GOSSIP WITH TASABA

Maneno ya Diamond Platnumz baada ya kutajwa kuwania tuzo ya MTV Europe Music Awards 2015

.
.
Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz amepata nafasi ya kuipeperusha bendera ya Tanzania katika tuzo za MTV Europe Music Awards 2015 zitakazotolewa mwezi October 25, 2015 jijini Milani Italy.
Msanii huyo ambaye ametajwa kuwania tuzo ya MTV Europe Music Awards katika kipengele cha Best African Act, akiongea na ripota wa millardayo.com alisema..‘Kiukweli namshukuru sana mwenyezi Mungu kwasababu najua mimi naamini sio mimi tu watanzania wengi ndoto zenu ni kuomba muziki wetu uweze kutambulika kimataifa sio tu kutambulika bali kupewa heshima kwa taifa letu la Tanzania‘ – Diamond Platnumz
Kwasasa mambo yanaenda vizuri kabisa kwa hiyo kuteuliwa katika tuzo za MTV Europe kwangu ndio mara yangu ya kwanza pia hata kwa Tanzania, namshukuru Mwenyezi Mungu nauzuri tuzo hizo haziangalii chochote kwani zinaangalia kura za watu so naamini muda ukifika basi mashabiki tupige sana kura ili tuweze kufanikiwe kuuleta ushindi nyumbani, nakumbuka mwaka jana walishinda Sauti Sol‘ – Diamond Platnumz


Mo Music aliingia kwenye Muziki rasmi akiwa darasa la ngapi?, Baba yake kayajibu hapa

.
.
Najua nina watu wangu mnaotamani kufahamu historia ya wasanii pindi bado hawajajulikana katika tasnia ya sanaa ukiwa na amu ya kufahamu tabia au kitu alichokuwa analichokuwa anapenda msanii enzi za utoto wake.
Sasa basi ripota wa millardayo.com amekutana na Baba mzazi wa Mo Music Martin Katemi na kuzungumza naye kuhusu historia ya msanii Moshi aka Mo Music.
Mimi ni Martin Katemi baba mzazi wa Moshi nyie mnamfahamu kama Mo Music nina watoto wawili  wa kiume yeye ni wa pili,kijana wangu enzi za utoto alikuwa anapenda sana kukaa na makundi ya vijana wenzake na kuna muda alikuwa anakuja nao marafiki zake nyumbani’ – Martin Katemi
.
.
‘Makundi yake walikuwa ni watu wa kutengeneza vitu kama magari pia hata ufugaji wa Mbwa ni mpenzi sana wa Mbwa kuna wakati alikuwa anajibishana sana na marafiki zake kuhusu ufugaji wa Mbwa na alipofikia darasa la saba alikuwa na kundi la muziki ambapo walikuwa wakienda mlimani hapa ulipo ukiangalia juu kuna eneo la mlima unaitwa Mlima wa Papa’ – Matin Katemi
Kule walikuwa wanafanya uimbaji lakini sisi wazee tulifanya kazi kubwa sana ya kuchuguza ni kitu gani wanachokifanya kwani kule ni eneo ambalo huwa wanakaa wahuni wavuta bangi na watu wengine lakini tulivyokwenda tukawakutana wana ma guitar na vifaa vya muziki baadae ndipo tukaanza kuona matunda kutoka kwa Mo Music baada ya kutoka wimbo wake wa kwanza’ – Martin Katemi
Na nyumbani kwao Mo Music ndio kando kando ya huo Mlima na ndio maana alikuwa akienda huko kwenda kufanya mazoezi yake na marafiki zake’ – Martin Katemi

Maneno ya Kalapina kuhusu pingamizi alilolipata dhidi ya mgombea mwenza…

.
.
Tukiwa bado tuko kwenye headlines za uchaguzi 2015 time hii nakusogezea stori kutoka kwa msanii wa Hip Hop Kalapina ambaye ni mgombea wa Ubunge jimbo la Kinondoni Dar es Salaam.
Msanii huyo alikutana na ripota wa millardayo.com leo Sept 9, 2015 na kuzungumza kuhusu pingamzi alilolipata jimboni kwake dhidi ya mgombea mwenza kupitia chama cha Mapinduzi
‘Kiukweli niliwekewa pingamizi na mgombea wa CCM Issa Mohamed akidai kwamba sija dhaminiwa na chama change lakini nikawa nimetoa utetezi wa kutosheleza tu kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi Salim Hassan Msuya wilayani Kinondoni na msaidizi wake anaitwa Victor Muhenge’
‘Lakini kinachoonekana kwa mimi binafsi na hata mtazamo wa chama changu ningependa kusema hiki watanzania wote wajue kwamba pale kuna hujuma manispaa ya Kinondoni kwamba Iddi Hassan anaonekana anashirikiana na watendaji wa pale katika ku engineer hizi pingamizi za namna moja au nyingine’ – Kalapina
‘Kwasababu aliwekea pingamizi wagombea wengi lakini kikuweli  hazikuwa pingamizi zenye mashiko na naishukuru ningependa kuishukuru tume ya uchaguzi na mkurugenzi wa tume kwa kuweza kutupilia mbali pingamizi la mgombea wa CCM’- Kalapina

Wande Coal kaja na hii Video nyingine ‘Same Shit’ Feat. AKA

Staa wa Nigeria Wande Coal ameachia Video ya ngoma yake mpya ‘Same Shit’ ndani akiwa amemshirikisha rapper kutoka Afrika Kusini AKA.


 


 

 

 

 

 

Share on Google Plus

About Unknown

TEAM TASABA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment