Movie sita kali kabisa zilizowakutanisha mastaa na watoto wao kwa pamoja… (+Pichaz)

Kwa mtu ambae anafatilia sana movie majina ya mastaa kama Angelina JolieWill Smithau Bruce Willis sio mageni kwao… hao wote ni mastaa wanaofanya poa wakiiwakilisha industry ya Holywood Marekani.
Nimepata kitu kingine kilichonivutia mtu wangu, unajua ni rahisi kumuona mtoto wa staa wa movie kwenye Movie za Bongo, tena urahisi wenyewe ni kwamba staa mwenyewe anaweza kumshika mkono mwanae akaenda nae location na mtoto nae akawa na scene yake ya kucheza.
Marekani mambo sio rahisi kiasi hicho, unaambiwa kama una mkataba na Will Smith basi ni wewe na Mr. Smith mwenyewe, masuala ya kumuingiza mtoto wake kwenye movie hiyo ni biashara nyingine kabisa.. yani mtoto nae lazima awe na mkataba wenye malipo yake kabisa, baada ya kukamilika kila kitu mambo mengine yanaendelea.
Kuna movie nyingi kumbe mastaa wako na watoto wao aisee, utaratibu ni huohuo wa Mikataba… nimeipata stori ya baadhi ya mastaa ambao wamewahi kucheza Movie pamoja na watoto wao Marekani mtu wa nguvu.
31f2e843a990518ef8a41268355075f0d64c5d0a
Angelina Jolie na Vivienne Jolie Pitt… Hapo ni mama na mtoto wake mtu wangu, wote wawili kwenye movie ya ‘Maleficent’ iliyotoka mwaka 2014.
56d15850831a3572acc721f2668f722769fa4976
Will Smith na mwanae wa kiume, Jaden Smith.. Wao wameonekana pamoja kwenye movie mbili, ya kwanza ni ‘Pursuit of Happyness’ iliyotoka mwaka 2006 na nyingine ni ‘After Earth’ iliyotoka mwaka 2013.. zote ni movie kali sana mtu wangu, baba na mwana wamefit poa kabisa mwanzo mwisho !!
c8be336cfdbf4a8b8d424452b6ab0f72709423a3
Yes yes, bado niko na Familia ya Will Smith mtu wa nguvu.. Hapo ni mama na mwana, Jada Pinkett Smith na mtoto wake Jaden Smith sauti zao zimetumika kwenye movie ya wanyama ambayo ni animation ya ‘Madagascar: Escape 2 Africa‘ iliyotengenezwa mwaka 2008.
9841baf500ae8fcf49a41888d53064b9f52db3de
Billy Ray na Miley Cyrus ni mtu na baba yake, Miley ni kama nguvu nyingi zaidi anaiweka kwenye muziki na kwenye masuala ya movie sio sana… Hawa nao wamecheza pamoja kwenye series ya ‘Hannah Montana’.
jon-voight-angelina-jolie
Angelina Jollie na baba yake, Jon Voight wamecheza pamoja kwenye movie ya Lara Croft: Tomb Raider‘ ambayo ilitoka mwaka 2001. MzeeJon Voight ni staa mkubwa sana kwenye movie, aliwahi pia kucheza movie ya Anaconda na akina Ice Cube pamoja na Jennifer Lopez.
Rumer-Willis-Bruce-Willis-G-Joe-Retaliation-z4SmSQ9EZ-xl
Rumer Willis na baba yake Bruce Willis waliwahi pia kushiriki pamoja kwenye movie ya ‘The Whole Nine Yards’ ya mwaka 2000 na pia ikafuatia ‘Hostage’ ambayo ilitoka mwaka 2005, wote wawili ndani.
Share on Google Plus

About Unknown

TEAM TASABA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment