Tume ya uchaguzi imepokea rufaa ngapi kutoka kwa Wabunge na Madiwani?, stori iko hapa..
Tukiwa bado kwenye headlines za Uchaguzi
2015, taarifa kutoka tume ya Uchaguzi NEC imesema imepokea rufaa za
wabunge na Madiwani wa Halmashauri.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa huduma za
kisheria wa tume ya Uchaguzi, Emmanuel Kawishe akizungumza na ripota wa
millardayo.com alisema..’Ni kweli tume ya
uchaguzi ilipokea rufaa ya wabunge na madiwani na zimezifanyia maamuzi
katika vikao mbalimbali kilianza tarehe 31, kikafanyika tarehe tena 1, 2
na baadae kikafanyika tarehe 5 kwa hiyo imeziamulia rufaa za wabunge 49
zingine unakuta kwamba walirudia kuleta mara mbili kwa hiyo
waliziamulia zikabaki rufaa kama mbili tu za wabunge ambazo zinasubiri
taarifa na maelezo kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi’ – Emmanuel Kawishe
‘Kwa
upande wa Madiwani mpaka kufikia juzi zilikuwa zimeshaamuliwa rufaa
zaidi ya 160 kwa hiyo sasa hivi tunazo kama 30 ambazo vielelezo
tumeshapokea na tunaendelea kuandikia na hivi punde tume itaendelea
kuzitoa ili wananchi waweze kujua hatima ya yale ambayo wanataka tume
kuamulia kwa misingi ya rufaa’- Emmanuel Kawishe
0 comments :
Post a Comment