top Hit gossips with TASABA

Mabibi na mabwana ile single mpya ya Sauti Sol ndio hii imetoka

Sauti Sol ni kundi la muziki kutokea Kenya wametuletea video yenye  Lyric ya nyimbo yao mpya  waliyoipa jina la Isabella ikiwa bado mpya kabisa mtuwangu
sauti-sol-picture_wide-f30ea33679f0eac215ec6d435bc587421778e8bb-s6-c30

Ushauri wa Arsene Wenger kwa Thierry Henry kama anataka kupata mafanikio katika ukocha…

Kocha wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger ambaye amewahi kumfundisha Thierry Henry kama mchezaji wake kwa miaka mingi, Wenger amemshauri Thierry Henry kama kweli ana nia ya dhati ya kutaka kupata mafanikio kama kocha katika soka.
2C00228A00000578-0-image-a-5_1441721092573
Wenger amemshauri Henry ambaye kwa sasa anaifundisha timu ya Arsenal chini ya umri wa miaka 18 kuwa, kama kweli anataka kupata mafanikio katika ukocha inabidi apate ushauri wa kisaikolojia katika akili yake. Henry anafundisha kikosi hicho cha vijana huku akipata mafunzo  ya ukocha.
0F6507DB00000578-0-image-a-3_1441721083367
Henry ambaye anaheshima ya kuwa mfungaji bora wa klabu ya Arsenal kwa muda wote, alisajiliwa na Wenger akitokea klabu ya Juventus ya Italia mwaka 1999 ila Wenger amemueleza utofauti uliyopo kati ya kuwa mchezaji na kuwa kocha.

Picha 10 kutoka uwanja wa Tangamano Tanga kwenye kampeni za Urais za Mh.John Magufuli

7mgflKasi ya Wanasiasa kuzungumza na wapiga kura wao kwa sasa ndiyo stori ambayo inazungumzwa karibu kila kona ya Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambapo kwa Tanzania tutakua tunamchagua Rais wa awamu ya tano.
8mgflChama Cha Mapinduzi (CCM) kinaendelea kumnadi mgombea wake Urais Dr. John Magufuli na septemba 8 2015 walikua Tanga kwenye uwanja wa Tangamano ambapo wananchi wengi walijitokeza kwa ajili ya kumsikiliza Mgombea Urais,Ubunge na Madiwani.
1mgflKampeni hizi ziliambatana na utoaji wa burudani kwa wasanii kadhaa akiwemo Diamond Platnumz,Alikiba,Yamoto Band,Barakah Da Prince,Marlaw,Kassim Mganga,Matonya,Mwana Fa,Chege na Temba,Isha Mashauzi,Khadija Kopa,Mzee Yusuph na wengine.
14mgfl
Diamond Platnumz
13mgfl
Alikiba
11mgfl
Miongoni mwa vijana wanaounda Yamoto Band.
10mgfl
Kundi la Orijino Komedi
9mgfl
8mgfl
Wananchi waliokuja kumsikiliza Mgombea Urais John Magufuli.
7mgfl

 

Nimekusogezea na hizi nyumba 10 kali zilizojengwa ndani ya maji mtu wangu…(Pichaz)

Kati ya vitu ambavyo huwa vinanivutia nia aina ya nyumba na jinsi zilivyojengwa kwa ufundi mkubwa.
Leo nimekusogezea hizi nyumba ambazo zimekuwa zikitumiwa na watu bila wasiwasi wowote huku zikiwa zimejengwa kitaalamu zaidi ndani ya maji.
MANS1
MANS2
MANS3
MANS4
MANS5
MANS6
MANS7
MANS8
MANS9
MANS10

 

Ninayo good news kutoka kwa bondia Francis Cheka iko hapa….

