Majibizano kati ya Soundcity TV na manager wa P Square yanaendelea… hili ndio tamko la Soundcity!!

Majibizano kati ya Soundcity TV na manager wa P Square yanaendelea… hili ndio tamko la Soundcity!!

Beef la Soundcity TV na P Square ikiwemo manager wao Jude Okoye bado linaendelea na pengine litaendelea kwa muda mrefu.
Soundcity TV imekerekwa na kauli ya manager wa P Square Jude Okoye iliyosema kuwa; “nyinyi mnapata mamilioni ya pesa lakini wasanii hawalipwi fungu lao kwenye hayo mamilioni”…  kwa hasira wamepost picha inayoonyesha kama kumshushia heshima manager wa P Square na kuandika ujumbe mrefu sana kujibu tuhuma hizo…
SOUND2

Cha kwanza ambacho Soundcity TV imesema ni kwamba wanatambua kuwa hawawapi P Square favour yoyote kwani wakiwa na kazi nzuri na wakiileta kwenye kituo hicho, Soundcity haitakiwi kuikataa bali kuipromote kazi hiyo kwenye platform mbalimbali walizonazo kwani kusupport kazi za wasanii sio ombi la msanii bali ni jukumu lao.
Kuhusu kutokulipa wasanii fungu lao Soundcity TV wamekataa kabisa kitendo hiki na wamesisitiza kuwa kazi ya manager ni kupokea na kuthibitisha kuwa amepokea ile asilimia yake na ya msanii iliyotokana na wimbo wao kupigwa kwenye kituo hicho cha TV…
SOUND
>>>“Kazi yako kama manager ni kuhakikisha wasanii wako wanapata mafungu yao kutokana na kazi zao kuchezwa kwenye TV, ukifuatilia kupitia COSON, MSCN utagundua kuwa SOUNDCITY inawalipa wasanii mafungu yao kila mwaka… COSON ni Chama cha Haki Miliki Nigeria na MSCN ni Chama cha Haki Miliki na Muziki Nigeria, pengine ungeweza kujifunza zaidi kuhusu hivi vitu viwili kupita tovuti yao http://www.cosonng.com… <<< SOUNDCITY.

 

Share on Google Plus

About Unknown

TEAM TASABA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment