TOP SPORT NEWS OF THE DAY,

Mtoto wa mchezaji bora wa dunia kutokea Brazil amejiunga na klabu hii ya Ureno….

Mtoto wa mchezaji wa zamani wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Rivaldinho Rivaldo ambaye anafuata nyayo za baba yake Rivaldo katika soka, amesajiliwa na klabu ya Boavista ya Ureno akitokea klabu ya Mogi Mirim ya kwao Brazil. Hivyo hiyo inakuwa mwanzo wa safari yake ya kusaka mafanikio kama aliyoyapata baba yake Ulaya.
ng887322E8-A487-4317-B9AD-945B6421D929
Rivaldinho ambaye ana umri wa miaka 20 amejiunga na klabu ya Boavista kwa mkataba wa miaka mitatu na kuhama katika klabu ambayo baba yake mzazi ni Rais, hiyo itamfanya kukua na kukomaa kisoka kwani ataanza kuishi mbali na uangalizi wa baba yake.
ng4618719
Mchezaji huyo ambaye amepata umaarufu kutokana na ukubwa wa jina la baba yake, ni kawaida kuingia katika headlines kila mara anapofunga goli, ameichezea klabu ya Mogi Mirim jumla ya mechi 44 na kufunga goli 10. Rivaldinho ili aweze kufikia rekodi za baba yake inabidi ajitume kwani hadi sasa hajawahi cheza katika timu ya taifa ya Brazil hata ya vijana.

Ujenzi wa Uwanja mpya wa Chelsea utafanana kitu hiki na Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam (Pichaz)

Klabu ya Chelsea ya Uingereza imeonyesha muonekano wa uwanja wao mpya ambao hadi mwaka 2020 inaripotiwa ujenzi wa uwanja huo utakuwa umekamilika. Bado mashauriano yanaendelea kuhusiana na wakazi wa eneo husika utakapo jengwa uwanja huo.
2BDA18B000000578-0-image-a-4_1441054162717
Mpango wa mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich ni kutumia pound milioni 500 katika ujenzi wa uwanja huo ili uwe biashara tofauti inayojitegemea mbali na Chelsea. Ujenzi huo ambao unatarajiwa kuanza baada ya miezi 9 kutokea sasa utaifanya klabu ya Chelsea kuhama uwanja wao wa Stamford Bridge na kutumia Uwanja wa Wembley kwa kipindi cha misimu mitatu.
2BDA1DDF00000578-3217477-image-a-1_1441068450794
Ujenzi huo wa Uwanja mpya wa Stamford Bridge utakuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000 sawa na uwanja wa Taifa wa Dar Es Salaam, ambapo uwanja wa sasa wa Chelsea unachukua watu wasio zidi 41,000.
2BDA18F000000578-0-image-a-1_1441054152161
2BDA13FB00000578-0-image-a-5_1441054173682
2BDA190700000578-0-image-a-2_1441054154803
Stamford-Bridge-Chelsea-007
Huu ni muonekano wa sasa wa Uwanja wa Stamford Bridge

Pichaz za baadhi ya mastaa waliowasili katika timu zao za taifa, Ronaldo, Depay na Sanchez wapo pia..

Wiki hii ni wiki ya mechi za kimataifa kwa upande wa bara la Ulaya wao timu zao za taifa zitakuwa na mechi za kuwania kufuzu kucheza michuano ya Euro2016, ila kwa upande wa Afrika timu za taifa zitacheza michezo ya kuwania kufuzu katika michuano ya AFCON 2017.
2BD8659C00000578-3217081-image-m-37_1441032271425
Memphis Depay wa Man United akiwa Uholanzi
Cristiano Ronaldo tayari yeye ameshajiunga na timu yake ya taifa ya Ureno na kuanza mazoezi. Timu ya taifa ya Ureno yenyewe itacheza mechi moja ya kirafiki siku ya Septemba 4 dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa kabla ya kusafiri kwenda kucheza mechi na Albania ya kuwania kufuzu Euro 2016.
Alex Sanchez naye amejiunga na timu yake ya taifa ya Chile kujiandaa na mechi za kimataifa za kirafiki ambazo zipo katika kalenda ya FIFA alipiga picha na kuweka katika mtandao wa twitter. Chile wataikaribisha Paraguay siku ya Jumamosi ya Septemba 5.
sanchez
2BD8629600000578-3217081-image-a-38_1441032287637
Arjen Robben akiwa Uholanzi tayari

Sababu ya kushindwa kusajiliwa De Gea Real Madrid na maamuzi ya klabu hiyo kwa FIFA viko hapa…

Golikipa wa kimataifa wa Hispania ambaye anaichezea klabu ya Manchester United David De Gea, alikuwa akihusishwa kujiunga na klabu ya Real Madrid ya Hispania, hivyo kila kitu kilikuwa kimesha kuwa sawa ikiwemo maslahi binafsi ya mchezaji.
Football - Manchester United v Arsenal - Barclays Premier League - Old Trafford - 17/5/15 Manchester United's David De Gea applauds fans as he walks down the tunnel after being substituted after sustaining an injury Reuters / Phil Noble Livepic EDITORIAL USE ONLY. No use with unauthorized audio, video, data, fixture lists, club/league logos or "live" services. Online in-match use limited to 45 images, no video emulation. No use in betting, games or single club/league/player publications. Please contact your account representative for further details.
De Gea ambaye aliripotiwa usiku wa August 31 kuwa karibu na kujiunga na Real Madrid timu aliyokuwa akihusishwa kujiunga nayo tokea zamani, mpango wa De Gea kujiunga na timu hiyo ulikwama baada ya viongozi wa Man United kuchelewa kutuma mikataba katika klabu ya Real Madrid, hivyo walituma dakika moja baada ya dirisha la usajili kufungwa.
1415622744685_wps_11_David_De_Gea_of_Mancheste
Tatizo la kuchelewa kwa documents za mikataba hiyo ni mfumo wa usajili wa FIFA ndio umefanya documents kutoka klabu ya Man United kuchelewa kufika kwa Real Madrid, kutokana na Real Madrid kuwa na ushaidi wa hizo documents watakata rufaa FIFA ili wapewe nafasi ya kumsajili De Gea nje ya muda wa usajili kwani mfumo wa FIFA ndio uliochelewesha usajili huo.
51940-lsh
Klabu ya Real Madrid ya Hispania na Man United walikuwa wamekubaliana kuuziana golikipa huyo kwa ada ya pound milioni 29 pamoja na kupewa golikipa Keylor Navas, kama rufaa yao haitashinda watalazimika kusubiri hadi dirisha dogo mwezi January, dirisha la usajili kwa upande wa Hispania na Ufaransa tayari yashafungwa.

 


 

 


 


 

Share on Google Plus

About Unknown

TEAM TASABA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment