HABARI NOW

RAIS KIKWETE APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA MABALOZI WA USWISI NA UTURUKI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Saluti na wimbo wa Taifa kwa Balozi mpya wa Uswisi nchini Bi. Florence Tinguely Mattli, alipofika kuwasilisha hati zake za Utambulisho kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2015
 Balozi mpya wa Uswisi nchini Bi. Florence Tinguely Mattli, akisaini kitabu cha wageni alipofika kuwasilisha hati zake za Utambulisho kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2015
 Balozi mpya wa Uswisi nchini Bi. Florence Tinguely Mattli akiwasilisha  hati zake za Utambulisho kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2015.
  Balozi mpya wa Uswisi nchini Bi. Florence Tinguely Mattli, akiongea na Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipofika kuwasilisha hati zake za Utambulisho kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2015.
 Balozi mpya wa Uturuki nchini Bi. Yasemin Eralp akisanini kitabu cha wageni alipofika kuwasilisha hati zake za Utambulisho kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2015
 Balozi mpya wa  Uturuki nchini Bi. Yasemin Eralp akiwasilisha  hati zake za Utambulisho kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2015
 Balozi mpya wa  Uturuki nchini Bi. Yasemin Eralp na ujumbe wake akizungumza na Rais Kikwete baada ya kuwasilisha  hati zake za Utambulisho kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI UKANDA WA ZIWA TANGANYIKA, MJINI KIGOMA LEO.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja ya jiwe lenye Madini huku akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Aifola Investiment Co. Ltd, Zubery Mabie, kuhusu upatikanaji wa madini na utengenezaji wa Unga wa 'Lime Powder', wakati Makamu alipokuwa akitembelea Mabanda ya maonesho kwenye ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji wa Ziwa Tanganyika, lililofanyika leo Sept 9, 2015 kwenye Hoteli ya Tanganyika Mjini Kigoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wauza Samaki wa Mapambo, Nunu Mrisho, kuhusu upatikanaji wa Samaki hao na soko lake , wakati Makamu alipokuwa akitembelea Mabanda ya maonesho kwenye ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji wa Ziwa Tanganyika, lililofanyika leo Sept 9, 2015 kwenye Hoteli ya Tanganyika Mjini Kigoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Uwekezaji wa Ziwa Tanganyika, lililofanyika leo Sept 9, 2015 kwenye Hoteli ya Tanganyika Mjini Kigoma.
 Sehemu ya washiriki wa Kongamano hilo wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, alipokuwa akihutubia kwenye ufunguzi wa Kongamano hilo.
 Mwakilishi wa Umoja wa wafanyabishara wa Burundi, akizungumza.
 Waziri wa Nchi- Uwekezaji na Uwezeshaji, Eng. Christopher Chiza, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Makamu wa Rais Dkt. Bilal ili kufungua Kongamano hilo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na Balozi waliohudhuria Kongamano hilo baada ya ufunguzi, uliofanyika leo Sept 9, 2015.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na Makatibu Wakuu waliohudhuria Kongamano hilo baada ya ufunguzi, uliofanyika leo Sept 9, 2015.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na Viongozi wa Halmashauri wa Wilaya za Mkoa wa Kigoma waliohudhuria Kongamano hilo baada ya ufunguzi, uliofanyika leo Sept 9, 2015.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Kigoma waliohudhuria Kongamano hilo baada ya ufunguzi, uliofanyika leo Sept 9, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo waliohudhuria Kongamano hilo baada ya ufunguzi, uliofanyika leo Sept 9, 2015. Picha na OMR



HOTUBA YA MHE.
DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL, MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA UFUNGUZI WA KONGAMANO
LA UWEKEZAJI UKANDA WA ZIWA TANGANYIKA TAREHE 09 SEPTEMBA 2015
 
Mhe.  Mizengo Kayanza Peter Pinda
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mhe. Eng. Cristopher Chiza
Waziri wa Nchi - Uwekezaji na Uwezeshaji;
Waheshimiwa Mawaziri;
Wakuu wa Mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma;
Waheshimiwa Mabalozi;
Washiriki;
Wageni Waalikwa;
Waandishi wa Habari;
Mabibi na Mabwana;
Awali ya yote napenda kushukuru kupata fursa ya kushiriki nanyi kwenye Kongamano hili, linaloangazia fursa za uwekezaji na utanuaji maendeleo kwa ukanda huu wa Ziwa Tanganyika. Nimefurahi kuwa nanyi hapa Kigoma na nafarijika zaidi kuona namna mlivyojitokeza katika kongamano hili ukilinganisha na lile lililofanyika mwaka jana mjini Sumbawanga ambapo pia nilipata fursa ya kuhudhuria.
Pili, napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wenyeji wetu kwa mapokezi mazuri. Nimefurahishwa na maandalizi mazuri ya Kongamano hili kwenye mazingira mazuri ambayo yanaonesha umakini katika uandaaji. Nadhani washiriki wote mtakubaliana nami kwenye hili. Asanteni sana.
Ninawashukuru pia Mabalozi kutoka nchi mbalimbali walioshiriki. Hali kadhalika nawashukuru wageni wetu kutoka nchi za nje kama vile Marekani, Jumuiya ya Ulaya na Burundi.  Na washiriki wengine kutoka taasisi na sehemu mbalimbali kwa kushiriki Kongamano letu, hii inadhihirisha umuhimu wa shughuli yenyewe na inatuhakikishia mafanikio chanya siku zijazo.
Tatu, napenda kuwashukuru Wananchi wa Kigoma na hasa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma  Lt. Col. (Mst.) Issa S. Machibya  kwa ukarimu wao na kukubali kutupokea kwenye Kongamano hili. Ni ukweli ulio dhahiri kwamba Kongamano hili kufanyika katika mkoa wenu ni mafanikio makubwa ya kuutangaza mji wenu Kigoma/Ujiji.
Waheshimiwa,
Mabibi na Mabwana;
Katika msafara wangu nimefuatana na Maafisa kadhaa Waandamizi wa Serikali ambao wako hapa kusikiliza, kuzungumza na kuchangia hoja mbali mbali kwenye sekta ya Uwekezaji na Mazingira ya Biashara katika Ukanda huu wa Ziwa Tanganyika. Ninawaomba washiriki wote kuitumia fursa hiyo ya kupata habari muhimu wakiwa hapa ili kufanikisha malengo yenu ya Uwekezaji katika Ukanda huu.
Ninaelewa baadaye mtapata fursa ya kufanya mazungumzo ya mtu mmoja mmoja na wenzenu kutoka Ukanda huu. Mtapata maelezo ya kutosha kuhusu fursa za Uwekezaji nchini na maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uendelezaji Maeneo Maalum ya Kiuchumi (EPZA) kuhusu fursa na mazingira ya biashara katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika. Hali hiyo itaifanya kazi yangu iwe rahisi. Nachukua fursa hii kuwaeleza kwa kifupi kwa nini Ukanda huu ni eneo muhimu la kimkakati kwa uwekezaji nchini.
Waheshimiwa,
Mabibi na Mabwana;
Ukanda wa Ziwa Tanganyika unajumuisha mikoa mitatu (Rukwa, Kigoma na Katavi), sina shaka ukanda huu ni mahali muafaka pa kuwekeza katika nchi yetu. Ukanda huu ulikuwa nyuma kimaendeleo kwa miaka mingi na ukombali na Makao makuu ya nchi Dodoma na hata kutoka kwenye mji mkuu wa kibiashara wa Dar es Salaam.
 
