TASABA HABARI KAMILI

Lipumba na CUF sasa basi, UKAWA watikiswa Lowassa kuwapasua? Wasanii na kikao cha TCRA? 

news-1
Magazeti ya Ijumaa 7 August 2015 yako mtaani tayari na vichwa vyake vikubwa vya habari, kazi yangu ni kukusogezea zile zote zinazoweka headlines magazetini… baadhi zikiwa na hizi kubwa kubwa.

Prof. Ibrahim Lipumba ango’ka hali tete UKAWA, ajiuluzu uwenyekiti wa miaka 16 CUF akimpinga Edward Lowassa adai UKAWA washindwa kuenzi uadilifu na uzalendo.
CCM kupitisha wagombea Ubunge leo…Edward Lowassa aipasua vipande UKAWANEC yaonya kampeni nyumba za ibada…Siri yafichuka CUF watoa taamko…na mke wa Dk. Wilbroad Slaa afunguka.

UKAWA wapata mtikisiko mkubwa baada ya Prof. Ibrahim Lipumba kujiuzulu uwenyekiti wa chama cha CUF na kuamua kubaki kuwa mwanachama wa kawaida wa Chama hicho…idadi ya Wabunge 51 waanguka kura za maoni ndani ya vyama vyao.
Zaidi ya majambazi 10 waliohusika na tukio la Sitakishari wakamatwa na Polisi…Wamachinga wanaendelea na ujenzi wa vibanda Jangwani pamoja na Serekali kusisitiza kuwa wanapaswa kuhama eneo hilo.

Wasanii waingia mitini kwenye kikao kilichoandaliwa na idara ya mawasiliano TCRA na kati ya wasanii 70 walioalikwa waliofika ni wasanii sio chini ya 20.
Sauti ya uchambuzi wote wa magazeti @Cloudsfm nimekurekodia na kukuwekea hapa chini.

 

Share on Google Plus

About Unknown

TEAM TASABA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment