Kifaa kipya toka FC Barcelona ndani ya jezi ya Chelsea
Habari nyingi kwa sasa katika michezo ni
kuhusiana na usajili wa wachezaji mbalimbali ndicho kitu kinacho weka
headlines kubwa katika vyombo vya habari, ilikuwa ni kuhusiana na Pedro Rodriguez kuhamia katika klabu ya Manchester United kabla ya dili hilo kubadilika.
Usiku wa August 19 zilianza kuandikwa tetesi kuwa Pedro atajiunga na klabu ya Chelsea na sio Man United kama ilivyoandikwa awali katika vyombo vya habari na kuwa walikubaliana bei, habari zimethibitika kwa Pedro kujiunga na Chelsea kwani alipewa ruhusu na FC Barcelona August 18 ili kwenda London kufanya vipimo vya afya na amesaini mkataba wa miaka minne Stamford Bridge.
Masaa 11 pekee yalitosha kuipiku Man United katika mbio za kusaka saini ya nyota huyo hivyo Pedro amethibitisha kuwa London kwa ajili ya vipimo vya afaya na anafuraha kujiunga na Chelsea… FC Barcelona na Chelsea wamekubaliana uhamisho wa euro milioni 30 ila kuna uwezekano wa kuongezwa euro milion 3 kulingana na kiwango atakacho onyesha Pedro. Pande zote mbili zimethibitisha uhamisho huo wa Pedro.
“Nafuraha
kuwa hapa na nina furaha kuanza kuitumikia Chelsea na nipo hapa
kuendeleza kutwaa mataji shukrani kwa klabu na mashabiki kwa kunipa
nafasi ya kuvaa jezi ya Chelsea “>>>Pedro
Hawa ndio wachezaji watoto chini ya Miaka 15 watakaojiunga na Orlando Pirates ya Afrika Kusini..
Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, Jamal Malinzi August 20 2015 ametangaza mpango wa kukuza soka la vijana na hii ni kama mrejesho wa mashindano yaliyofanyika Mwanza kwa timu za watoto, Malinzi ameeleza mpango huo wa kuwaandaa vijana ambao watashiriki michuano ya mataifa ya Afrika chini ya miaka 17 yatakayofanyika mwaka 2019, Tanzania itakuwa timu mwenyeji hivyo imefuzu moja kwa moja.
Hata hivyo Malinzi pia ametangaza kupatikana kwa wachezaji watano waliocheza michuano Mwanza na August 29 wataelekea Afrika ya Kusini kufanya majaribio katika Academy ya klabu ya Orlando Pirates inayomilikiwa na Irvin Khoza.
Majina ya wachezaji watano watakaoondoka kwenda kufanya majaribio katika klabu ya Orlando Pirates ni Assad Ally Juma kutoka Zanzibar, Maziku Amani na Issa Abdi kutoka Dodoma, Kelvin Deogratius kutoka Geita na Athumani Maulid kutoka Kigoma.
Sambamba na hayo Malinzi
pia amethibitisha kuendelea na mipango ya kuomba nchi mbalimbali
duniani ili kupata nafasi ya kuwapeleka wachezaji wa umri chini ya
miaka 15 kujiunga na Academy za huko ili kukuza soka la vijana hao na kupata wachezaji watakaounda kikosi imara kwa michuano ya Afrika 2019 Tanzania.
Hii ni list ya wachezaji 20 waliochaguliwa katika kikosi cha Wachezaji chini ya miaka 13 kutoka katika michuano iliyofanyika Mwanza.
Huyu ni staa mwingine kutoka Ghana aliyejiunga na Chelsea
Jose Mourinho ni miongoni mwa makocha wanaopenda wachezaji wenye asili ya Afrika August 19 2015 habari za kumsajili beki wa kimataifa wa Ghana aliyekuwa anaichezea klabu ya FC Augsburg ya Ujerumani Baba Rahman na kujiunga na klabu ya Chelsea kwa ada ya uhamisho ya pound milioni 21.7.
Beki huyo wa Ghana mwenye umri wa miaka 21 huenda atapangwa kucheza beki ya kushoto namba ambayo ilikuwa ikichezwa na beki wa kihispania Cesar Azpiliceuta ambaye baada ya ujio wa Baba, Stamford Bridge Cesar Azpiliceuta ataenda kucheza upande wa kulia.
Klabu ya Chelsea ambayo imefanikiwa kumnasa Baba bado haijakata tamaa ya kusaka saini ya beki wa kiingereza anayeichezea klabu ya Everton John Stones licha ya ofa ya pound milioni 30 kukataliwa hivyo inajiandaa kutuma ofa nyingine ya pound milioni 40 ndani ya masaa 48.
Hii ndio Ratiba rasmi ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara 2015 iliyotolewa na TFF…
August 19 Afisa mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi Boniface Wambura ametangaza ratiba rasmi ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara ambapo Ligi Kuu itaanza Septemba 12 2015 ambapo itakuwa ni wiki moja baada ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kucheza na timu ya taifa ya Nigeria mchezo wa kufuzu AFCON 2017.
Wambura
amethibitisha kupangwa kwa ratiba ya Ligi hiyo kwa kuzingatia mazingira
ya timu zinakotoka na sehemu zinakoenda ili kuvisaidia vilabu kupunguza
gharama za nauli, ratiba pia imepangwa kwa kuzingatia timu
zitakazoshiriki klabu Bingwa barani Afrika na kombe la shirikisho.
Hata hivyo Wambura alitangaza pia kuanza kwa kombe la FA
ambapo litashirikisha timu 64, timu 16 za Ligi Kuu, timu 24 za Ligi
daraja la kwanza na timu 24 za Ligi daraja la pili kwani ujio wa Kombe
la FA unakuja sambamba na neema ya kupatikana kwa mdhamini wa Kombe la FA.
Ratiba ya Kombe la FA
itatoka baada ya kutoka kwa ratiba za Ligi daraja la kwanza na Ligi
daraja la pili kwani timu shiriki zinategemea viwanja ambavyo pia
vitatumika katika michezo ya Ligi Kuu.
“Msimu wa
Ligi umeshafunguliwa kwa maana ya usajili ila kwa mashindano tutaanza
kucheza Septemba 12 na tutamaliza mzunguko wa kwanza Novemba 7 baada ya
hapo tutaingia katika usajili wa dirisha dogo kupisha michuano ya Challenge Cup na tutaendelea December 19 na tutaenda kumaliza Ligi Mei 7 2016″>>>Wambura
Hii ndio ratiba yote ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2015/16.
0 comments :
Post a Comment