Miundombinu ya usafiri wa Barabara, Reli, Maji na Anga ulikuwa hafifu hali ambayo iliathiri kwa kiasi kikubwa maendelo ya ukanda huu. Lakini kwa sasa Serikali imewekeza kwa kiwango kikubwa kwenye Barabara, Viwanja vya ndege, Bandari na Reli, hivyo kuufanya Ukanda huu ufunguke.
Uboreshaji wa miundombinu ya barabara kwa kiwango cha lami unaendelea, ujenzi wa barabara ya  Tunduma hadi Sumbawanga, kutoka Sumbawanga hadi Kasanga kupitia Matai, kutoka Sumbawanga hadi Tabora kupitia Namanyere na Mpanda, pia barabara ya Mpanda hadi Tabora kupitia Koga, kutoka daraja la Mto Malagarasi hadi Tabora kupitia Kaliua na Urambo, kutoka Mpanda kupitia Uvinza hadi Kanyani, Wilaya ya Kasulu. Barabara kutoka Kigoma hadi mpaka wa Burundi na kutoka Kigoma kupitia Kidahwe hadi Uvinza.
Ukamilikaji wa barabara hizo unaufanya ukanda huu ufunguke na kuwezesha kufikika kwa urahisi kutoka kwenye miji mikubwa ya Mbeya, Dar es salaam na Dodoma, na pia kwa nchi jirani za  Afrika ya Kati na Kusini kama vile Malawi, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Msumbiji, Rwanda, Burundi na Afrika ya Kusini. Hali ya maji kwa sasa inaridhisha, umeme upo wa kutosha kwa matumizi ya nyumbani hata hivyo kuna juhudi mbalimbali kuuongeza ukidhi kwenye shughuli za viwanda. Sehemu za Mkoa wa Rukwa zimeunganishwa na Shirika la Umeme la Zambia “Zambian Electricity Supply Company (ZESCO)”. Kwa upande wa Kigoma na Katavi bado wanatumia umeme wa jenereta hata hivyo kuna juhudi za ujenzi wa umeme wa jua katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji na kuunganisha na umeme wa gridi ya Taifa kutokea Tabora.
Waheshimiwa,
Mabibi na Mabwana;
Ninaweza kuendelea tena na tena kuelezea fursa na hatua zilizochukuliwa na Serikali. Lakini ni vyema kusema tu kuwa kwa sasa mazingira ya biashara yameboreshwa sana na yameanza kuvutia wawekezaji wengi kiasi kwamba shughuli za uwekezaji zimeongezeka kwenye sekta za Kilimo, Madini na Umeme katika kipindi cha miaka mine iliyopita. 
Kuna wawekezaji ambao wanasema kuwa ukanda huu ni eneo ambalo wawekezaji wanaliangalia kwa jicho la kimkakati kwa sasa. Hii inatokana na ukweli kuwa madini mengi yanapatikana katika Ukanda huu kama vile Dhahabu, Nickel, Makaa ya Mawe, Chokaa, Shaba na Madini ya Vito. Hivyo mtu anaweza kuchagua eneo lo lote analopenda katika ukanda huu ambao una watu wapatao 3,697,073 kutokana na sensa ya mwaka 2012. Kulingana na takwimu za Shirika la Takwimu za mwaka 2013 pato la mkaaji wa ukanda huu anapata wastani wa Tshs. 910,963 kwa mwaka.
Uanzishwaji wa Eneo Maalum la Kiuchumi Kigoma (Kigoma Special Economic Zone “KiSEZ”) ni hatua nyingine ya Serikali kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji katika viwanda, biashara na huduma za kiuchumi katika “kuunganisha fursa zilizopo na masoko ya ndani na nje ya nchi”. Hali hiyo imelenga katika kuufanya mji wa Kigoma/Ujiji kuwa kituo kikuu cha biashara katika eneo la Maziwa Makuu. Kuwekeza kwenye eneo hili kunamfanya mwekezaji kupata faida ya kiushindani  katika shughuli za viwanda na biashara kwenye eneo lote la Maziwa Makuu.
Waheshimiwa;
Mabibi na Mabwana;
Kwa sasa napenda kuwakaribisha nyote na biashara zenu kuwekeza katika Ukanda huu wa Ziwa Tanganyika. Kuna fursa nyingi ambazo watoa mada watabainisha na mtapata fursa ya kuwasiliana mmoja mmoja na kila Mkoa au kila Halmashauri au kila Mfanyabiashara.
Ukanda unategemea zaidi kilimo na zaidi mazao ya chakula kama vile mpunga, ndizi, mahindi, viazi, maharage, na karanga ambapo mazao ya biashara ni kahawa, tumbaku, alizeti, mawese. Mazao hayo ndiyo yanaendesha maisha ya watu wa ukanda huu shughuli zingine ni uvuvi na biashara. Hata hivyo kilimo ni cha hali ya chini sambamba na uvuvi. Ninawaalika kuwekeza kwenye eneo hilo kuboresha sekta ya kilimo ambayo inaajiri watu wengi. Ukanda huu umejaliwa mito na maziwa yenye maji baridi na safi, hivyo umwagiliaji unaweza kufanyika kwa ufanisi mkubwa.
Nimesikia kuna baadhi yenu mnataka kuwekeza kwenye nishati, ninawakaribisha. Kama nilivyosema hapo awali Ukanda huu unahitaji umeme mwingi zaidi ili kuweza kuimarisha sekta ya viwanda hasa viwanda vya usindikaji wa mazao ya kilimo na uvuvi.
Waheshimiwa;
Mabibi na Mabwana;
Ninafahamu kuwa baadhi yenu mnataka kuwekeza kwenye utalii. Ukanda huu bado haujapiga hatua nzuri kwenye sekta ya utalii, hivyo ni fursa nzuri kwa sasa kuwekeza kwani hili ni eneo lililojaliwa aina mbali mbali ya wanyamapori wanaopatikana kwenye mbuga na maeneo mengine ya hifadhi kama vile Hifadhi za Taifa za Mahale, Gombe na Katavi au pori la Moyowosi na Ugalla. Katika mbuga hizo kuna wanyama kama vile tembo, twiga, mamba, nyati, kiboko na sokwe mtu. Aidha, kuna ndege na mimea ya aina yake. Wawekezaji wanaweza kuwekeza kwenye hoteli na  huduma mbali mbali za kitalii.
Kama nilivyosema awali, eneo la viwanda ni muhimu kuangaliwa kwa mapana yake, ukanda huu una maliasili nyingi kama vile madini na mazao mbali mbali. Hali hiyo inaufanya Ukanda uwe na mali ghafi ya kusaidia kuanzishwa kwa viwanda vya uchakataji wa mazao mbali mbali kama vile mazao ya alizeti, mchikichi, mahindi, mpunga, mazao ya mifugo na madini.  
Waheshimiwa;
Mabibi na Mabwana;
Tanzania kwa sasa inatoa huduma bora za kiushindani kupitia sheria mbali mbali kama vile sheria ya Uwekezaji ya mwaka 1997, sheria ya Maeneo Uchakataji kwa ajili ya kuuza nje ya mwaka 2002, sheria ya Maeneo Maalum ya Kiuchumi ya mwaka 2006, sheria ya Madini ya mwaka 1998 na sheria ya mafuta ya Nishati ya mwaka 1981.
Serikali imejikita katika kutekeleza Mpango wa Kuboresha na Kuimarisha Mazingira ya Biashara (Business Environment Strengthening for Tanzania “BEST”). Lengo kubwa la mradi huo ambao ulianza Desemba, 2003, ni kupunguza urasimu wa Serikali na kuboresha huduma kwa sekta binafsi ikiwemo na mashauri ya kibiashara.
Tanzania ni nchi inayotoa motisha nzuri kwa wawekezaji. Pengine ni moja ya nchi zinazotoa motisha bora kuliko nchi nyingi katika Afrika. Nina imani kuwa Wakurugenzi wa Maeneo Maalum ya Kiuchumi (EPZA) na Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Nchini watakuwa wako hapa pamoja nasi. Nina hakika watazungumza kwa kina kwenye mawasilisho yao kuhusu jambo hilo.
Ni dhahiri kuwa, Ukanda wa Ziwa Tanganyika ndiyo lango kwa nchi nne zinazopakana na Ukanda huo. Ukanda huu unatoa njia fupi ambayo ni ya asili kwa nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi, na Zambia. Hivyo kuwekeza katika Ukanda huu unatoa fursa ya kuyafikia masoko ya nchi hizo kwa urahisi zaidi.
Waheshimiwa;
Mabibi na Mabwana;
Nimezungumza kwa kirefu kuliko nilivyotarajia. Naomba nihitimishe kwa kusema yafuatayo. Kwanza, Ukanda wa Ziwa Tanganyika uko tayari kufanya biashara nanyi. Pili, katika ukanda huu kuna kila kitu kinachohitajika katika uwekezaji: mazingira mazuri ya biashara, hali ya amani na utulivu, serikali inayojali wawekezaji, mali asili, wafanyakazi wanaojituma, soko la kutosha, hali nzauri ya kijiografia na kadhalika.
Lakini, kitu cha muhimu, kuwepo kwangu na kuwepo kwa Waziri Mkuu na Serikali yote kwa ujumla ni kuwahakikishia kuwa tuko makini na tumejipanga kikamilifu kufanya biashara nanyi. Serikali hii ni ya kuwawezesha wadau na imedhamiria katika  “kuunganisha fursa zilizopo na masoko ya ndani na nje ya nchi” kama kauli mbiyu ya kongamano inavyosema.
Ninaimani kuwa hakuna sababu ya kusita kuwekeza na kufanya biashara katika Ukanda huu wa Ziwa Tanganyika.
Ninawashukuru sana na ninawatakia mafanikio katika mazungumzo yenu. Karibuni sana Ukanda wa Ziwa Tanganyika.
ASANTENI KWA KUNISIKILIZA
 

A DECADE LONG OF BLOGGING: 6 IMPORTANT LESSONS FROM MICHUZI BLOG

By Mdau wa globu ya jamii
Every niche has a name. And when it comes to blogging in Tanzania you cannot miss the name of Muhidin Issa Michuzi. His blog, dubbed as Globu ya Jamii (societal blog) , with a slogan “The most read swahili blog on earth”, is unquestionably one of the most informative and most authoritative Swahili blog on earth. I know he has come a long way to deserve all this, and he is still going strong.
With Collins Mtita, author of this note, in Paris
It was on the 8th September of 2005 when Michuzi wrote his first post (see below) for what would become one of the most famous Swahili blogs. Today this very platform marks the first day into another decade. Many have come and many have gone, a few have persistently stood the test of time, and he is one of them.
It is rather uncustomary to find such articles on Michuzi Blog, (taking into slide his rather down-to-earth attitude) but this being a mark to celebrating  his decade long blogging career; I thought he deserves a  pat on the shoulder. And I dare take this opportunity to do just that. 
I know strong people never get this all the time, but once in a while it does more good than harm.
Michuzi was certainly a household name before blogging. He was, and still is, one of the most prominent photojournalists in Tanzania, since way long back in the days when print media ruled. When blogging started, Michuzi found an opportunity to express his burning passion in a more tangible way to reaching more people. The rest is history.
I am aware that he was not the first (but he was the pioneering blogger in Tanzania as then all Tanzanian bloggers were in the Diaspora), but he has made blogging famous. He is not the only one, but he has created a career for many to follow through. He may not be the last, but his name will be engraved in the minds of those who think of blogging as an opportunity to express oneself, as a source of income and a channel to let others shine as well.
If I had to sum up the last decade, here are a few things that I have managed to learn from Michuzi though his long and amusing career of blogging.

1. Love what you do
Falling in love with that you do is perhaps one of the most precious thing I have learnt though my constant encounters with Michuzi. Through chats with him I could easily tell that he does not stress for what he does, simply because he is having fun doing it. When you love what you do, that love becomes expressed in what you do. People can see and they will get to love it too.
At Finlandia hall in Helsinki, Finland
Loving what you do is doing it every day. Loving what you do is doing it with the best of your abilities. Loving what you do is to think about it almost all the time. And Michuzi cannot be overstated in this, because he still loves what he does.
2. Timely provide what people want with standards
Blogging is a hard work, but it rewards handsomely. This can be well understood by those in this niche. What is even harder is to provide what people want while maintaining standards.
When Michuzi started blogging, there was hardly any media outlet that entertained the idea of instantly publishing news or events within a short period of time of it breaking, not even Television. Michuzi saw this opportunity and seized it. In effect, he helped shape news reporting in Tanzania by proving almost real-time updates on main events – on politics, sports, entertainment, and lifestyle. With time, this habit built trust among daily visitors and they became permanent audiences.
It goes without saying that this blog has been so resourceful to the people in the Diaspora. A few years back when social media was  still in its infancy, and not so many people blogging, Michuzi blog was the only way to get updates from Tanzania, and that still continues today.
3. Be simple
Simplicity is the key to brilliance, a simple quote in itself with such a powerful meaning. Simplicity is the power to attract audience and it can never be explained any easier.
Success comes when you think beyond today and trivial challenges. Think at a very higher level, make big decisions but act simple so that more people understand you. That is the recipe for success.
4. Do not be predictable
Predictability is a weakness. If people can tell what you will do next, then you are in the wrong path. The best way is to become so unpredictable that people will keep coming back for more. For so long Michuzi blog has been a homepages for many. These people understood that within a very small span of time there will be something new on Michuzi blog, but they could hardly tell, hence they kept coming back for more hot updates from all walks of life.
5. Become a trendsetter
With Fidelis Tungaraza in Helsinki
The leader is visionary and never distracted by petty issues. He is more focused on solving perennial issues and create path for others to follow. Trendsetting is not easy if you are not focused or do not know what you want, but it is left for a few who have the courage to follow through their ideas even if none believes in them yet.
6. Never give up, enjoy the journey
I once asked Michuzi on how he finds blogging after being in the niche for nearly a decade, his reply was “The journey through blogging has not been easy, but for me it was more fun. I have faced my a share of obstacles on the way, but the best thing about challenges whenever you have fun is that they have a tendency to propelling  you forward. I can say it is magic in disguise.
As we celebrate 10 years of Michuzi blog, I sincerely wish Michuzi Media Group a lot more success and more wonderful opportunities ahead. May you reach and touch more people as they go through their own battles through life. You are inspiration to many.
Thanks a lot Ankal  Muhidin Issa Michuzi. You have been a force to reckon with and an inspiration to me, and hopefully many more.
Wako,

