Ufisadi CCM na UKAWA, Lowassa na Kikwete, , CCM Zanzibar, Waislam wa Tz Mecca?

Ufisadi CCM na UKAWA, CCM Zanzibar, Lowassa na Kikwete, Waislam wa Tz Mecca?

Magazeti ya Jumatatu 14 September 2015 yako mtaani tayari kama uchambuzi wa magazeti @CloudsFM umekupita ninazo hapa zile zote kubwa kwenye vichwa vya habari leo..
Lowassa asema Kikwete ameshindwa kutimiza yale aliyoahidi kwa muda wa miaka 10 ya uongozi wake, Tundu Lissu amtaka Rais Kikwete aseme RICHMOND ya nani, Mgombea Ubunge wa Lushoto kupita CHADEMA Mohamed Mtoi afariki dunia kwa ajali ya gari.
CCM wazindua kampeni kwa kishindo Zanzibar, John Magufuli asema Serikali yake itatoa kipao mbele kwa wakulima na wafugaji, Rais Kikwete asema CCM ushindi hauwezekani bila watu wa Zanzibar kujipanga.
Lori lavamia msafara wa mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Magufuli, Zitto Kabwe asema CCM haibadiliki hata waje malaika , Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi amesema hakuna taarifa za vifo vya waislam wa Tanzania walioenda kuhiji ibada Mecca.
Hoja ya ufisadi yaigawa CCM na UKAWA, Zanzibar imeanza mazungumzo na kampuni ya Shell Uingereza kwa ajili ya kuchimba mafuta, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imekemea vurugu, uvunjifu wa amani na fujo wakati huu wa kampeni, Rais Kikwete kuzindua barabara ya Malagarasi.

 

Share on Google Plus

About Unknown

TEAM TASABA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment