Chris Brown anazidi kuonyesha mapenzi kwa mwanae, aamua kumpatia zawadi ya album!
Msanii wa R&B Marekani Chris Brown siku hizi amekuwa mtu wa kuspend muda mwingi sana na mtoto wake wa kike, kila atakapo kwenda basi na mtoto Royalty yupo nyuma, sio siri mtu wangu ni wazi kuwa Chris Brown anaenjoy sana kuwa na kuitwa baba.
Headlines za Chris Brown time
hii kwenye kurasa za burudani ni ujio wa album yake mpya ambayo
anategemea kuidondosha very soon, kizuri zaidi kuhusu album hii mpya ni
jina aliloipa ablbum hiyo!
Chris Brown kaamua
safari hii awape mashabiki wake kitu tofauti, kitu kitakachowagusa
mioyo ya mashabiki kama vile ambayo mtoto wake kaugusa moyo na maisha
yake… kupitia Twitter page yake Chris alichukua time na kuandika maneno machache yaliosema; “Album yangu mpya itaitwa ‘ROYALTY'”.
Tarehe ya uzinduzi wa album hiyo bado haijafahamika ila kwenye interview moja aliofanya Chris Brown na mtangazaji maarufu wa Radio Ryan Seacrest, Chris alizungumzia jinsi gani ambayo mtoto Royalty kayabadilisha maisha yake, jinsi ambavyo kamfanya atake kuwa baba bora na mwanaume bora.
Kwa sasa Chris ametoka kutengeneza video ya wimbo wake Liquor
siku chache zilizopita na very soon itasogezwa kwetu mtu wangu, lakini
kama hukubahatika kuusikia basi nimekusogezea wimbo huo hapa chini.
Rapper T.I kwenye headlines akwepa deni, vyombo vya Sheria vyamkalia shingoni!
Msanii maarufu wa hiphop kutoka Marekani T.I
anaziandika headlines siku ya leo, baada ya kukaa chini ya carptet
kwenye headlines za vyombo vya Sheria kwa muda, kwa bahati mbaya urafiki
wake na vyombo vya kulipa kodi ‘IRS’ vya Marekani upo matatani.
IRIS inamshitaki msanii huyo wa Hiphop maarufu kama The King of Atlanta kwa deni la dola Million 4.5 (zaidi ya Tzs. Billion 900 ) ya kodi, na hii itakuwa mara ya tatu kwa T.I kudaiwa kodi na IRS, mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2012 alidaiwa dola Millioni 1,397,283 na mwaka 2013 alidaiwa dola Million 3,173,476.
Mwaka 2014 T.I alikuwa salama kabisa IRS haikuwa na cha kumdai lakini mwaka huu mambo hayajaenda vizuri, IRS
imekuja juu na kudai kuwa msanii huyo alilipa kiasi cha fedha za kodi
lakini kwa miezi kadha amekuwa akilipoteza deni lililobaki la dola Million 4.3 na wanashangazwa anavyofungua biashara mpya kila kukicha lakini kulipa hiyo Millioni 4.3 inakuwa tatizo.
Kwasababu hiyo T.I yupo matatani kufilisiwa baadhi ya mali zake kwani IRS
imesema kama akiendelea kukwepa kulipa deni hilo basi watalazimika
kusimamisha baadhi ya biashara zake ama kuuza baadhi ya mali zake ili
kurudisha hela wanaomdai msanii huyo.
FC Barcelona Vs Athletic Bilbao, matokeo yapo hapa (Picha
Klabu ya FC Barcelona imeshuka uwanjani kucheza mechi yake ya kwanza Ligi Kuu Hispania, FC Barcelona imeingia uwanjani kucheza na klabu ya Athletic Bilbao ikiwa ni wiki moja imepita toka ipokee kipigo kutoka kwa Athletic Bilbao katika mchezo wa Super Cup.
August 23 FC Barcelona imerudi kucheza mechi ya Ligi Kuu na Athletic Bilbao ila imefuta uteja wa kukosa ubingwa wa Super Cup ila katika mchezo wa Ligi Athletic Bilbao imekubali kipigo cha goli 1-0, goli pekee la dakika ya 54 kutoka kwa Luis Suarez liliwafanya FC Barcelona kuondoka na point 3 muhimu.
Nimekusogezea matokeo ya mechi ya Everton Vs Man City (Picha
Klabu ya Manchester City imeshuka dimbani August 23 katika uwanja wa Goodson Park kukipiga na mwenyeji wake klabu ya Everton katika mechi ya Ligi Kuu, Man City bado inaendeleza wimbi la ushindi kwani imecheza mechi tatu na kushinda zote, Man City imeifunnga Everton kwa jumla ya goli 2-0.
Magoli ya Manchester City yalifungwa na Aleksandar Kolarov dakika ya 60 na baada ya hapo kiungo wa kimataifa wa Ufaransa Samir Nasri kufuatia kupachika goli la mwisho mnamo dakika ya 88 ya mchezo na kuifanya Man City kuwa na jumla ya point 6.
Hizi ni picha za mchezo
Pedro aanza na bao Chelsea.
Mchezaji mpya wa Chelsea Pedro Rodriguez ameanza maisha mapya ndani ya klabu yake mpya baada ya kuifungia bao moja huku akitoa pasi ya mwisho kwa bao lingine katika mchezo wa ligi kuu ya England ambao Chelsea ilishinda kwa matokeo ya 3-0.
Pedro alisajiliwa na Chelsea katikati ya wiki iliyopita alifunga moja kati ya mabao matatu ambayo yalifungwa na wachezaji raia wa Hispania ndani ya Chelsea ikiwa ni ishara ya matunda ya usajili ambao Chelsea imeufanya .
Ushindi huu dhidi ya Westbromwich Albion unakuwa ushindi wa kwanza kwa Chelsea msimu huu baada ya timu hii kuanza ligi kwa kasi ya chini ambapo walifungwa na Manchester City huku wakitoka sare kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya Swansea .
Picha 30 za mwanzo kutoka Jangwani katika uzinduzi wa kampeni za CCM 2015
Tanzania imeingia katika mwaka wa
uchaguzi na hivi karibuni kila chama cha kisiasa kilichoamua kusimamisha
mgombea wa kugombea nyadhifa mbalimbali za kisiasa vinajiandaa kuzindua
kampeni zake rasmi. August 23 ni siku ambayo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeamua kuzindua kampeni zake rasmi kuelekea uchaguzi mkuu wa Urais, Ubunge na madiwani Oktoba 25
Nimekusogezea picha 30 za kinachoendelea Jangwani
0 comments :
Post a Comment