.
.
Unakumbuka ile ishu ya bondia wa ngumi Francis Cheka ya kumpiga na kumuumiza meneja wa baa yake akimtuhumu kusababisha hasara?
Sasa good news ninayotaka kukusogezea ni kwamba bondia huyo wa mchezo wa masumbwi akiwa anatumikia kifungo cha nje kwa sasa anatarajia kwenda nchini Uingereza tarehe 15 mwezi huu kwenye mchezo wa masumbwi.
Leo sept 8 alikuta na ripota wa millardayo.com na kuzungumza machache kuhusiana na taratibu za safari yake pamoja na kifungo anachotumikia nje…’Kwanza namshukuru mwenyezi mungu niko katika hali ya salama kesi yangu katika ustawi wa jamii inaendelea vizuri na ustawi wa jamii niko nao katika hali ya kawaida sababu wao wanajua umuhimu wangu na kuweza kujua mimi Francis Cheka nahitaji nini kwa mashabiki wangu, mimi ni mtanzania ambaye ninawajenga umma wa watanzania kwenye michezo ya boxer’ – Francis Cheka
‘Ustawi wa jamii wamenipa ruksa ya kwenda kupigana kwenye pambano hilo nchini Uingereza nategemea kwenda tarehe 15 mwezi huu na mkurugenzi wa ustawi wa jamii ameweza kuniambia mawili matatu kuhusiana na taratibu au kitu gani ninachotakiwa kukifanya ili niweze kufanikisha safari yangu ya Uingereza’ – Francis Cheka

Kuhusu Kipre Bolou, hali ya Shomari Kapombe na Allan Wanga viko hapa kuelekea mechi ya Jumamosi 

Wakati shirikisho la soka Tanzania TFF likithibitisha kuanza kwa Ligi Kuu soka Tanzania bara siku ya Jumamosi ya September 12 na kudai mpango wa kuwataka vilabu viwalipie wachezaji wa kigeni dola 2000 upo pale pale. Kwa upande wa Azam FC kupitia kwa afisa habari wake Jafari Iddi Maganga amethibitisha kurejea kwa wachezaji wao.
Awali klabu ya Azam FC katika mchezo wa Ngao ya Hisani iliwakosa wachezaji wake wawili Kipre Bolou aliyekuwa majeruhi na Allan Wanga ambaye alifiwa na mama yake mzazi. Wanga amerejea baada ya kukosekana kwa kufiwa na mama yake na kuitumikia timu yake ya taifa ya Kenya.
Wilfred Michael Bolou (R) Azam FC from Tanzania tackes Amehe Belete of Adamma City FC of Ethiopia during their Cecafa Kagame Club Cup 2014 championship at Kigali Regional Stadium in Nyamirambo on August 16,2014.Photo/Stafford Ondego/www.pic-centre.com/CECAFA (RWANDA)
Kipre Bolou mwenye jezi nyeupe
“Kipre Bolou ambaye alikuwa ameenda Cape Town kwa matibabu, amerejea jana usiku tumempokea na alienda kule kwa ajili ya matibabu yake na tutakuwa naye kwa muda wa mwezi mmoja akiangalia afya yake na wakati huo huo akiandaliwa kucheza katika Ligi Kuu” >>> Jafari Iddi Maganga
“Utaratibu wa madaktari ni kwamba amekwenda wameangalia afya yake na wamesema kuwa hawawezi kumfanyia upasuaji kutokana na hali aliyokuwa nayo lakini wametoa maelekezo kwa madaktari wetu kitu gani kwamba anapaswa kufanyiwa ili aweze kurudi uwanjani”>>> Jafari Iddi Maganga

Comedy

Kipaji kingine cha mbwa… jamaa akaona amtumie kumshikia wine yake…

Mbwa ni moja ya wanyama wanaopewa nafasi kubwa ya kuwa karibu na binadamu na mara nyingi kwa nchi za kwetu wamekuwa wakitumika kama walinzi.
Lakini kwa wenzetu mbwa amekuwa sehemu ya familia na wamekuwa wakipewa huduma zote ambazo binadamu wengine wanazipata.
Wako wengine ambao hutumia gharama kubwa kuwatunza mbwa wao pamoja na kuwafundisha mambo mbalimbali.
Eve anaiyeishi Carlifonia,Marekani yeye aliamua kumfundisha mbwa wake jinsi ya kubalance glass yenye wine kichwani huku akiwa hana wasiwasi wowote.
Tazama hapa alichofanya…
emp

dog2

dog3

dog4
Nimekuwekea na video yake kabisa mtuwangu…


 


 


 


 

 

Share on Google Plus

About Unknown

TEAM TASABA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment