SPORTS NEWS OF THE DAY WITH GREAT GOSSIP

Paul Kagame anarudi Madarakani mwaka 2017? Hii hapa kutoka Mahakamani Rwanda..

Mahakama Kuu Rwanda imepokea Shauri kutoka Vyama vya Upinzani Rwanda ambavyo vinahitaji Rais Paul Kagame asigombee Urais kwa awamu nyingine tena baada ya kumaliza awamu mbili za kuiongoza Nchi hiyo.
Jopo la Majaji nane litajadili ishu hiyo, japo Serikali iliweka pingamizi Mahakamani kwamba kisijadiliwe chochote lakini jopo hilo linaloongozwa na Jaji Immaculee Nyirinkwaya lilitupilia mbali pingamizi hilo na Shauri litaendelea kusikilizwa Mahakamani September 23 2015.
Rwanda's President Paul Kagame attends the opening ceremony of the 24th Ordinary session of the Assembly of Heads of State and Government of the African Union (AU) at the African Union headquarters in Ethiopia's capital Addis Ababa, January 30, 2015. REUTERS/Tiksa Negeri
Rais wa Rwanda, Paul Kagame
Rais Kagame hakuwahi kutamka kama atagombea awamu ya tatu ya Urais au hapana, lakini kila alipoulizwa amekuwa akijibu kwamba hayo ni maamuzi ya Watu wa Rwanda wenyewe kumruhusu aendelee au hapana.
Kumekuwa na mvutano wa muda mrefu kuhusu ishu ya Katiba ya Rwanda kufanyiwa mabadiliko ili kumruhusu Kagame agombee tena Urais kwenye Uchaguzi Mkuu 2017 lakini upande wa Upinzani wameonekana kutokubaliana kabisa na mapendekezo hayo.
gty_obama_ethiopia_presser_02_mm_150727_4x3_992
Rais Barack Obama alipokuwa Ethiopia July 2015.
Rais wa Marekani Barack Obama ni mmoja ya Viongozi ambao hawakubaliani na kitendo cha  Kiongozi yoyote kubadili Katiba ili aendelee kubaki Madarakani >>> ‘Nadhani mimi ni Rais bora kabisa, hata nikisema nigombee Urais wa Marekani kwa mara nyingine ninashinda… Hakuna mtu anatakiwa kuwa Rais milele, ni vizuri mkapeana nafasi na mwingine aje aongoze akiwa na mawazo mapya‘- Hii ni nukuu ya alichokisema Rais Obama akiwa kwenye ziara Ethiopia July 2015.

Uchafuzi wa Mazingira China sio kesi ndogo, hii ndio faini kwa waliokamatwa mwaka 2015…

Zipo nchi Duniani ambazo huwa hazipendezwi na aina ya hukumu ambazo zinatolewa na China hasa kwa watu waliokamatwa kwa makosa ya jinai kama ya ubadhirifu ama ishu ya kukamatwa na dawa za kulevya, lakini kwa upande mwingine hukumu za aina hiyo zimesaidia kuwatia hofu watu kujiingiza na kufanya makosa ya aina hiyo.
Dar es Salaam ni moja ya Majiji ambayo kiukweli hali ya usafi na utunzaji wa Mazingira sio ya kuridhisha kwenye maeneo mengi, lakini kuna Miji kama Moshi wameweza kujitahidi kutokana na adhabu kali ambayo imewekwa ikitokea umekamatwa kwa kosa la uchafuzi wa Mazingira, faini yake tu inaogopwa !!
0,,17687721_303,00
Ripoti kutoka China inaonesha kwa kipindi cha miezi saba ndani ya mwaka 2015, wamekusanya Yuan Milioni 28 zilizotokana na faini kwa kesi za Uchafuzi wa mazingira… Hizo ni zaidi ya Trilioni 9 kwa pesa ya Tanzania !!
Kilichofanyika ni kwamba January 2015 walifanya marekebisho ya Sheria ambapo kuanzia hapo Kiwanda au mtu yoyote akikamatwa kwa kosa linalohusu uchafuzi wa mazingira faini yake ni kubwa na hakuna kiwango cha mwisho ambacho mtu anatakiwa kulipia.
Pesa iliyokusanywa China kwa miezi saba tu ni karibia nusu ya Bajeti ya Tanzania 2015-16, ikitokea Dar au Tanzania kunakuwa na Sheria kali kiasi hicho unadhani tutamaliza tatizo la uchafu mtu wangu??

Jeshi la Nigeria limewakamata hawa wengine waliojihusisha na Boko Haram!

Headlines za Boko Haram zinaendelea kusikika, ni kama vile wanapumzika kidogo alafu wanaibuka tena… Mpya kutoka Nigeria leo inawahusu baadhi ya watu waliokamatwa na Jeshi la Nigeria kwa mashtaka ya kuwa wao ndio waliokuwa wanahusika kupeleka mafuta ya petroli na bangi kwenye maficho ya Boko Haram.
supplier1
Baadhi ya watu waliokamatwa wakijihusisha na vitendo vya kigaidi na Boko Haram.
Mkurugenzi wa Jeshi Mahusiano ya Umma Nigeria, Sani Usman alitoa kauli hiyo kupitia mtandao uitwao Prompt News Online, na kusema…
>>> ” Waalifu hawa ndio waliokuwa wakijihusisha na biashara ya kupeleka mafuta ya petroli, bangi na vilevi vingine … Jeshi la Nigeria litaendelea kupambana kadri liwezavyo dhidi ya vitendo vya kigaidi kwenye nchi hii ili kuhakikisha Nigeria inabaki salama na yenye amani… Lakini hivi vyote vitakuwa vigumu kutimiza kama hatutakuwa na ushirikiano kutoka kwa umma, tunakaribisha taarifa yoyote ile dhidi ya matukio au mipango ya Boko Haram inayoendelea kwenye jamii “. <<<  Sani Usman.
Supplier-2
Baadhi ya vitu vilivyokamatwa kwenye camp ya Boko Haram.
Mkurugenzi wa Jeshi Mahusiano ya Umma, Sani Usman amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watu hao waliokamatwa ambao kwa muda mrefu wamekuwa kikwazo cha amani sehemu mbalimbali nchini Nigeria kwa kujihusisha na Boko Haram.

Cristiano Ronaldo kaja na biashara ya perfume time hii… Pichaz na Video za uzinduzi hizi hapa..

Michezo

Cristiano Ronaldo kaja na biashara ya perfume time hii… Pichaz na Video za uzinduzi hizi hapa..

on
Cristiano Ronaldo ni staa mkubwa kwenye soka, YES… Dunia inamjua, hii ni kumaanisha kwamba hata wasio na ushabiki kwenye soka jina lake wanalijua !!
1900832
Mastaa kama Michael Jordan wamestaafu kwenye Michezo lakini majina yao yako juu bado kutokana na kujiingiza pia kwenye biashara kubwakubwa Duniani… Ronaldo anahitaji hata ikitokea leo anaachana na soka, jina lake likumbukwe pia tena kwenye uzito wake !!
Ni dili juu ya dili kwa Cristiano Ronaldo… baada ya kuingia Mikataba mingi ikiwemo ya kutengeneza nguo na viatu vyenye jina lake, safari hii amezindua perfume zenye jina la ‘Legacy‘ na tayari zimesogezwa sokoni kuuzwa.
Hapa nimekuwekea Pichaz na Video, Ronaldo na watu wake wa karibu wakati wa uzinduzi huo…
ron
ron2
ron3
ron4
ron6

 


 



 


 

Share on Google Plus

About Unknown

TEAM TASABA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment