Taarifa zimenifikia za Ajali ya Moto iliyouwa watu 9 Dar es Salaam… (picha)
Tangu mwaka 2015 umeanza tumesikia stori
kadhaa za Ajali ya moto ikiwemo ile ya familia yenye watu sita wakiwa
wamefariki ndani ya nyumbani chanzo kilisemakana ni itilafu ya Umeme,
sasa hapa nakusogezea stori nyingine ya kusikitisha ambapo usiku wa
kuamkia leo kumetokea ajali ya moto ilyouwa familia ya watu 9 wakiwa
ndani ya nyumba maeneo Buguruni Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Katibu wa mtaa Amina Kichalala….’Mimi
niliamshwa usiku na mume wangu akatuambia kwa jirani kuna moto ilikuwa n
majira ya saa tisa usiku mara tunasikia sauti zao wanasema tuwasaidie
moto ulikuwa ni mkubwa sana watu wakaanza kurusha mawe, wamejitahidi
lakini moto ukawa mkubwa mpaka mida ya saa kumi na moja kasoro ndio
zijaka fire kuuzima huo moto na kutoa miili ya watu tisa wakiwa
washamefariki katika ajali hiyo ya moto’ – Amina‘Sauti iliyosikika wakati tukio hilo la ajali ya moto ilikuwa ni ya msichana mdogo anaitwa Aisha yuko kama darasa la saba motto wa huyo Baba, katika hiyo nyumba alikuwa anaishi Mama Habilai, Mohamed, Ashlafu,Aisha na Bibi yao asiyejiweza kwasababu uwa wanamtoa kumpeleka hospitali na wageni kutoka Oman walioingia jana nao wamefariki’ – Amina
‘Majirani walifanya juhudi za kuuzima moto huo lakini hakuna kilichowezekana kwasababu moto ulikuwa ni mkubwa sana, uamuzi uliofuata ile miili 9 ya ndugu zetu imepelekwa muhimbili kuoshwa na kuzikwa katika makaburi ya Kisutu Dar es Salaam‘ -Amina
0 comments :
Post a Comment