Real Madrid wako tayari kumuuza Cristiano Ronaldo kwenda PSG, ila…
Klabu ya Real Madrid ya Hispania
ni klabu ambayo inasifika kwa kupenda kununua wachezaji kwa gharama ya
juu maadam iwe inamuhitaji basi itatoa fedha ili kukamilisha usajili
wake. Headlines ambayo ipo katika vyombo vya habari ni kuhusiana
na klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa ambayo inahusishwa kutaka kumsajili Cristiano Ronaldo.
Kabla ya dirisha la usajili kufungwa klabu ya PSG ilikuwa ikihusishwa kutaka kumsajili Cristiano Ronaldo ila klabu ya Real Madrid ya Hispania hawakuwahi kutoa majibu yoyote kuhusu mpango huo. September 10 kupitia kwa Rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez amesema kama PSG wanamuhitaji Ronaldo hakuna shida ila waje na pound milioni 728.
“Kama PSG
wanamuhitaji Cristiano Ronaldo ni kazi rahisi na wala hakuna tatizo,
wanatakiwa kulipa pound milioni 728, hakuna nabii katika mchezo wa mpira
wa miguu yoyote anaweza kuuzwa lakini hatuhitaji kumuuza mwaka 2016
kwani bado ana mkataba wa miaka mitatu umebakia”>>> Florentino Perez
Cristiano Ronaldo alijiunga na klabu ya Real Madrid mwaka 2009 akitokea klabu ya Manchester United ya Uingereza kwa dau la pound milioni 80, dau ambalo liliweka rekodi ya dunia, ila klabu ya PSG ipo tayari kumsajili mshambuliaji huyo kwa dau la pound milioni 87, hii ilikuwa kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Idadi ya wanaoutaka Urais FIFA yaongezeka…Huyu mwingine katangaza nia!!
Uchaguzi wa Rais wa Shirikisho la
soka duniani umepangwa kufanyika Februari mwakani na tayari kuna baadhi
ya wanamichezo wamejitokeza kuwania naasi hiyo.
Wengine ni Rais wa shirikiso la soka barani Ulaya UEFA Michel Platini na Chung Mong-Joon wa Korea Kusini wameonesha nia yao kuwania nafasi hiyo.
Mwanamfalme wa Jordan Ali Bin Al-Hussain ametangaza kuwa atasimama kuwania nafasi hiyo kuwa duniani ili kurithi nafasi ya Rais wa sasa anayestaafu Sepp Blatter.
Wakati wa uzinduzi wa kampeni zake mwanamfalme huyo aliahidi kufanya
mageuzi katika uongozi wa soka,kupambana na rushwa na kuimarisha soka la
wanawake.Mgombea huyo alipoteza ushindi mwezi Mei ambapo Sepp Blatter alishinda kabla ya kutangaza kujiuzulu wadhifa huo.
Maafisa wa ngazi ya juu ya FIFA wanatuhumiwa kuhusika na rushwa na mamlaka za Marekani mapema mwaka huu.
Hizi ni sababu za viongozi wa Tottenham Hotspur kumkataza mchezaji huyu kununua gari lenye rangi nyekundu…
Klabu ya Tottenham Hotspur ambayo makao makuu yake ni jiji la London imemzuia winga wa kimataifa wa Korea Kusini Son Heung-Min kununua gari lenye rangi nyekundu. Spurs ambao wanajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu weekend hii dhidi ya Sunderland wametoa sharti hilo kwa Son Heung-Min.
Stori kutoka mtandao wa mirror.co.uk Son Heung-Min anatajwa kuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya soka kutokea bara la Asia, lakini amethibitisha kuzuiwa na viongozi wa Spurs kununua gari lenye rangi nyekundu kwa sababu ni rangi ambayo inatumiwa na wapinzani wao Arsenal.
“Viongozi
wa Tottenham tayari wameniambia siruhusiwi kununua gari lenye rangi
nyekundu, nina furaha kucheza mechi yoyote ile dhidi ya Arsenal na
ninapenda kushinda kwa sababu mimi ni mshambuliaji, rekodi yangu ya
ufungaji itaongea kwa ajili yangu”>>> Son Heung-Min
Son Heung-Min alisajiliwa na klabu ya Tottenham Hotspur kwa dau la pound milioni 22 akitokea klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani na kusaini mkataba wa miaka mitano, Son Heung-Min amecheza mechi 87 na kufunga magoli 29 akiwa na klabu ya Bayer Leverkusen.
Kombe la shirikisho kurejea Tanzania, pichaz za uzinduzi na mengineyo vipo hapa..
Hii ni good news nyingine katika soka la Tanzania, Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF September 10 limetangaza kuingia mkataba na Azam Sports wa kudhamini na kurudisha kombe la shirikisho Tanzania, mkataba huo wa kipindi cha miaka minne umesainiwa na Rais wa TFF Jamal Malinzi na mkurugenzi mtendaji mkuu wa Azam Media Rhys Torrington.
Rais
wa TFF Jamal Malinzi (kushoto) akiwa na afisa mtendaji mkuu wa Azam
Media Rhys Torrington wakisaini mkataba wa miaka minne wa udhamini wa
ASFC.
Malinzi
amesaini mkataba wenye thamani ya bilioni 3.3 za kitanzania ambao
utadumu katika kipindi cha miaka minne, mkataba huo wa udhamini
utahusisha mdhamini kugawa vifaa kwa timu shiriki, hela ya nauli kwa
timu itakayosafiri kwenda kucheza ugenini na marefa watalipwa katika
viwango vile vile wanavyolipwa Ligi Kuu.
Timu zitakazoshiriki ni 64 ambazo ni
mjumuisho wa timu za Ligi Kuu, Ligi daraja la kwanza na Ligi daraja la
pili, timu itakayokwenda kucheza ugenini itapewa Tsh milioni 3 kama
gharama ya usafiri na itakayocheza nyumbani itapewa Tsh milioni 1.
Mshindi wa kombe hilo ambalo litakuwa likiitwa Azam Sports Federation Cup (ASFC) atapata zawadi ya kombe pamoja na Tsh milioni 50 na kupewa nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Kurejea kwa kombe hili ambalo mara ya mwisho ilikuwa mwanzoni mwa miaka
ya 2000, kunaondoa nafasi ya mshindi wa pili wa Ligi Kuu Tanzania bara kushiriki Kombe la shirikisho barani Afrika.
Ratiba ya Sept 12 na 13 ya Ligi Kuu Tanzania, Uingereza, Hispania na Italia zipo hapa mtu wangu…
Baada ya mapumziko ya mechi za
kimataifa, weekend ya September 12 na 13 kuna michezo za kadhaa ya Ligi
Kuu mbalimbali inachezwa huku kwa Tanzania September 12 ndio siku ya
kuanza kwa Ligi Kuu soka Tanzania bara. Mtu wangu wa nguvu nakusogezea
karibu yako ratiba ya baadhi ya Ligi uzipendazo.
Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania bara September 12 na 13
Ratiba ya Ligi Kuu Uingereza September 12 na 13
Hii ni ratiba kwa saa ya Afrika Mashariki
- Everton Vs Chelsea saa 14:45
- Arsenal Vs Stoke saa 17:00
- Crystal Palace Vs Man City saa 17:00
- Norwich Vs Bournemouth saa 17:00
- Watford Vs Swansea saa 17:00
- West Brom Vs Southampton saa 17:00
- Man United Vs Liverpool saa 19:30
- Sunderland Vs Tottenham saa 15:30
- Leicester Vs Aston Villa saa 18:00
Ratiba ya Laliga kwa saa za Afrika Mashariki
- Espanyol Vs Real Madrid saa 17:00
- Sporting de Gejon Vs Valencia saa 19:15
- Atletico Madrid Vs FC Barcelona saa 21:30
- Real Betis Vs Real Sociedad saa 23:00
- Granada CF Vs Villarreal saa 13:00
- Ath Bilbao Vs Getafe saa 17:00
- Celta de Vigo Vs Las Palmas saa 19:15
- Malaga Vs Eibar saa 21:30
Ratiba ya Italia kwa saa za Afrika Mashariki
- Fiorentina Vs Genoa saa 19:00
- Frosinone Vs Roma saa 19:00
- Juventus Vs Chievo saa 21:45
- Verona Vs Torino saa 13:30
- Empoli Vs Napoli saa 16:00
- Palermo Vs Carpi saa 16:00
- Sapdoria Vs Bologna 16:00
- Sassuolo Vs Atalanta saa 16:00
- Lazio Vs Udinnese saa 19:00
- Inter Milan Vs AC Milan 21:45
Kocha Van Gaal kamtetea Anthony Martial ?? Cheki na pichaz Martial alivyoyaanza maisha Uingereza..
Kocha wa Manchester United Louis van Gaal amemtetea mapema mshambuliaji mpya wa klabu hiyo Anthony Martial kuwa itachukua muda kuizoea Ligi Kuu Uingereza, hivyo wasitegemee kuanza kwa kufanya vizuri au kufunga magoli, kauli hii inakuja ikiwa ni saa chache zimesalia kabla ya Man United kucheza mechi dhidi ya Liverpool.
Mshambuliaji huyo wa kifaransa alisajiliwa na Man United wakati wa mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa, hivyo Van Gaal anajaribu
kuwashauri mashabiki wampe muda wa kutosha kwanza wa kuizoea Ligi kabla
ya kuanza kufanya vizuri, kwani ada ya pound milioni 36 aliyosajiliwa
kutokea Monaco ni kiasi kikubwa ukilinganisha na umri wake hivyo mashabiki wengi huenda wakawa na matarajio makubwa.
Kwa upande wa Anthony Martial ameonekana akifanya matembezi na mkewe Samantha na mtoto wao katika jiji la Manchester, huku akionekana kufurahia maisha mapya katika jiji la Manchester. Martial anapewa nafasi kubwa ya kucheza katika mechi dhidi ya Liverpool, hivyo kutokana na usajili wake kugharimu fedha nyingi, huenda mashabiki wakatarajia makubwa kutoka kwake.
0 comments :
Post a Comment