao kutambulika kwenye muziki wa Bongo Fleva, kuna kipindi kirefu hajasikika… haikumaanisha kauacha muziki.
Nuru anarudi tena, muziki una mchakamchaka sasahivi, ataweza kushika?? kaachia video ya ngoma yake mpya ambayo kaipa jina la ‘L’ .
Milango imefunguka sana mastaa wa Bongo kufanya Video zao nje ya TZ sanasana South AfricaNuru hajavuka huko, kaiamini kazi ya Director Adam Juma wa Visual Lab Tanzania, Video hii yote imekamilika kwenye mikono yake !

Baada ya kumaliza beef na Drake, Meek Mill anamtafuta Future…!?

Meek Mill kwenye headlines kwa mara nyingine tena, na kwa muonekano inaonekana kama Meek Mill bado hajatosheka na beefs na pengine time hii anataka kuanzisha beef lingine na msanii mwenzake wa HipHop Future!
Kwenye performance ya tamasha la ‘Made In America Festival’ siku ya jumapili September 6  jijini Philadelphia, Meek Mill alimzuia DJ wake kupiga nyimbo za Future na kumuamuru atoe nyimbo zote za Future kwenye playlist yake.
meekFutch
>>>Oya jamaa vipi wewe, unapiga sana ngoma za Future usiku huu… Kwani Future ndio msanii pekee anayerap?! Wewe vipi bwana… emu acha hizo na piga ngoma nyingine kali, huyo future bwana imetosha!!” <<< Meek Mill alisema baada ya kukerekwa na nyimbo hizo.
Hakuna anayejua kwanini Meek Mill aliamua kumwambia DJ wake hivyo, na hakuna anayejua kwa nini nyimbo hizo zimesababisha kikwazo kwa rapper huyo… imepita mwezi tu toka Meek Mill na Drake wamalize beef lao, pengine Meek anataka aanzishe lingine na Future!
Wewe unaonaje?

Diamond Platnumz ametaja tarehe atakayoonekana sura mtoto wake (Tiffah)

Kama umekua ukifuatilia akaunti za Diamond Platnumz na mpenzi wake Zari tangu mtoto wao Tiffah azaliwe utakua umekutana na picha nusu ambayo anaonekana mtoto wao huyo na sehemu kubwa hua ni kuanzia kwenye kidevu kushuka chini.
tifHii imekua ni style nyingine ya mastaa wetu kadhaa kuchukua mfumo huu wa kutowapost au kuwaonyesha watoto wao hadi umri fulani ufike,Diamond Platnumz leo ametaja siku ambayo mtoto wao huyo ataonekana sura kwa wale ambao bado hawajapata nafasi ya kumuona.

Hii ndio Shopping Mall iliyopewa jina la rais Jakaya Mrisho Kikwete 88.1 (Mwanza)

.
.
Stori ninayokusogezea sasa hivi ni hii kutokea 88.1 Mwanza kuhusu Shopping Mall mpya inayotarajiwa kufunguliwa wakati wowote ambayo itakuwa ikiitwa jina la rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.
Kwa mujibu wa afisa mahusiano wa jiji la Mwanza alipokutana na ripota wa millardayo.com..‘Tumeamua kuita Jakaya Mrisho Kikwete kwasababu ni utamaduni wa muda mrefu kwa kweli za utamaduni kwamba inapotokea kiongozi akafanya jambo jema na ni zuri basi vitu uwa vinaitwa kwa jina lake ukaona kuna baadhi ya barabra zimepewa majina kama ya Kenyatta,Nyerere’ – Joseph Mlinzi
.
.
‘Katika hili la Jakaya Mrisho Kikwete Shopping Mall ni kwa utambuzi kwamba huyu ni rais wa jamhuri wa Muungano wa Tanzania ambaye ameongoza kwa awamu mbili mfululizo ameweka mchango mkubwa katika nchi yetu kipindi cha utawala wake ikiwa pamoja na utekelezaji mzuri kupitia chama cha Mapinduzi’ – Joseph Mlinzi
DSC_0020
.
‘Shopping Mall hii ni kubwa kwa Afrika Mashabiki na kati kwa mfano ukienda Dar Mlimani city ambayo ina mita za mraba 15000, ukienda Kenya wana Westgate ambayo haifiki mita za mraba 30000, ukienda za Uganda na sehemu zingine, mwisho wa siku tulitaka kufanikisha yale maono ya Mheshimu Rais kwamba katika jiji la mwanza tunaona kitu kizuri bora na kinaelekea kule ambako yeye alisema anataka jiji la mwanza liwe kama California ya Tanzania’ – Joseph Mlinzi
.
.
.
.
.
.

Nimekusogezea list ya viongozi wanaolipwa pesa nyingi duniani…

.
.
Ninayo list ya viongozi wa mataifa mbalimbali duniani wanaoongoza kwa kulipwa pesa nyingi , taarifa ikufikie kwamba anayeshika nafasi ya tano ni Michael D. Higgins ambaye ni rais wa jamhuri ya Ireland, nafasi ya nne inashikwa na waziri mkuu wa Australia Tony Abbott, nafasi ya tatu inashikwa na rais wa Marekani Barack Obama, nafasi ya pili inashikwa na kiongozi wa Hong Kong  Leung Chun-ying mshahara wake unauzidi mshahara wa rais wa China.
Nafasi ya kwanza wanasema katika viongozi wa mataifa mbalimbali duniani anayelipwa pesa nyingi ni waziri mkuu wa Singapore Lee Hsien Loong.
.
.
Waziri Mkuu huyo ndio kiongozi wa taifa anayelipwa kwa mshahara mkubwa duniani akiwa analipwa dola za kimarekani milioni 1 na laki 7.

Mashtaka dhidi ya Masha batili?, Karatasi za kura September 29, Sheria za kampeni… vivutio vya utalii CNN na BBC!?

Inawezekana ulikuwa kwenye foleni na uchambuzi wa magazeti @CloudsFM umekupita, kazi yangu siku zote ni kuhakikisha zile zote kubwa za asubuhi hazikupiti…
Mgombea Urais wa CHADEMA Edward Lowassa asema hakuta kuwa na muda wa kupoteza, ataanza  kufanyia kazi ahadi zote alizotoa baada ya kuapishwa, Mgombea Urais wa CCM John Magufuli asema kama akichaguliwa kua Rais hakutakuwa na maadhimisho ya siku ya maji.
Mgombea Ubunge wa ACT Wazalendo jimbo la Chilonwa, Eva Mpagana amewaomba wananchi kumteuwa ili aweze kutatua tatizo la mawasiliano, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu amesema hakuna Sheria inayozuia wagombea Urais, Ubunge na Madiwani kufanya kampeni zaidi ya saa kumi na mbili jioni.
Chama cha TPP kimeonywa kuhusu kuendelea na kampeni, Lawrence Masha adai mashtaka dhidi yake ni batili, Rais mstaafu Benjamin William Mkapa anategemea kuzindua kampeni za CCM Bukoba.
Karatasi za kura kutua September 29 , vivutio vya Utalii nchini kurushwa kwenye vituo vya CNN na BBC wakati wowote kuanzia sasa, Waalifu wawili watoroka kwenye kituo cha polisi, Sheikh mkuu wa Dar es salaam Alhaj Musa Salum asema mchakato wa kumpata Mufti mkuu wa Tanzania kufanyika ndani ya siku 90.
Mfanyabiashara afikishwa Mahakamani baada ya kuingiza samaki nchini kutoka China bila kuwa na kibali maalum.

 


 

 


 


 


 

Share on Google Plus

About Unknown

TEAM TASABA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment