Di Maria aeleza tatizo lililomfanya ahame Man United na kujiunga na PSG……
Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina aliyekuwa ana kipiga katika klabu ya Manchester United kabla ya kutimkia klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Angel Di Maria, ameeleza sababu za yeye kulazimisha kuhama katika klabu ya Manchester United.
Di Maria ameeleza kuwa moja kati ya vitu vilivyomfanya asikubali kuendelea kubakia katika klabu ya Manchester United, ni falsafa za kocha wa klabu hiyo Louis van Gaal
ambaye alikuwa akimpanga nafasi ambayo yeye hakuwa na uzoefu nayo,
hivyo ni kitu ambacho kilikuwa kinapelekea yeye na kocha huyo kupishana
kauli wakati mwingine.
“Falsafa
alizokuwa nazo Van Gaal ni moja kati ya sababu zilizonifanya nihame
Manchester United ni ngumu kuzielewa falsafa zake, nilikuwa nikipishana
naye kauli mara kadhaa. Nilizungumza na Blanc na ninaamini nitacheza
namba yangu ambayo nilikuwa nacheza katika klabu ya Real Madrid hivyo
nikahamia PSG” >>> Di Maria
Kiungo huyo alijiunga na Manchester United msimu uliomalizika, hivyo baada ya kwenda likizo hakurudi tena katika maandalizi ya msimu mpya, hadi pale Van Gaal alipokiri kuwa hafahamu alipo mchezaji huyo na siku kadhaa baadae uhamisho wake kwenda PSG hukawa umekamilika.
Saa kadhaa kabla ya dirisha la usajili kufungwa Southampton yaweka kikao na Mkenya huyu…
Klabu ya Southampton ya Uingereza bado inahangaika namna ya kumzuia kiungo wa kimataifa wa Kenya anayeichezea klabu hiyo Victor Wanyama asiihame Southampton, kupitia mtandao maarufu wa habari za michezo wa goal.com umeeleza namna ya viongozi wa klabu hiyo walivyo kaa kikao na Wanyama na wakala wake ili asihame.
Wanyama ambaye siku ya August 28 aliomba uongozi wa Southampton umuuze, hakuwa sehemu ya timu iliyoshinda goli 3-0 dhidi ya Norwich, kocha wake Ronald Koeman alisema Wanyama hakucheza mechi hiyo kwa sababu hakuwa fit kiakili na kimwili hivyo isingekuwa rahisi kwake kumpanga.
Kiungo huyo wa Kenya ambaye amebakiza mkataba wa miaka miwili klabuni hapo toka pale alipojiunga mwaka 2013 akitokea klabu ya Celtic ya Scotland, anahusishwa kuhamia katika klabu ya Tottenham Hotspur, sasa bado haijajulikana kama klabu hiyo itamruhusu ahame katika dakika za mwisho kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.
Usajili wa De Gea na Navas waelekea kukamilika usiku huu...
Baada ya kujaribu kumsajili De Gea kwa muda wote wa dirisha la usajili hatimaye Madrid wamefikia makubaliano na United juu ya usajili wa David De Gea kwenda Santigo Bernabeu katika dili ambalo linatajwa kumhusisha Keylor Navas kuhamia Old Trafford.
Usajili huo bado haujakamilika lakini inaripotiwa Madrid watailipa Manchester United kiasi cha 40m euros (£29m).
Kwa muda wote wa dirisha la usajili Man United imekuwa ikisisitiza kulipwa ada ya uhamisho itakayovunja rekodi kwa uhamisho wa magolikipa au dili hiyo imhusishe Sergio Ramos, lakini mwisho wa siku Kylor Navas ndio ataenda Theater of Dreams.
Liverpool yamsajili mshambuliaji huyu kutokea Nigeria……….
Klabu ya Liverpool ya
Uingereza haiko nyuma na yenyewe kumalizia masaa ya usajili yaliosalia
vizuri, kila klabu ina angaika ili iweze kusajili mchezaji iliyekuwa
inamtaka kwa muda mrefu au inasajili mchezaji ambaye ni mbadala wa yule
ilio mkosa. Jioni ya August 31 klabu ya Liverpool imetangaza kumsajili Taiwo Awoniyi.
Liverpool imemsajili Taiwo Awoniyi ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Nigeria amezaliwa mwaka 1997 na alikuwa akichezea timu ya taifa ya Nigeria ya umri chini ya miaka 23 lakini imempeleka kwa mkopo katika klabu ya FSV Frankfurt ya Ujerumani.
Baada ya Januzaj, Chicharito nae aondoka Man Utd
Adnan Januzaj ameondoka rasmi Manchester United
Baada ya jana kumpeleka kwa mkopo Tyler Blackett kwenda Celtic, Jonny Evans kwenda West Brom, leo hii imethibitishwa Adnan Januzaj amepelekwa kwa mkopo katika klabu ya Dortmund ya Ujerumani.
Wakati huo huo Manchester United leo imefanyia vipimo vya afya Mshambuliaji Anthony Martial kutoka klabu ya As Monaco ya Ufaransa.
Masaa kadhaa kabla ya kufungwa kwa usajili hawa ndio wachezaji waliowahi kusajiliwa dakika za mwisho....
Tukiwa tunaelekea kufungwa kwa dirisha la usajili wa Ligi Kuu Uingereza,
nimeona nikukumbushe wachezaji watano waliowahi kusajiliwa kwa fedha
nyingi saa chache kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.
Mesut Ozil – 2013
Ikiwa saa kadhaa zilikuwa zimesalia kabla ya dirisha la usajili kufungwa Uingereza mwaka 2013, klabu ya Arsenal iliridhia kutoa pound milioni 42.4 kumsajili kiungo wa Kijerumani aliyekuwa katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Mesut Ozil na kuvunja rekodi ya usajili ya klabu hiyo.
Fernando Torres na David Luiz 2011
Baada ya misimu mitatu ya mafanikio katika klabu ya Liverpool Fernando Torres mwaka 2011 alijiunga na klabu ya Chelsea ya London kwa pound milioni 50 kwa wakati huo ilikuwa ni rekodi kubwa ya usajili kwa vilabu vya Ligi Kuu Uingereza. Lakini Torres alishindwa kuonyesha makali yake Chelsea kwani alicheza mechi 110 na kufunga goli 20. Siku hiyo hiyo aliyosajiliwa Torres ndio siku aliosajiliwa beki wa Kibrazil David Luiz akitokea Benfica ya Ureno.
Dimitar Berbatov 2008
Mwaka 2008 klabu ya Manchester United ilikamilisha uhamisho wa pound milioni 30.75 kwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Bulgaria Dimitar Berbatov kutokea klabu ya Tottenham Hotspur, hata hivyo uhamisho huo ambao ulifanywa na Man United ilikuwa ni sawa na wao walivyozidiwa kete na Chelsea kwa Pedro kwani Berbatov alikuwa ajiunge na Man City kabla ya Ferguson kumdaka Uwanja wa ndege.
Andy Carroll na Luis Suarez – 2011
Mwaka 2011 kocha wa zamani wa klabu ya Liverpool Kenny Dalglish aliwasajili kwa pamoja Andy Carrol kutokea klabu ya Newcastle United na Luis Suarez akitokea klabu ya Ajax ya Uholanzi.
Andrei Arshavin – 2009
Andrei Arshavin mshambulaiji wa kimataifa wa Urusi aliyetua katika klabu ya Arsenal ya Uingereza kwa pound milioni 15 Zenit, licha ya Arshavin kushindwa kutamba katika klabu ya Arsenal na kitu pekee kikubwa alichowahi kufanya ni kuifunga Liverpool magoli manne.
Hiyo ndio kumbukumbu ambayo
nimekukumbusha mtu wangu kwani hadi sasa tunategemea kuona lolote
likitokea katika masaa machache yaliosalia ili kufungwa kwa dirisha la
usajili la Ligi Kuu Uingereza.
0 comments :
Post a Comment