Mdau wa globu ya jamii, Diaspora

PS: Nashukuru sana mdau wa Diaspora ambaye si mwingine ila huyo hapo juu, Collins Mtita, ambaye ndiye webmaster wangu. Picha inayofuata ni mimi nikiwa Finlandia Hall mwaka huu, miaka 10 baada ya kuanzisha Michuzi Blog mahali hapo Septemba 8, 2005. Fidelis Tunaraza ambaye niko naye katika picha ya mwisho ndiye aliyenishawishi kuanza ku-blog. Picha ya mwisho (ambayo ndito ya kwanza kuweka katika Michuzi Blog) niko na Ndesanjo Macha aliyenifungulia blog na namna ya kuiendesha siku ya kwanza kabisa) . Hawa watu watatu ni muhimu mno katika maisha yangu ya blogging. Nilipanga kufanya sherehe kubwa kuadhimisha siku hii adhimu lakini nikaona haitonoga sana kwa kuwa kuna mambo ya kampeni kila kona. Sherehe nitaifanya mwezi Desemba mwaka huu.




TOTAL TANZANIA YADHAMINI MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI KWA SHULE 10 ZA MSINGI JIJINI DAR

 Askali wa usalama barabarani akitoa mafunzo kwa wanafunzi wa shule ya za msingi jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa navyeti walivyo tunukiwa mara baada ya kupata mafunzo ya usalama barabarani jijini Dar es Salaam.
 

Na Tom Bishop.
KAMPUNI  ya Mafuta ya Tatal  Tanzania imedhamini mafunzo ya usalama barabarani kwa shule za msingi 10 jijini Dar es Salaam.
 
Udhamini wa mafunzo hayo yamegharimu kiasi cha Dola za Kimarekani 20,000 kupeleka kwenye mradi wake wa elimu ya usalama barabarani.
Tatal   imekuwa ikidhamini mafunzo ya Usalama barabarani kila mwaka  kutokana na  kutenga  bajeti hiyo kwa ajili ya mafunzo hayo.
 
Utengaji huo wanatumia Boksi la Usalama barabrani ambao ni mradi wa  kuendelea kwa kipindi cha miaka 10 na utakuwa ukitolewa nchi nzima, kwa maeneo yenye kiwango kikubwa cha hatari za ajali kwa wanafunzi.
 
Mpaka sasa zaidi ya wanafunzi 150,000 wamefundishwa juu ya usalama barabarani katika jiji la Dar es Salaam, Kibaha na Bagamoyo.
 
 Boksi la usalama barabarani lina alama za barabarani, maelekezo ya elimu ya usalama barabarani kwa mwanafunzi, maelekezo ya usalama barabarani kwa mwalimu, mfano wa barabara yenye alama na vifaa vingine kama viakisi mwanga, vyeti pamoja na kalamu.
 
Katika mradi huo, mwaka huu Total Tanzania imefanikiwa kuzifikia shule za msingi  10 jijini Dar es Salaam.
 
Shule zilizopata mafunzo hayo ni    Shule ya Msingi Kawe A,Shule ya Msingi Tumaini,Shule ya Msingi Hananasif,Shule ya Msingi Mkunguni, Shule ya Msingi Mwongozo, Shule ya Msingi Yombo Dovya, Shule ya Msingi Jitihada, Shule ya Msingi Mivinjeni , Shule ya Msingi Mzambarauni pamoja na Shule ya Msingi Amani.
Share on Google Plus

About Unknown

TEAM TASABA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment