Maneno ya Waziri wa Fedha kuhusu fedha zilizotumika kuboresha Miundombinu
Agosti 25 ni siku ambayo Waziri wa Fedha
Saada Mkuya Salum alizindua bodi ya PPF na mafao mapya ya mfuko
huo.Katika mazungumzo ya Waziri huyo pia alitoa ufanunuzi kuhusiana na
fedha za mfuko wa jamii zilizotumika katika kuboresha miundombinu.
‘Na mimi kama msimamizi wa wizara ya
fedha nina wajibu wa kujitolea maelezo kuhusiana na madeni ya mifuko ya
hifadhi ya jamii, sisi Serikali ama hazina pale tumeunda kikosi kazi
kwanza tuseme hatukuweza kulipa haya madeni kwasababu tulikuwa
tumekwenda katika utaratibu wa kiserikali ni lazima maamuzi ya jinsi
gani madeni haya yatalipwa katika baraza la Mawaziri’ – Saada Mkuya
Mratibu wa Kanda za Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mbaruku akielezea namna fao hilo lilivyozingatia Mwanachama na Mwenza wake.
‘Kwa hiyo tulikuwa katika process lazima
waraka uandaliwe na unaandaliwa katika ngazi ya chini kabisa lakini
baada ya kufanyiwa marekebisho kwasababu inakwenda inaangaliwa inapewa
comment, inafanyiwa marekebisho baada ya hapo imekwenda katika kikao cha
makatibu wakuu baada ya kutolewa ufafanuzi baadhi ya maswali ama
kuboreshwa zaidi waraka ule ukawasilishwa katika Baraza la Mawaziri’ – Saada Mkuya
‘Na kweli siku ambayo tulikuwa tumekaa katika baraza la Mawaziri mada ilikuwa ni hiyo moja tu ni lazima tuangalie ishu ya ulipaji wa mfuko ya pension napenda kuwahakikishia kwamba tumetoka na jawabu na muongozo mzuri na tulikuwa na timu ambayo inaangalia jinsi gani tunaweza tukatoa bond‘ -Saada Mkuya
Waziri
Saada Mkuya akimpongeza Mwanachama wa PPF, Sara Jonas Haule, baada ya
kumkabidhi shilingi milioni moja ikiwa ni malipo ya fao la uzazi.
Wizara ya Afya imetoa Idadi kamili na maeneo wanayotoka waathirika wa ugonjwa wa kipindupindu
NI Ugonjwa ambayo umechukua headline sana kwa mwaka huu, sasa leo Mh. Dr.Seif Selemani Rashid kutoka wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii aliitisha mkutano wa waandishi wa habari kuzungumzia idadi na maeneo wanayotoka waathirika wa ugonjwa wa Kipindupindu.
Kwa mujibu wa Waziri huyo alisema..‘Ndugu ya Wananchi Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu hali ya ugonjwa Kipindupindu ambao umejitokeza katika mkoa wa Dar es Salaam na Morogoro, ugonjwa wa kipindupindu kwa mkoa wa Dar es Salaam ulianza katika manispaa ya Kinondoni kuanzia tarehe 15 mwezi wa nane mwaka huu, na hadi sasa Manispaa tatu zimeathirika kwa ugonjwa huu’ – Dr Seif
‘Aidha kwa Mkoa wa Morogoro ugonjwa ulianza tarehe 17 mwezi wa nane mwaka huu 2015, Kipindupindu ni Ugonjwa hatari unaoambukizwa kwa kula chakula au kinywaji chenye vimelea vya Ugonjwa “Vibrio cholera”ambavyo usababisha ugonjwa wa Kipindupindu, vimelea hivyo upatikana kwenye kinyesi, matapishi ya mgonjwa mwenye ugonjwa wa Kipindupindu au kwenye kituo chochote kilichochafuliwa na mgonjwa’ – Dr Seif
‘Ugonjwa huu unaweza ukasambaa kwa haraka iwepo kanuni za Afya hazitazingatiwa kama ifuatavyo ni kanuni hizo ambazo ninazitaja sasa ni zile zinazopelekea kupata Ugonjwa huo
1.Kutokunawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni kabla ya Kula au baada ya kutoka Chooni
2.Kula chakula kilichoandaliwa katika mazingira yasiyo safi na Salama
3.Kunywa maji yasiyo safi na salama
4.Kumuhumia mgonjwa mwenye dalili za ugonjwa huu bila kuzingatia kanuni za Afya juu ya kuepuka kupata maambukizi.
5.Waandaji na upikaji wa Chakula bila kuzingatia kanuni za Afya’ – Dr Seif
6.Usafirishaji Olela kwa wagonjwa wanaohisiwa kuwa wana Ugonjwa wa Kipindupindu ni vema kutoa taarifa iwepo kuna abiria mwenye dalili za ugonjwa huu ushauri namna ya kumsafirisha kwa namba ya Simu -0767300234 ili ushauri uweze kutolewa
Tangu ugonjwa wa Kipindupindu uanze tarehe 15 mwezi wa nane mwaka huu hadi kufikia tarehe 24 jana idadi ya wagonjwa walioripotiwa kwa mkoa wa Dar es Salaam ni 230 na vifo vya watu 7.
Idadi ya wagonjwa katika manispaa ni kama ifuatavyo
1.Kinondoni ni wagonjwa 186
2.Ilala ni wagonjwa- 22
3.Temeke ni wagonjwa 22
‘Aidha wagonjwa waliopo kwenye kambi za matibabu kwa tarehe ya jana 24 mwezi wa nane mwaka huu ni wagonjwa 71 mburahati 47, Buguruni wagonjwa 15 na Temeke wagonjwa 9′ – Dr Seif
‘Kwa taarifa zilizotufikia leo kwamba wagonjwa ambao wapo kwenye vituo vyetu hii leo katika jiji la Dar es Salaam ni wagonjwa 92, Kinondoni kukiwa na wagonjwa 65, Ilala wagonjwa 16 na Temeke wagojwa 11’ – Dr Seif
‘Katika Manispaa ya Kinondoni wagonjwa wengi wanatoka, Makumbusho, Kimara, Tandale,Goba, Kibamba, Manzese, Magomeni, Mwanyamala, Kijitonyama,Kigogo na Mburahati’ – Dr Seif
‘Katika manispaa ya Ilala maeneo yaliyoathirika au wanapotokea wagonjwa wenye vimelea vya Ugonjwa wa Kipindupindu yakiwemo Buguruni, Tabata, Chanika, Shaurishamba na Ilala, Katika manispaa ya Temeke ni Mtoni kwa Azizi Ally, Keko, na Yombo Vituka’- Dr Seif
Polisi wazuia ziara za Lowassa zisizo rasmi Dar es Salaam….
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es
salaam limepiga marufuku wagombea wa vyama vya siasa kufanya vitendo
vinavyo hatarisha usalama wa raia na mali zao kwa kufanya mikusanyiko
isiyo rasmi kwenye masoko na vituo vya daladala.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova.. ‘Sasa
kuna jambo limejitokeza ambalo limetulazimisha sisi jeshi la Polisi
kupiga marufuku wagombea mbalimbali wa vyama katika uchaguzi huu
hususani wale wenye nafasi ya Urais kwa vitendo vyao au kwa mtindo ambao
umeibuka sasa hivi wa kwanza kutembelea maeneo mbalimbali ya jiji la
Dar es Salaam kama vile vituo vya Daladala, Masoko, ndani ya Daladala au
Mabasi yoyote yale – Kova
‘Na hii inasemakana kwasababu ya kujua
matatizo ya watu ambao wenye kipato cha chini inawezekana nia ni nzuri
sana lakini sisi hapa atuzungumzia siasa au Uchumi hapa tunazungumzia
suala la Usalama kutokana na uzoefu uliojitokeza kwa zoezi hilo ni
kwamba hilo zoezi sio la rasmi pia ziara hizo zinasababisha mikusanyiko
mikubwa isiyo ya lazima katika hali ambayo inaashiria kutokuwepo kwa
Amani – Kova
‘Wakati wa
ziara wa aina hizo wamejitokeza makundi tofauti ya watu wakiwemo,
waendesha Bodaboda wengi, watu wa Daladala wengi wanajitokeza sawa
wanashangilia lakini kwa watu wengine ambao wasio wa makundi hayo ni
kwamba inakuwa inaleta taharuki, hofu, usumbufu, kuna kuwa na makelele
mengi, msongamano wa magari, au hata kusimamisha usafiri katika eneo
hilo ambalo mgombea anakuwepo nasema kwamba inawezekana huyo mgombea
kuna faida anayoipata lakini yeye kupata faida peke yake haitoshi kama
suala la usalama alizingatiwa’ – Kova
‘Kwa mfano
leo tarehe 25 mwezi wa nane ilibidi RPC wa kamanda Polisi Mkoa wa
Ilala, Lucas Mkondya alilazimika kukutana ana kwa ana na Mgombea Urais
kupitia Chadema, Edward Lowassa saa sita mchana watu walikuwa wamejaa
pale katika mtaa wa Congo nadhani na Uhuru misongamano ya Magari mengi,
Pikipiki wananchi wakalalamika kwamba ni nini sasa kinatokea na unajua
Dar es Salaam ukisimamisha magari kutokana na kundi lako kubwa basi
litawaathiri Wananchi’ – Kova
Hizi ni picha za Mesut Ozil na Miss Uturuki zinazozua hofu kuhusu ukaribu wao
Picha ambazo zimekuwa zikizunguuka katika vyombo vya habari mbalimbali Uturuki zikimuonesha kiungo wa kimataifa wa Ujerumani anayeichezea klabu ya Arsenal ya Uingereza Mesut Ozil ameonekana akiwa na miss Uturuki kitu ambacho kinazua maswali mengi huenda wanamahusiano ya Kimapenzi.
Taarifa hizo zinakuja ikiwa masaa kadhaa yamepita toka beki wa zamani wa klabu ya Manchester United Gary Neville ahoji kuhusu mchango wa kiungo huyo katika klabu ya Arsenal ya Uingereza kabla ya mechi ya Liverpool dhidi ya Arsenal ambayo ilimalizika kwa 0-0.
Behind the scenes ya video mpya ya Future ‘Where Ya At’ feat Drake isikupite mtu wangu.
Siku chache zilizopita niliisogeza kwako video mpya ya Future ‘Where Ya At‘ aliomshirikisha rapper ,wemgome maarufu Drake. Lakini baada ya video hiyo kutoka na kupokelewa vizuri na mashabaiki, Future kanona bora aendelee kutupa burudani
Rapper huyo karudi tena wiki hii kuweka
headlines zake kwenye kurasa za burudani, anaisogeza kwetu behind the
scenes ya video yake mpya.
Rasmi Juventus wamsajili nyota huyu kutokea Chelsea
Klabu ya Juventus ya Italia
bado inaongeza nguvu katika kikosi chake kwa kusajili wachezaji kadhaa
ili kuweza kuendana na kasi ya michuano mbalimbali itakayoshiriki msimu
huu. Juventus ambayo imeondokewa na nyota kadhaa kikosini mwake ikiwemo Carlos Tevez na Andre Pirlo imeongeza nguvu katika kikosi chake.
Juventus August 25 wamekamilisha usajili wa mkopo wa muda wa mrefu kwa aliyekuwa winga wa klabu ya Chelsea Juan Cuadrado ambaye alijiunga na Chelsea mwaka 2015 akitokea katika klabu ya Fiorentina ya Italia.
Pichaz Juan Cuadrado alivyowasili Italia August 24 kabla ya August 25 kutangazwa kusajiliwa
0 comments :
Post a Comment