Lowassa na Magufuli kimyakimya? NEC matokeo ni ndani ya siku 3!? Nkurunziza aapishwa!?
Ni ijumaa nyingine na uchambuzi wa
magazeti @CloudsFM umefanyika, ninazo zile zote zilizotawala kwenye
vichwa vya habari na kuguswa na Uchambuzi wa Redioni.
Hofu imetanda kwa watumiaji wa magari na mitambo nchini kutokana na taarifa ya uwezekano wa bei ya diesel na Petroli kupanda… Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewataka viongozi wa Siasa kuacha kuwatumia walezi wao kwenye kampeni za Kisiasa.
Lowassa na Magufuli kurudisha fomu za Ugombea Urais kimyakimya…. James Mbatia asema UKAWA
wataendelea kusonga mbele licha ya tofauti na changamoto zao na
anayetaka kuondoka kwenye Umoja huo ana haki ya kufanya hivyo bila
kuzuiwa na mtu.
NEC yaonya siasa kwenye
nyumba za ibada, yawapiga marufuku viongozi wa dini kufanya kampeni za
kisiasa kwenye nyumba za ibada… NEC imesema safari hii matokeo ya Urais
kutangazwa ndani ya siku 3.
Wagonjwa wa Kipindupindu wafikia 56 Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar amewataka watu wa Dar kuacha kusalimiana kwa mikono kwenye kipindi hiki ili Jambazi sugu wa tukio la Sitakishari atajwa.
Moja kutoka Burundi yasema Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
aapishwa ghafla jana kutumikia muhula mwingine wa miaka 5 na hakuna
mgeni wa nchi za nje aliyehudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais huyo.
0 comments :
Post a Comment