Slaa kuzungumza leo, Magufuli aahidi ajira kwa 40%, Lowassa asema ‘msiogope’ +Sheria ya Mitandao leo.
Tarehe 1 September 2015 imeanza na uchambuzi wa magazeti @CloudsFM, kazi yangu ni kukusogezea zile zote zilizoweka headlines kwenye magazeti baadhi zikiwa…
John Magufuli ahaidi ajira kwa 40% kupitia sekta ya viwanda, Mgombea Urais kupitia CHADEMA Edward Lowassa awaomba Watanzania wasiogope kwani atatumia pesa za mradi wa gesi kuboresha elimu kwanzia shule ya msingi hadi elimu ya juu. .
Baada ya ukimya wa zaidi ya mwezi mmoja na kutokuonekana hadharani katibu mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa anategemea kuzungumza na waandishi wa habari leo… Hatimaye Jimbo la Segerea laachiwa kwa CUF na la Kigamboni kuangukia mikononi mwa CHADEMA.
Ahadi za mgombea Urais kupita CHADEMA zimeanza kuichanganya Serekali… Sheria ya Makosa ya Mitandao kuanza kutumika rasmi leo huku wengi waonywa kuhusu matumizi mabaya ya mitandao na Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata majambazi 38 waliokuwa wakijihusisha na matukio na vitendo vya kigaidi kati yao wapo vijana wenye umri chini ya miaka 16.
0 comments :
Post a Comment