Hivi ni viatu na gloves maalum Juma Kaseja katengeneza kwa ajili yake(Picha)
Golikipa mkongwe katika soka la Tanzania ambaye amecheza kwa kiwango cha juu kwa muda mrefu Juma Kaseja amerejea tena katika soka baada ya kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi sita. Kaseja amerejea uwanjani na amesajiliwa na klabu ya Mbeya City hivyo msimu ujao tutamuona langoni.
Katika maandalizi ya kurudi langoni Kaseja ametengeneza viatu maalum kwa ajili yake hivyo usishangae kumuona akiwa langoni na viatu vyenye jina lake Kaseja Coper 1 pamoja na gloves. Kaseja ametoa exclusive hiyo kwa millardayo.com ila amegoma kutaja gharama ya aliotumia kutengeneza viatu hivyo.
Kaseja ambaye amewahi kupatiwa jina la Tanzania One
kutokana na umahiri wake awapo langoni Je ni mpango wake kufanya
biashara ya vifaa vya michezo kwa kutumia jina lake jibu ni kuwa
ametengeneza kwa ajili yake pekee.
T.I & Young Thug washirikiana kuisogeza kwetu ‘Off-Set’.
T.I na Young Thug wanaziandika headlines za burudani kwa mara nyingine tena, baada ya kufanya kazi pamoja mwaka 2014 kwenye wimbo wa ‘About the Money’ time hii wanaisogeza kwetu ‘Off-Set’.
Kitu kizuri kuhusu video hii ni kwamba wimbo wa ‘Off-Set‘ ni moja kati ya soundtracks za movie ya Fast Furious 7, na kama bado hujabahatika kukutana na video ya wimbo huo karibu uitazame hapa.
Sentesi za UKAWA baada ya LOWASSA kuzuiwa kufanya ziara mitaani..
Leo James Mbatia amezungumza na
Vyombo vya habari kuhusu hatma ya uzinduzi wa kampeni zao ambazo
zitafanyika August 29, Dar es salaam pamoja na mambo mengine mbalimbali
ndani ya UKAWA ikiwemo issue ya Mgombea wao Edward LOWASSA kuzuiwa kufanya ziara mitaani.
Hapa nimekuwekea baadhi ya Sentesi alizozungumza wakati wa Mkutano huo na waandishi wa habari…
Taylor Swift akataa kutoa show ya billion 4.4 kwa sababu hii hapa
Headlines kutoka Marekani zinaandikwa na superstaa wa muziki wa R&B Pop Taylor Swift
baada ya taarifa kusambaa kuwa amepiga chini dili ya kutoa show kwenye
harusi ya Billionea, dili ambalo lingempatia superstaa huyo kiasi cha Billion 4.4 (USD 2 Million).
Kutokana na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao, Taylor Swift alipewa ofa ya kulipwa dola Million 1 (Billion 2.2)
kwa kila wimbo ambao angependa kuuimba kwenye harusi hiyo na bonus
nyingine ya pesa kama angechukua time kukaa na kupiga stori na bibi na
bwana harusi… lakini bado staa huyo aliipiga chini ofa hiyo.
Sababu zilizowekwa wazi na baadhi ya blogs zinasema kwamba Taylor Swift aliikataa ofa hiyo kwa ajili ya kwenda kuimba bure kwenye ubatizo wa mtoto wa rafiki yake ambako Taylor ni mama wa ubatizo wa mtoto huyo.
Taylor
Swift na mtoto wa Kyle Newman ‘Leo’. Taylor alikutana na mtoto huyo
kwa mara ya kwanza baada ya kutajwa kuwa mama wa ubatizo.
Kwenye ubatizo huo Taylor Swift alienda na boyfriend wake Calvin Harris na bendi yake na kutoa show ya nyimbo zake kali zikiwemo; Love Story, I Knew You Were Trouble na Red.
Taylor Swift na rafiki yake Kyle Newman.
0 comments :
Post a Comment