Nimekusogezea matokeo ya Arsenal vs Newcastle na Man City vs Watford
Wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Etihad, City wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya timu iliyopanda daraja la Watford.
Raheem Sterling aliyenunuliwa kwa ada ya £49m kutoka Liverpool leo alifunga goli la kwanza katika msimu mpya Barclays Premier League na Fernadinho akifunga goli lingine.
Arsenal vs Newcastle
Goli pekee lilofungwa na Alexander Chamberlain lilitosha kuipa Arsenal ushindi dhidi ya timu ngumu ya Newcastle katika mchezo uliofanyika mapema leo mchana katika uwanja wa St James Park.
Full time ya Liverpool vs West Ham nimekuwekea hapa
Wakicheza kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Anfield – Liverpool wamepoteza mchezo wao wa kwanza msimu huu baada ya kukubali kipigo cha 3-0 kutoka West Ham.
Magoli ya West Ham ambao walifungua ligi kwa kuifunga Arsenal – yalifungwa na Lanzini katika dakika ya 3, Noble akaongeza la pili dakika ya 29, Sakho akafunga biashara kwa kushindilia msumari wa mwisho dakika ya 90.
Vikosi vilipangwa hivi: Liverpool: Mignolet, Clyne, Skrtel, Lovren, Gomez (Ibe 78), Can (Moreno 45), Lucas, Milner, Firmino (Ings 61), Benteke, Coutinho.
Subs not used: Sakho, Origi, Bogdan, Rossiter.
Booked: Lucas, Ings, Clyne.
Sent off: Coutinho 52.
West Ham: Randolph, Tomkins, Reid, Ogbonna, Cresswell, Kouyate, Obiang, Noble (Oxford 81), Lanzini, Sakho (Cullen 90), Payet (Jarvis 88).
Kilichoikuta Chelsea vs Crystal Palace hiki hapa
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Stamford Bridge umemalizika kwa Crystal Palace kuharibu rekodi ya Mourinho kutopoteza mechi katika dimba la nyumbani.
Mechi hiyo imemalizika kwa matokeo ya ushindi wa 2-1 kwa Palace inayofundishwa na kocha wa zamani wa Newcastle – Alan Perdew.
Sako alianza kuifungia Palace goli katika dakika ya 65, kabla ya Radamel Falcao kusawazisha katika dakika ya 79.
Dakika ya 81, James Ward aliifungia Palace goli la ushindi na kuzidi kuiharibu rekodi ya Mourinho katika uwanja wa nyumbani ambapo leo alikuwa anatimiza mechi ya 100 tangu alipoanza kuifundisha tena timu hiyo.
0 comments :
Post a Comment