Wiz Khalifa na Ty Dolla $ign kuachia movie…!?
Wiz Khalifa na Ty Dolla $ign wanaziandika headlines siku ya leo, baada ya kuachia collabo yao ‘Talk About It In The Morning’ mwezi March mwaka huu, wawili hao wana mpango wa kuipeleka project hiyo mbele zaidi.
Siku ya Jumatatu, wawili hao waliachia teaser ya kile wanachodai kuwa movie yao mpya iliyopewa jina la wimbo wao ‘Talk About It In The Morning’.
Hawajasema mengi sana kuhusiana na movie hiyo ila kwa muonekano tu wa ‘teaser’
hiyo, tutegeme chochote kwenye movie ya wawili hao… watu wengine
wamekuwa na wasiwasi kuwa kama teaser ya movie hiyo iko hivi ilivyo basi
pengine hata kibali cha kucheza movie hiyo kwenye nyumba za sinema
itakuwa ngumu kupata!
0 comments :
Post a Comment